Ukiwaelewa na kuwajua wanawake huwezi kuoa

Kazi inakuja sasa, pale tunapo wauliza hao wanao wajua wanawake watueleze kuhusu hao wanawake. Lazima ucheke.

Wanawake ni viumbe dhaifu kwa ujumla wao, kadhalika wana upungufu wa akili kwa ujumla wake (japokuwa kwa mmoja mmoja wapo wanawake wanawazidi baadhi ya wanaume kwa akili) sasa hao wanaosadikiwa ya kuwa wanawajua wanawake utakuta kila uchwao wanshindana na hao wanawake. Hili ni kosa la kifundi la kutokuwajua wanawake.

Msilazimishe uongo ukaonekana kuwa kweli, hao ambao wenye sifa za kuoa kisha wasioe sio kweli kwamba wanawajua sana wanawake, bali hawawajui na matokeo yake wanawahofia na kuwaogopa.

Mimi siwezi kuacha kuoa sababu nawajua wanawake vizuri mno.
Maarifa yatakulevya mkuu.

Wàsio kuelewa wape muda, wataujua ukweli baadae
 
Kwema Wakuu!

Kuna namna mbili za kutokuwa interested na Ndoa.
Mosi, kutowaelewa na kutowajua kabisa wanawake.
Pili, kuwaelewa na kuwajua sana wanawake.

Hiyo ya pili ndio zaidi. Watu wengi wanaowajua wanawake kindakindaki huishia kuwa bachelor sugu. Hawaoi.

Wapo wanaume wenye kila sifa ya kuoa lakini hawataki kufanya hivyo kutokana na uelewa wao mkubwa kuhusu wanawake.

Jioni njema

Mwanadamu hatabiriki, kumjua kiwango cha kusema unamjua mtu hilo suala halipo. Ndiposa waswahili wanasema hujafa hujaumbika. Kwamba mtu/watu hubadilika.

Ndiposa kwenye kuoa, ukipata mtu mmeelewana, mkakubaliana...ndoa ifungwe.

Mambo yakibadilika, ndoa ikawa ndoana, ukiweza vumilia, ukishindwa achana naye kisha anza upya. Maisha ni safari imejaa hekaheka
 
Ukipata Mwanamke mwenye sifa hizi chukua
1. Msafi
Tabia kwanza kisha mwili.

2. Mvuto na Mzuri

3. Mtiifu anayejiamini na kufanya chochote utakachomuamuru
Narudia chochote bila kujali ni kizuri au kibaya.

4. Anayekupa pesa😊
Sijasema tajiri nazungumzia ambaye sio mbinafsi.
Mwanamke kama hajawahi wala hafikirii kukupa pesa na unatafuta mchumba huyo achana naye.

5. Anayekufanya wewe ni Role model wake.

6. Mwenye kiu ya mafanikio. Anayetaka na kupenda mafanikio yako.
Chochote unachofanya anakusaidia hasa kukupa kampani na kukupa moyo

7. Ambaye yupo tayari kukana hata ndugu zake kwaajili yako.
Huyo ni mkeo acha ujinga chukua jiko hiko. Kinyume na hapo weka mbali na watoto

8. Ambaye anashukuru kwa kila kizuri unachomfanyia kiwe kidogo au kikubwa.

9. Anayependa na kuheshimu wazazi wako.

10. Ambaye hata ukikorofishana na wazazi au ndugu zako anakutuliza na kukushauri vizuri kwa hekima sio kuchochea mgogoro

10. Ambaye mnaweza kuishi kama watoto na washkaji.

11. Ambaye atakuambia mno yote ya siri kuhusu yeye au jambo lolote

12. Ambaye hata kama umekosea yeye ndiye ananyenyekea.

13. Ambaye atakuonea wivu na hataki wanawake wengine wakuletee mazoea ya kipuuzi. Huyo ni mkeo.

14. Ambaye anaweza kuziba zile gap nyeti ambazo unakuwa unazisahau. Yaani anayekukamilisha.

Yaani mwanaume uwe 80% alafu hiyo 20% anastaajabu ameiweka.

Katika Ujasusi wanapotumwa Majasusi wawili wakike na wakiume katika mission fulani lengo kuu ni hilo.
Wakati jasusi wa kiume amemwambia jasusi wa kike abaki nyumbani kwa sababu ya hatari ya kumpoteza kutokana na adui kuwa hatari.

Jasusi wa kike hukubali kukaa nyumbani na kumwacha Jasusi wa kiume aende kwenye mission.
Wakati huo jasusi wa kiume anaamini kuwa anauwezo mkubwa(ni kweli lakini sio 100%)

Anafika kwa maadui anapambana na anawamaliza wote kasoro adui kuu.
Wakati anapambana na adui kuu wakiwa wamepigana vyakutosha na huenda amemzidi adui kuu lakini kwa bahati mbaya adui kuu baada ya kujua amezidiwa kwa hila anairukia bastola na kunyooshewa jasusi wa kiume, maskini jasusi wa kiume ni kweli anauwezo, ni kweli alimdhibiti adui kuu lakini kafanya kosa dogo lililompa upenyo adui kuu kuirukia bastola. Sasa jasusi wa kiume hana ujanja wowote anasubiri tuu kilimi cha bastola kiachiwe apasuliwe ubongo.

Lakini kabla adui hajaachia risasi ghafla mlio mwingine wa risasi unasikika adui anaanguka akiwa amepigwa risasi.
Jasusi wa kiume anashikwa mshangao anatazama huku na huku anamuona jasusi wa kike akiwa amebeba bastola. Ndie aliyemuua adui kuu.

Mkeo au Mwanamke kwenye maisha yako ndio anatakiwa kuwa hivyo.
Kuhakiki na ku- clear errors ndogo ndogo unazofanya unapokabiliana na maadui.

Ndio hivyo Mkuu

Vijana mnaandika maneno mengi sana kuwahusu hawa viumbe, wakati mlitakiwa mtumie maneno machache yenye kujitosheleza.

Kwanza kabisa mnatakiwa mjue hakuna mkamilifu, ukimpata mwanamke mwenye tabia njema na dini oa. Tabia njema ni jambo kubwa sana, ambalo ungelijua usingeandika maneno mengi hivi.

Kuna sifa za msingi na sifa za ziada. Tabia njema na dini, hizi ndio sifa za msingi ambazo zikitimia hizi kadhia inakuwa imeisha.
 
"Tabia njema na dini"

NAKAZIA
 
Hicho kipengere namba 4 sasa 😀😀😀 jiandae kuitwa marioo.. wao wenyewe wanayaangalia mahusiano na ndoa kama fursa ya kupata hela halafu ndio akupe wewe tena
 
Nimeshaoa kama miaka kumi iliyopita..Katika utafiti wangu nimegundua kwamba:
1.Wanaume ni waathirika wakuu wa ndoa kiuchumi,Pato lake linatumika kwaajili ya mke,mashemeji,watoto nk.Yaani unakuta anasuruali tatu, pair1 za viatu kinyume na kipato chako

2.Stress nyingi kwaajili ya mkewe, na familia ie kuchitiwa na migogoro ya hapa na pale yaliyosababishwa na kuoa
Unasafa sana kwaajili ya familia yako wakati wanaoinjoy ni wengine.

Mwisho wake baba anadharauliwa na sifa zote Kwa mke na huko uzeeni watoto na mama yao wanakutenga, na watoto wanamjali mama yao kuliko baba....
Ndoa ni utapeli uliohalalishwa kisheria na kijamii.
 
Mkuu wa like kesho asubuhi piga supu chapati mbili ila itabidi ulipie

Hili swali lako hata huko kwenyw jamii ukiuliza hawana majibu, tunapigishana michango ila michongo ya kuhakikisha michango ikiyokea tunaimudu hatupeani/hatujadili/hatushauriani
Wabongo waambie unatarajia kuoa watakuchangia milioni za kutosha tu, wasikie umekufa watatoa hela za rambirambi nyingi tu ila wape business plan yako waambie umekwama mtaji hakuna atakaekuchangia hata buku.
 
ukishindwa achana naye kisha anza upya. Maisha ni safari imejaa hekaheka
Hapo kwenye kuachana ndipo maumivu makali anakutana nayo mwanaume maana mali zake zinagawanywa wakati za mwanamke haziguswi., kumbuka sheria ya ndoa haitambua kipato na mali za mwanamke. Kwa mwanaume kuoa ni kamali
 
Kamali huwa Ina kupata na kukosa. Sasa upande wa kupata ktk ndoa (hasa wanaume) mbona siuoni? Hebu tusaidie kudadavua.
Mwanaume anatakiwa ku-provide security kwa mwanamke na in-return mwanaume huyu atafaidika na huduma za nyumbani kutoka kwa uyo mwanamke. Tatizo ni kwamba anachotakiwa ku-provide mwanaume kipo kisheria na anachotakiwa ku-provide mwanamke kinategemeana na hiyari yake. Ndio maana nikasema kwa mwanamke ni mchongo wa uhakika kwa maana haki yake inalindwa kisheria ila kwa mwanaume ni kamali kwa maana mwanamke asipotimiza wajibu wake hauna cha kumfanya kisheria kumbuka ukimpa talaka mali zinapigwa pasu kwa pasu hata kama mwanamke ndio tatizo.
 
Ni kweli. Na ni kwa muktadha huo, ndiyo maana mabaharia wanahitimisha kwa kusema kuwa " ndoa haina faida kwa mwanaume".
 
Binafsi mahusiano ya kimapenzi na mwanamke siwezi kuepuka nishapitia mahusiano mengi sana na bado sijafika mwisho lakini ule mkataba wa kitapeli uliopewa jina la "ndoa" sitakuja kuweka saini yangu.
 
Vijana mnaandika maneno mengi sana kuwahusu hawa viumbe, wakati mlitakiwa mtumie maneno machache yenye kujitosheleza.

Kwanza kabisa mnatakiwa mjue hakuna mkamilifu, ukimpata mwanamke mwenye tabia njema na dini oa. Tabia njema ni jambo kubwa sana, ambalo ungelijua usingeandika maneno mengi hivi.

Kuna sifa za msingi na sifa za ziada. Tabia njema na dini, hizi ndio sifa za msingi ambazo zikitimia hizi kadhia inakuwa imeisha.

Tabia njema inatokana na maadili ya kitamaduni au dini.
Elewa maadili ya tamaduni au dini hii sio maadili ya dini au tamaduni nyingine.

Kwa hiyo unaposema tabia njema ni lazima urejelee maadili ya tamaduni au dini ipi.
Upo Mzee
 
Hicho kipengere namba 4 sasa 😀😀😀 jiandae kuitwa marioo.. wao wenyewe wanayaangalia mahusiano na ndoa kama fursa ya kupata hela halafu ndio akupe wewe tena

Hiyo ni kauli ya kuwadhibiti wanaume wajinga waendelee kuwa misukule yao.
 
Back
Top Bottom