Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Beberu akiona kundi la mbuzi kilometa 3 hafikirii hata sekunde anaanza mbio ili aonje hata jike moja ambalo hajawahi kulipanda. Mbuzi wengine wanaanza kumfukuzia ila wakikutana na shamba la mtu wanaanza kufyeka mazao kwanza na safari inaendelea.
Na wakianza kukimbia unatakiwa uwe mwehu Kwa mda kuweza kuwacontrol
 
Wanapenda mazao ya watu utasema wanajua kulima. Niliwahi kumpiga mmoja ñusura nimuue baada ya kuwaongoza wenzake kula mazao nikapigwa halafu ile nimekaa nasikilizia maumivu kakaja kakanipigia chafya usoni
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa mbuzi mbona umeenda mbali sana?

"Siku ukiwa na jirani Muhaya halafu awe alitumbuliwa kwenye sakata la vyeti feki" ndiyo utajua kwamba kwanza umekuwa mtu mzima pia kiwango chako cha uvumilivu kwenye mambo ya kijinga siyo cha level ya kawaida.
 
Ukiwa na akili timamu sio rahs kukaa na mbuzi 😁
 
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mbavu sina
 
Halafu bora kuchunga mbuzi wakiwa wengi.. wakiwa wachache tatizo linakuwa kubwa zaidi maana usumbufu unakuwa usioelezeka. Pia ukiambiwa uwapeleke mnadani bora upewe kundi la ng'ombe kuliko mbuzi mmoja. Hadi mfike mnadani umesota.
Kwann unasota mkuu?[emoji38]
 
Kuna hawa wa kufunga na kamba aisee akikata kamba atakupigisha tizi ya kiwango cha SGR, usipokuwa makini unaweza gongwa na gari mana mwenzio anavuka road Kwa speed ya mwanga
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]ha ha ha....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…