Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Mzee Bongo Zozo kashavuta yake na anapeta mtaani hebu watu tuchukue mamuzi.magu tuhudumiane wenyewe,ziletwe gari zipigwe bei tusisubiri wapika pilau la clean energy waje kutusaidia hili jambo.I swear the problem isn't over yet.
Niliona siku nikajua anazingua tu, alikua na Toyota BZ4x EV.
Toyota ujanja mwingi ila kwenye EV anaogopa. Wajapan wote EV wanaingia kwa mguu nusu, wengi wanashirikiana na Mchina kufanya maajabu sio wenyewe.
 
Haha mkuu ni kweli inabidi kuangalia vitu vingine vidogo dogo kwenye EV au kubadili kwenda kwenye tyres services kwani huko hata EV zitatumia tyres tu.

Mkuu upande wa fake Tanzania sio Oil pekee, kuna nguo, simu na hata dawa fake mkuu. ni kuwa makini na kujua unachonunua.
 
Sure. Ila bors nguo fake au kiatu. Imagine soil fake. Dah
 
😅😅😅 mie Traffic waliniandikia ingaw ktk 50 natembea na 50, kuna sehem nilijichanganya ktk 50 nikaw nipo na 75 hivi..

Kumpa leseni akaandika nime overspeed basi nikakubali matokeo.. Nilivyofika Mjini nikalipa siku hiyo hiyo.

Mie 200 mpk 215 nafika nikiwa nafanya test (kupima Kifua), hii gari speedometer yake ni 180 ila Engine yake haina limiter inafika 180 mpk inalala chini (inabaki uwezo wa Engine kuperform) so kwa kutumia Digital Speedometer na Real time GPS najua current speed nayokuw nayo wakati wa testing.
 

Uko sahihi Mkuu, nimetaja oil Kwa sababu tunaongrlea magari, hakuna eneo tuko salama. Hata kile kitu unachouziwa ghali Kwa kuambiwa ni original ndio uwe makini zaidi.

Tunaua gari sana Kwa oil fake. Unashangaa umefanya service hata mwezi haujaisha na umeenda kilometer chache tu, inaanza kutoa milio ya kukoroma. Ni hatari.

Kweli kiongozi Kwa Sasa anza kufuatilia kidogo kidogo kuona Kuna fursa zipi zinakuja na EV.
 
Umeme wa kuchaji upo? Huwezi kuchaji na huu umeme wa nyumbani.
 

Kaka hongera, hiyo 200 nna ifikia hapa usifikiri ni Kwa hiari, ilikua nafukuzia STM naona naenda tu, kutazama mshale kisahani kinasoma 200. Hapo siongei wala kupepesa macho. Wameandika inaenda Hadi 260.

Lakini hadi Sasa, speed nzuri yenye amani, furaha na baraka zote zikiwemo za serikali, 80-100 ni Bora zaidi.

Kwenye trafiki nashukuru Kwa Sasa siwezi ingia nao mgogoro. Tunawashiana taa tu Kwa mbali.
 
Kwa barabara ya Morogoro kuna kipande cha UBENA ZOMOZI... hapo ndio sehem yangu sasa ya kujidai.. kwa hii ya Kaskazini ni huku katikati Makanya Makanya huku..
 
Mie nilishangaa😅 IST ya cc 1500 kwa safari ya DSM to Arusha napishana nayo liter 5-8 tu za mafuta, nikiwa na jiko la cc 2000.
IST inaweza kwenda hadi 17.20 per litre lakini hapa tuna-assume unatembelea gia za juu(means uko kwenye barabara flat) sasa hii ni rare case
Kwa kawaida ni 14km/L

Toyota IST 2012/6: Grade
Model CodeDBA‐NCP110‐AHXEK
Engine Capacity1,496
Number of Seats5
Fuel Consumption17.20km/L
 
Bongo ni vurugu tupu ni muhimu kuwa makini usiingizwe kingi.

Mkuu una kacheo kwenye serikali ya kizimkazi?😄 Hao jamaa wa road bila wadhifa fulani hawakuachi kizembe namna hiyo.
 
Kwa barabara ya Morogoro kuna kipande cha UBENA ZOMOZI... hapo ndio sehem yangu sasa ya kujidai.. kwa hii ya Kaskazini ni huku katikati Makanya Makanya huku..

Kwenye zile shamba za mkonge Kwa Morogoro ipo vizuri sana.

Kuna siku nilipita Nzega Manyoni kupitia Tabora, Ile barabara Iko vizuri sana.

Binafsi naangazia EV au hybrid za Volvo miaka ijayo. Zishuke shuke Bei kwanza.

Faida niliyonayo ni exemption kwenye Kodi. Na kama hakuna uchakavu, ntalipa registration na port charges kidogo sana. Unaona kabisa Kuna motisha ya kumiliki gari ya kueleweka.
 
Na hiyo rate ni straight from kiwandani.. sasa ambayo tyr ishatembelewa kwa kms 80-100k, maintenance ya kuunga unga m sure inashuka kutok 17kpl mpk 13-14kpl..
 
Yaah kwa Watu wa Serikalini kuna exemption kwa gari chini ya cc 4k.

EV ni nzuri, mie pia nitatafuta moja ya kutembea nayo mjini.

Ingawa gari za mafuta hasa petrol ni tamu sana unakuwa Engaged kwa kila hatua.

Mfano, nilikataa kutumia gari za Auto kabisa na wala sipatani nazo, leo hii ndio nihamie ktk EV tena unakuta ina Autopilot kbs unalala chuma inaenda yenyewe.. nitaweza mimi kweli..🥺
 
Bongo ni vurugu tupu ni muhimu kuwa makini usiingizwe kingi.

Mkuu una kacheo kwenye serikali ya kizimkazi?😄 Hao jamaa wa road bila wadhifa fulani hawakuachi kizembe namna hiyo.

Bora uendelee kunitakia mwema Dua zako zisikilizwe mambo yazodi kuwa mazuri kwangu na kwako pia, Bahati mbaya Sina vinasaba na Kizimkazi Kwa Sasa ila Kuna baadhi ya mambo tunashirikiana. Si unajua mjini mipango mingi ndugu yangu?

Kuna mmoja alinisimamisha kimakosa siku Moja, akaniambia kwanini naendesha gari na malapa, kimsingi nili overtake sehem sio na speed kubwa Sasa akawa amenipiga mkono. Akasema angalia usiache watoto bila Baba.

Kiroho safi wakati naondoka nikamwachia ten la kiwi Kwa vile alikua muungwana nikaanza kutafuta Ruvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…