Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #141
Mwanadamu hatabiriki, kumjua kiwango cha kusema unamjua mtu hilo suala halipo. Ndiposa waswahili wanasema hujafa hujaumbika. Kwamba mtu/watu hubadilika.
Ndiposa kwenye kuoa, ukipata mtu mmeelewana, mkakubaliana...ndoa ifungwe.
Mambo yakibadilika, ndoa ikawa ndoana, ukiweza vumilia, ukishindwa achana naye kisha anza upya. Maisha ni safari imejaa hekaheka
Mwanadamu habadiliki.
Mwanadamu unayemuona kabadilika ni yule ambaye ulikuwa hujamjua uhalisia wake.
Wewe ndiye unamuona kabadilika lakini yeye hajabadilika ila anaonyesha hulka yake halisi.