Ukiwaelewa na kuwajua wanawake huwezi kuoa

Ukiwaelewa na kuwajua wanawake huwezi kuoa

Matokea ya 50 kwa 50 mkuu , tumempigania mtoto wa kike mpaka ikapitiliza tukamsahau mtoto wa kiume , sasa inakua ni ngumu mtoto huyo wa kiume kuishi ya mtoto huyo wa kike aliyepiganiwa kwa kila namna .
Nadhani hata ukiachana na mpambano wa 50 kwa 50, hoja kubwa hapa ni je, ndoa Ina faida?
 
Ukipata Mwanamke mwenye sifa hizi chukua
1. Msafi
Tabia kwanza kisha mwili.

2. Mvuto na Mzuri

3. Mtiifu anayejiamini na kufanya chochote utakachomuamuru
Narudia chochote bila kujali ni kizuri au kibaya.

4. Anayekupa pesa😊
Sijasema tajiri nazungumzia ambaye sio mbinafsi.
Mwanamke kama hajawahi wala hafikirii kukupa pesa na unatafuta mchumba huyo achana naye.

5. Anayekufanya wewe ni Role model wake.

6. Mwenye kiu ya mafanikio. Anayetaka na kupenda mafanikio yako.
Chochote unachofanya anakusaidia hasa kukupa kampani na kukupa moyo

7. Ambaye yupo tayari kukana hata ndugu zake kwaajili yako.
Huyo ni mkeo acha ujinga chukua jiko hiko. Kinyume na hapo weka mbali na watoto

8. Ambaye anashukuru kwa kila kizuri unachomfanyia kiwe kidogo au kikubwa.

9. Anayependa na kuheshimu wazazi wako.

10. Ambaye hata ukikorofishana na wazazi au ndugu zako anakutuliza na kukushauri vizuri kwa hekima sio kuchochea mgogoro

10. Ambaye mnaweza kuishi kama watoto na washkaji.

11. Ambaye atakuambia mno yote ya siri kuhusu yeye au jambo lolote

12. Ambaye hata kama umekosea yeye ndiye ananyenyekea.

13. Ambaye atakuonea wivu na hataki wanawake wengine wakuletee mazoea ya kipuuzi. Huyo ni mkeo.

14. Ambaye anaweza kuziba zile gap nyeti ambazo unakuwa unazisahau. Yaani anayekukamilisha.

Yaani mwanaume uwe 80% alafu hiyo 20% anastaajabu ameiweka.

Katika Ujasusi wanapotumwa Majasusi wawili wakike na wakiume katika mission fulani lengo kuu ni hilo.
Wakati jasusi wa kiume amemwambia jasusi wa kike abaki nyumbani kwa sababu ya hatari ya kumpoteza kutokana na adui kuwa hatari.

Jasusi wa kike hukubali kukaa nyumbani na kumwacha Jasusi wa kiume aende kwenye mission.
Wakati huo jasusi wa kiume anaamini kuwa anauwezo mkubwa(ni kweli lakini sio 100%)

Anafika kwa maadui anapambana na anawamaliza wote kasoro adui kuu.
Wakati anapambana na adui kuu wakiwa wamepigana vyakutosha na huenda amemzidi adui kuu lakini kwa bahati mbaya adui kuu baada ya kujua amezidiwa kwa hila anairukia bastola na kunyooshewa jasusi wa kiume, maskini jasusi wa kiume ni kweli anauwezo, ni kweli alimdhibiti adui kuu lakini kafanya kosa dogo lililompa upenyo adui kuu kuirukia bastola. Sasa jasusi wa kiume hana ujanja wowote anasubiri tuu kilimi cha bastola kiachiwe apasuliwe ubongo.

Lakini kabla adui hajaachia risasi ghafla mlio mwingine wa risasi unasikika adui anaanguka akiwa amepigwa risasi.
Jasusi wa kiume anashikwa mshangao anatazama huku na huku anamuona jasusi wa kike akiwa amebeba bastola. Ndie aliyemuua adui kuu.

Mkeo au Mwanamke kwenye maisha yako ndio anatakiwa kuwa hivyo.
Kuhakiki na ku- clear errors ndogo ndogo unazofanya unapokabiliana na maadui.

Ndio hivyo Mkuu
Sina uhakika kama utapata binadamu wa kike mwenye sifa hizo zote
 
Kwema Wakuu!

Kuna namna mbili za kutokuwa interested na Ndoa.
Mosi, kutowaelewa na kutowajua kabisa wanawake.
Pili, kuwaelewa na kuwajua sana wanawake.

Hiyo ya pili ndio zaidi. Watu wengi wanaowajua wanawake kindakindaki huishia kuwa bachelor sugu. Hawaoi.

Wapo wanaume wenye kila sifa ya kuoa lakini hawataki kufanya hivyo kutokana na uelewa wao mkubwa kuhusu wanawake.

Jioni njema
Usipooa utaolewa ty mkuuu somaaa maandiko hili neno futa
 
Ivi ni kwanni uhamasishaji wa kuoa kwa Tanzania umekua mkubwa mno kuliko kupeana michongo ?
Mkuu wa like kesho asubuhi piga supu chapati mbili ila itabidi ulipie

Hili swali lako hata huko kwenyw jamii ukiuliza hawana majibu, tunapigishana michango ila michongo ya kuhakikisha michango ikiyokea tunaimudu hatupeani/hatujadili/hatushauriani
 
Mwanaume kuoa ni sawa na kujitumbukiza kwenye karai la kukaangia kiepe.
 
Not just to marry them, once you have full knowledge about women's hubristic female nature and how they navigate in the whole premise of intersexual dynamics to attain their personal desirability, you may even hate them for the rest of your life.
 
Hiyo ya pili ndio zaidi. Watu wengi wanaowajua wanawake kindakindaki huishia kuwa bachelor sugu. Hawaoi.

Vijana mna ujinga mwingi sana, naona mnaandika vitu kinyume nyume sana. Hao ambao hawaoi kwa kujidanganya ya kuwa wanawajua wanawake ndio ndio hawawajui Wanawake sasa.
 
Wapo wanaume wenye kila sifa ya kuoa lakini hawataki kufanya hivyo kutokana na uelewa wao mkubwa kuhusu wanawake.

Kazi inakuja sasa, pale tunapo wauliza hao wanao wajua wanawake watueleze kuhusu hao wanawake. Lazima ucheke.

Wanawake ni viumbe dhaifu kwa ujumla wao, kadhalika wana upungufu wa akili kwa ujumla wake (japokuwa kwa mmoja mmoja wapo wanawake wanawazidi baadhi ya wanaume kwa akili) sasa hao wanaosadikiwa ya kuwa wanawajua wanawake utakuta kila uchwao wanashindana na hao wanawake. Hili ni kosa la kiufundi la kutokuwajua wanawake.

Msilazimishe uongo ukaonekana kuwa kweli, hao ambao wenye sifa za kuoa kisha wasioe sio kweli kwamba wanawajua sana wanawake, bali hawawajui na matokeo yake wanawahofia na kuwaogopa.

Mimi siwezi kuacha kuoa sababu nawajua wanawake vizuri mno.
 
Ivi ni kwanni uhamasishaji wa kuoa kwa Tanzania umekua mkubwa mno kuliko kupeana michongo ?
Ndoa ni taasisi, Ndoa ni serikali, Ndoa ni shule, ukitaka jamii yako ieleweke na kukua katika misingi ya muunbaji wa mbingu na dunia, Ndoa ikiwa stable bila 50/50 unatoboa.

Kwa taarifa za mapema ni kwanba kuna kundi kubwa sana wanandoa wanaodai taraka hivi sasa, kwa hiyo hata hawa wanao hamasisha watu waingie huko wanafanya jambo zuri sana.

Mchongo wa pesa bila matumiaji ni O!.
 
Back
Top Bottom