Kwa sisi tatizo ni muundo tu wa uongozi huwa unategemea aliyebeba kofia ya chama na si raia kwa ujumla. Tunajiita democratic country ila its obviously a mix of Monarchy and Oligarchy na ili kuubadili huu muundo tunahitaji revision ya katiba.
Muundo huu wa kutukuza fikra za mwenyekiti ndio umetufikisha hapa tulipo na hali itazidi kuwa mbaya sababu sauti na nguvu ya umma imebakwa completely. Kibaya zaidi ili u survive kwenye mfumo wa aina hii ni lazma uwe mpambe wa Mwenyekiti na umtukuze yeye no mara waah. Yeye ndio alfa na Omega na ukionekana unataka kuleta any crazy ideas you are doomed sababu anamiliki heads wa mihimili yote ya serikali, heads wa mashirika yote, heads wa mamlaka zote, heads wa majeshi yote. Kiufupi he/she has absolute power which is completely absurd.
He/She can make orders to make your life miserable in a fraction of seconds. Tunaishi ndani ya huo mfumo na ndio maana inapotokea mtu ana nafasi hawezi kufikiria kufanya vitu kwa utaratibu ambao ni contrary na anavyotaka aliyempa nafasi. You want to live to see the better days then take orders and do things that will never irritate the big boss hata kama vitaumiza umati wa raia.
Mimi siwalaumu ambao wana nafasi kufanya wanayofanya sababu naelewa fika tatizo liko wapi. Tunabaki kulaumiana tu ila ukipata nafasi you would do exactly the same. Hatuna katiba inayoruhusu independent thinking na uwajibikaji this is the main culprit na ndio maana tunategemea uzalendo wa kiongozi ndio uamue fate yetu. Kiongozi asipokuwa na uchungu na taifa ndio kama hivyo tena mambo hayawezi kuwa sawa. Ukionekana cheerleader wa mabadiliko you are as good as dead man. Nani kati yetu hataki kuishi???