Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Aiseee..
 
Waliwah kumuaibisha mzee mmoja,walikuwa na kamba afu akawashika kwa pamoja ili akawafunge malishoni,sasa ile tabia yao ya mwingine anaenda huku,mwingine mbele mwingine nyuma mzee akawa amekomaa kuwashikilia ili wasimkimbie alijikuta wamemfunga miguu akakosa balance akajipiga chini
 
Nishawah kulea kamoja mama yake alikufa
Kila napoenda kako miguun nikienda dukan ananifata nikimuacha nikamfungia analia balaaa
Nikilala anakuja kuniamsha
Nilikuwa namnywesha maziwa na kumuogesha nilimpenda sana alivyojua akachukuliwa
 
Pamoja na mabaya yote,mnayoeleza, kijana ukitaka kutoboa Maisha haraka achana na kufunga kuku ,fuga mbuzi. Haeagi haraka , wanazaliana kwa wingi na chakula chake ni Cha bure. Tafuta Kambi weka uzio Anza kuwafuga
 
Kipindi tukiwa na mbuzi wengi,ilitokea kambuzi kamoja kadogo dogo kakazaa ila kakawa hakataki kumnyonyesha mwanae,ile kukachunguza vizuri tukagundua matiti yake yalikuwa magumu na ukiyakamua yanatoa vitu vizito vizito hv,basi ikabid tuachane nako

Ikabid kile kitoto tuanze kukipatia maziwa ya ng'ombe baada ya muda kilinenepa kweli na kikawa kinashinda ndani kama paka hadi tukawa tunakivalisha nguo na cheni ya kimsalaba tulikifunga shingoni

Pale nyumban kile kimbuzi tulikipenda sana,ilikuwa mtu akichukua lile kopo lake la kukanyweshea maziwa ukikaonesha kanakufata kwa kukimbilia kakizani unataka kukipatia maziwa,chuchu yake tulikuwa tunatumia zile kopo za mafuta ya cherehani

Siku moja wakati kameshaanza kuchangamka kakawa kanapiga misele ya nje na nyumbani,bahati mbaya kakagongwa na gari na kakafariki pale pale,kwanza waliokaona walishangaa kuona mbuzi ana cheni
Siku hyo tulipata huzuni sana pale nyumban,tulikazika na tukakatengenezea kaburi,tulipata shida sana kuzoea kwamba hakapo tena nyumban
 
Kwa sisi waislamu tunafundishwa kuwa kwanini Mungu alituma mitume na hao mitume asili ya kazi zao ilikuwa kuchunga mbuzi na wanyama wengine.

Tunafundishwa kuwa Allah aliwaandaa hawa mitume kwa kuwapa kazi ya kuchunga wanyama kwanza kabla ya kuwapa utume ili wawe na mioyo ya uvumilivu ili waweze kulea na kuhamiliana na wanadamu watakao kuwa wanawaongoza.

Tazama historia ya mitume wengi utaona kazi zao wa uchungaji wa wanyama na hasa mbuzi.
Allah alijua kuwa ikiwa wataweza kuchunga wanayama na hasa mnyama msumbufu na kisirani kama mbuzi basi kwa binadamu itakuwa rahisi.
 
Ha ha ha.....kama nakuona vule[emoji1787]
nmetamani nitembelee jamii za wafugaji nijionee hivi vituko[emoji38]
 
Ha ha ha ......hawa wadudu ni wasumbufu pro max[emoji38]
 
Ni kosa kubwa mno kuwaburuza wote Kwa pamoja kwenda kuwafunga , huwa wanakataa kabisa , na ukigeuka kuangalia Yani unaona kabisa Kwa kiburi na dharau hataki , aheri umchukue mmoja mmoja japo Napo ni kibembe tuu , kuja kumaliza kumfunga ushampiga vibao vya kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…