Ukiwaelewa na kuwajua wanawake huwezi kuoa

Ukiwaelewa na kuwajua wanawake huwezi kuoa

Tatizo Lenu Vijana mnajifunza kwa watu waliofeli. Badala ya Kujifunza kwa watu waliofanikiwa.

Vijana wengi Mnajifanya Mnajua kumbe Hamjui. Ili Ujue nilazima Uwe mjinga ili Ujue.

Ndio Maana mnaoa Na ndoa hazidumu hata mwaka 1


Sisi tupo kwenye ndoa zaidi ya miaka 30 tunadunda Mjini Na Maisha yanaendelea mpaka tuna wajukuu.


Hongera MTUMISHI 30 yrs sio mchezo
 
Kwema Wakuu!

Kuna namna mbili za kutokuwa interested na Ndoa.
mosi, Kutowaelewa na kutowajua kabisa wanawake.
Pili, kuwaelewa na kuwajua sana wanawake.

Hiyo ya pili ndio zaidi. Watu wengi wanaowajua wanawake kindakindaki huishia kuwa bachelor sugu. Hawaoi.

Wapo wanaume wenye kila sifa yd kuoa lakini hawataki kufanya hivyo kutokana na uelewa wao mkubwa kuhusu wanawake

Jioni njema
Inasikitisha sana...Chanzo cha mabaya ni pesa na wasichana chunga sana alishasema Salu T.
 
Tatizo Lenu Vijana mnajifunza kwa watu waliofeli. Badala ya Kujifunza kwa watu waliofanikiwa.

Vijana wengi Mnajifanya Mnajua kumbe Hamjui. Ili Ujue nilazima Uwe mjinga ili Ujue.

Ndio Maana mnaoa Na ndoa hazidumu hata mwaka 1


Sisi tupo kwenye ndoa zaidi ya miaka 30 tunadunda Mjini Na Maisha yanaendelea mpaka tuna wajukuu.
Mkuu, sio kwamba tunajifanya tunajua zama zenu sio hizi za sasa.
 
Kama hujaingia kwenye ndoa nakushauri achana na hayo mawazo ya ndoa, ndoa ni dimbwi la umasikini hasa kwa kijana unaepambana kutimiza ndoto zako,picha anayokunyesha upo nae mbali mkaribishe uone rangi yake harisi#kataa kuoa mishangazi kibao imeachika inashinda bar kutega chambo wanaume Sasa hivi
 
Ok Hongera Sana , Mungu ni mwema Sana she is seem to be smartest &brilliant Enough.

Ukipata Mwanamke mwenye sifa hizi chukua
1. Msafi
Tabia kwanza kisha mwili.

2. Mvuto na Mzuri

3. Mtiifu anayejiamini na kufanya chochote utakachomuamuru
Narudia chochote bila kujali ni kizuri au kibaya.

4. Anayekupa pesa😊
Sijasema tajiri nazungumzia ambaye sio mbinafsi.
Mwanamke kama hajawahi wala hafikirii kukupa pesa na unatafuta mchumba huyo achana naye.

5. Anayekufanya wewe ni Role model wake.

6. Mwenye kiu ya mafanikio. Anayetaka na kupenda mafanikio yako.
Chochote unachofanya anakusaidia hasa kukupa kampani na kukupa moyo

7. Ambaye yupo tayari kukana hata ndugu zake kwaajili yako.
Huyo ni mkeo acha ujinga chukua jiko hiko. Kinyume na hapo weka mbali na watoto

8. Ambaye anashukuru kwa kila kizuri unachomfanyia kiwe kidogo au kikubwa.

9. Anayependa na kuheshimu wazazi wako.

10. Ambaye hata ukikorofishana na wazazi au ndugu zako anakutuliza na kukushauri vizuri kwa hekima sio kuchochea mgogoro

10. Ambaye mnaweza kuishi kama watoto na washkaji.

11. Ambaye atakuambia mno yote ya siri kuhusu yeye au jambo lolote

12. Ambaye hata kama umekosea yeye ndiye ananyenyekea.

13. Ambaye atakuonea wivu na hataki wanawake wengine wakuletee mazoea ya kipuuzi. Huyo ni mkeo.

14. Ambaye anaweza kuziba zile gap nyeti ambazo unakuwa unazisahau. Yaani anayekukamilisha.

Yaani mwanaume uwe 80% alafu hiyo 20% anastaajabu ameiweka.

Katika Ujasusi wanapotumwa Majasusi wawili wakike na wakiume katika mission fulani lengo kuu ni hilo.
Wakati jasusi wa kiume amemwambia jasusi wa kike abaki nyumbani kwa sababu ya hatari ya kumpoteza kutokana na adui kuwa hatari.

Jasusi wa kike hukubali kukaa nyumbani na kumwacha Jasusi wa kiume aende kwenye mission.
Wakati huo jasusi wa kiume anaamini kuwa anauwezo mkubwa(ni kweli lakini sio 100%)

Anafika kwa maadui anapambana na anawamaliza wote kasoro adui kuu.
Wakati anapambana na adui kuu wakiwa wamepigana vyakutosha na huenda amemzidi adui kuu lakini kwa bahati mbaya adui kuu baada ya kujua amezidiwa kwa hila anairukia bastola na kunyooshewa jasusi wa kiume, maskini jasusi wa kiume ni kweli anauwezo, ni kweli alimdhibiti adui kuu lakini kafanya kosa dogo lililompa upenyo adui kuu kuirukia bastola. Sasa jasusi wa kiume hana ujanja wowote anasubiri tuu kilimi cha bastola kiachiwe apasuliwe ubongo.

Lakini kabla adui hajaachia risasi ghafla mlio mwingine wa risasi unasikika adui anaanguka akiwa amepigwa risasi.
Jasusi wa kiume anashikwa mshangao anatazama huku na huku anamuona jasusi wa kike akiwa amebeba bastola. Ndie aliyemuua adui kuu.

Mkeo au Mwanamke kwenye maisha yako ndio anatakiwa kuwa hivyo.
Kuhakiki na ku- clear errors ndogo ndogo unazofanya unapokabiliana na maadui.

Ndio hivyo Mkuu
 
Kama hujaingia kwenye ndoa nakushauri achana na hayo mawazo ya ndoa, ndoa ni dimbwi la umasikini hasa kwa kijana unaepambana kutimiza ndoto zako,picha anayokunyesha upo nae mbali mkaribishe uone rangi yake harisi#kataa kuoa mishangazi kibao imeachika inashinda bar kutega chambo wanaume Sasa hivi

Duuh😀
 
Back
Top Bottom