Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Ulivyoandika na nilivyousoma huu uzi asee kweli hawa viumbe wanatesa...

Wakiamua kula mahindi yako sasa uliyoyaanika yapigwe na jua...afu unatoka shambani njaa kali πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ asee utasema walikuwa wanakusubiri ndio wale mahindi yako.
 
Ao wajinga wanakuaga na kiongoz wao mjinga kuliko wako wao, yani ukiwafungua tu ye anaongoza to njia kwa speed kwenda kula mazao ya watu, dawa yao kamba asa iyo kamba ukute wako wa 3 ndo shughuli inakua ngumu mara wakuvute uku mara uku wakikushinda ujue kesi iyo, mazao ya watu washakula,

Basi nilikua nkiwatuliza kimbelembele na mfunga kamba kwenye lisho alafu namtia fimbo nyingi hadi asira yangu ipoe.... Kuna wakati kimbelembele alikua beberu mkorofi ukimchapa anageuka anaruka anataka akupige, basi nkawa nampa kolabo mwanangu mmoja, nafimbo zetu ndefu mmoja mbele mwingine nyuma akigeuka akupige fimbo akigeuka uku fimbo.....

Ila mikoa mingine noma Mbuzi 50 walipikutika mwezi mmoja, yani mbuzi anapatwa na kichaa, ukimpasua unakuta hadi irizi,

Pia kuna watu noma, waroho ata mbuzi kajifia hadi anaanza kuaribika ila wanakula tu....
 
Nimewavunja sana hao miguu, mbuzi na ng'ombe nimechunga sana.
Bora ufuge kondoo kuliko hao vicheche.

Wakishazoea kulisha shamba fulani, ukiwa njiani unawaswaga wanatimua mbio hata kama ni umbali wa kilometa 3 mbele. Inabidi ukimbizane nao na lazima utakuta wameshaharibu tu.

Raha ya kufuga hao ni nyama, baba alikuwa akichinja kila wiki mbuzi.

Nb: ukitaka kuwa mfugaji wa hutu "tushenzi" basi uwe na eneo kubwa vinginevyo kila siku utaitwa kwa mwenyekiti au mtendaji kujibu mashitaka ya kuharibu mazao ya watu.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wanapenda mazao ya watu utasema wanajua kulima. Niliwahi kumpiga mmoja Γ±usura nimuue baada ya kuwaongoza wenzake kula mazao nikapigwa halafu ile nimekaa nasikilizia maumivu kakaja kakanipigia chafya usoni
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] pole mkuuu

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Huku mbagala Kuna mbuzi kibao wanazurura tu Kama hawana mwenyewe. Wanakula chochote Hata andazi.
Wezi wanaogopa kuwaiba eti wanadai ukliba ukachinja na kula, unaanza kulia Kama mbuziπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Samahani:
Hivi ushawahi funga KONDOO?

Ushawahi wakuta ule ukiburi wao waki inamisha vichwa chini?

Kati ya mbuzi na Kondoo, basi kondoo ni mchafu zaidi, ni anakiburi zaidi alafu kiburi cha kimya kimya.

Alafu akili zao wanazijua wenyewe wakiamua jambo lao.

Nawashangaa sana wanakubaligi kuitwa MAKONDOO kanisani.
 
Mbuzi we Acha tuu , ukifuga hawa lazima ukumbane na kesi za mazao Kula miti ya watu , ni swala la mwez mmoja tuu majirani wote hamuongeleshani
 
Sipatii picha kiko kichwa chako πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…