Ukiwajua Polisi Tanzania, hutawashangaa kabisa na taarifa zao

Kwa mimi nisiyejua utendaji wa Polisi hapo nilichoona mtandao wa mawasiliano kwenye vituo vya Polisi hakuna.
(Sijui Radio call ni za kazi gani tena)
1.Kungekuwa na mawasiliano vituo vyote polisi pale mtuhumiwa ameripotiwa kituo kimoja cha Polisi vituo vyote vingepewa taarifa kwamba kuna mtuhumiwa fulani mwenye jina fulani kama ataripotiwa kituo kingine akamatwe.
2.Polisi ingeshirikisha jamii kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari au magazeti juu ya Polisi mtuhumiwa wa uharifu kwamba ko kote atakapoonekana watu watoe taarifa kituo cho chote polisi ili iwe rahisi kumkamata.
Nawaza hivyo kwa jiji kama Dar,mtu anaweza kufanya uharifu Temeke akakimbilia Tegeta! Hata Polisi wangekuwa na makachero kiasi inaweza ikachukua muda kumkamata muharifu.
 
I agree
 
Mna tuchanganya sana na hizi stori zenu za kusadikika.

Polisi hao hao mnao wasema wanaonyesha ufanisi mkubwa sana wakati wa maandamano ya CHADEMA! Vipi, hawa huwa wamekodiwa toka sehemu nyingine duniani?

Chukua mfano wa Lema, anatoka Arusha kuja Dar es Salaam kuungana na wenzake kwenye maandamano. Hata kabla ya kukanyaga ardhi ya Dar, tayari anadakwa humo humo kwenye ndege!

Kuna ubovu wa utendaji ndani ya jeshi la polisi, siyo kwa sababu ya muundo, kama inavyo elezwa kwenye mada hii. Huu "mfumo" unazuia mawasiliano kati ya kituo kimoja cha polisi na kingine?

Maswala ya uzembe na kuto wajibika kwa wahusika sasa nayo yanabatizwa kuwa ni sababu ya "mfumo"?

Hili nalo limekuwa ni tatizo kwa Tanzania, la kutafuta visingizio kwa kila jambo linalo fanyika vibaya.

Huo mfano ulio tolewa hapo kwa mtuhumiwa anaye tafutwa, ni swala la uzembe.
 
Hizi time line huwa zinafanyiwa kazi kabla ya taarifa, sema mambo huwa yanakuwa mengi, pressure za nje taarifa inabidi itolewe tu.

Wale walio wahi kufanya kazi za uchunguzi polisi wanaweza kuelewa nasema nini.

Zamani tulikuwa tunawaita Investigation Bureu, pale ghorofa ya 7 makao makuu ya zamani, kwa sasa Dodoma sijui wanajiitaje.

Ni ngumu kupanga kuongea vitu vya kuunga unga, ukweli upo lakini hautoki. Serikali ngumu sana.
 
HATUNA POLICE NCHI HII ILA WAUAJI NA WEZI WAKUBWA. KAMA MLIONA WALE WALIOTUHUMIWA KUTAKA KUMTEKA YULE TARIMO KULE KIBAHA, HAKUNA HATA MMOJA ALIYEFANANA NA WALIOKUWA KWENYE ILE VIDEO, WAMEWACHUKUA WATU WA MITAANI HALAFU BAADAYE WATAWAACHIA. WAHUNI HAO POLICE NA MAHAKAMA INAANGALIA TU.
 
This is a straight forward "Black and White" type of issue. Where do "notions" come from?
I am not the one making the accusations, the main viewpoint of the police conduct derive from post one.

That is to say I can’t justify nor disagree with the member’s accusation, why force people to make decisions on matters they can’t defend.
 
No one is "forcing" anybody about anything!
What does the word "agree" mean to you?
 
Hii inashangaza sana. Yaani ukienda kufungua jalada mahali kwingine ni kama vile hilo haliwahusu.
Kama uliibiwa ukiwa safarini, urudi huko huko ukafungue kesi. Polisi wa nchi hii sijui wameshajichokea na kesi za wananchi au wamechoka kazi?

Hata kuhusu tukio la aliyepata ajali na kisha wasamaria kumpeleka hospitali; ina maana hiyo ajali haikukaguliwa na polisi wa usalama barabarani? Hiyo pikipiki plate namba zilipotea? Huenda ingesaidia kumjua mmiliki na hatmaye kupata taarifa za majeruhi.
 
Nchi ya kitu kidogo hii. Kama tajiri na muwekezaji mkubwa aliwahi lalamika kuwa mahakama zinafanya kazi kwa maelekezo ya simu toka juu. Unadhani jeshi la polisi linaponaje
 
What does the phrase ‘I can’t conclude’ mean to you?
No. Let's deal with one step at a time, sequentially.
"I agree" came first, so let's deal with that, then we can move forward to where you want to have answers on "phrases".
 
No. Let's deal with one step at a time, sequentially.
"I agree" came first, so let's deal with that, then we can move forward to where you want to have answers on "phrases".
Steps start with the perspective (viewpoint) presented by post number one (based on his experience). Your demands have no merits rather forceful asking contributors to pick a side.

Even when they tell you, they can’t justify their position without evidence, but can only agree by implying based on general accusations of the police force.

You can’t conclude on things you have no evidence (hearsay is not evidence nor is one sided accusations) that’s not how knowledge works.
 
Ccm wanapenda libaki hivi hivi,
 
Ndiyo mimi nashangaa kwa maana watu hawajui polisi au kujichetua akili police siku zote wapo kimaslahi sana hao watu wanaowalaumu polisi wanaishi nchi gani? Ukiwajua na kuwafahamu polisi wala haileti shida kuumiza kichwa aisee
 
Una wazo zuri ila kibongobongo kama haligusi wanasaiasa litafanyika, ila kama linagusa vyeo vya watu, litapigwa danadana sana.

Na kweli jeshi linaendeshwa kizamani mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…