Ukiwajua Polisi Tanzania, hutawashangaa kabisa na taarifa zao

Duuh Hatari sana!
 
Umemaliza ! πŸ‘πŸ™Œ
 
Nina mkasa unaofanana na wako, na Mimi nilifungua taarifa chang,'ombe lakini mtuhumiwa walimkata wakamwachia kwa dhamana Ila ishu yangu ilifunguliwa jalafa na Dci na waliokuwa wanashugulika ni FCU Cha ajabu hawana taarifa zozote kwamba mtuhumiwa alishakamatwa Chang'ombe hata nilipowaambia bdo hawakuweza kuwasiliana
 
Polisi wana laana hao jamaa mie mtoto wangu yeyote atakaye kuja kuwa polisi mimie sie baba yake nitamkataaa hadharani
Angalia maisha Yao baada ya Kustaafu! Fanya utafiti kidogo tu utajua karma is real! Mwingine anajitengenezea kaburi huko,huku akiwa hama maelewano na familia yake kabisa anaitwa 7sita
 
Tatizo linaanza kwenye kutii amri bila ya kushirikisha akili (kupinga).
 
Angalia maisha Yao baada ya Kustaafu! Fanya utafiti kidogo tu utajua karma is real! Mwingine anajitengenezea kaburi huko,huku akiwa hama maelewano na familia yake kabisa anaitwa 7sita
Umenichekesha sana Hahaha 🀣
Hivi yule jamaa alishakamilisha ule mradi wake ??!
Dunia ina mambo ya ajabu 😱
 
Duuh Hatari sana!
Lengo ni kuhakikisha kwamba wajinga wanawasimamia polisi wasomi! Unakuta Askari polisi let's say RPC au OCD, Ni msomi mzuri wa Sheria kama Muliro! Anajua namna mifumo inavyofanya kazi, lakini juu yake amewekwa DC na RC mwenye kichwa kama Cha chalamila! Na amepewa title ya Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa au WILAYA na yeye ndiye anayetoa maelekezo, Nini kifanyike na Nini kisifanyike, jua kwamba OCD na RPC asubuhi anatoa taarifa (briefing) ya Hali ya usalama kwenye eneo lake Kwa huyu kilaza aliteteuliwa Kwa kulipa fadhila au jinsi alivyofanilisha wizi wa kura nk nk.
Hakuna mtu anayepinga au kupindisha Maagizo ya Mwenyekiti! Matokeo yake Ndio haya wanaagizwa Cha kufanya na wajinga wajinga.
 
Haaaa.. hata wewe muuza ngada unashitaki kutapeliwa πŸ™„ kanuni ya wauza ngada inasema hakuna kushitakiana kwa mambo ya utapeli wa aina yoyote songa mbele....ila kwa kuongeza mimi binafsi nawajua majambazi walio pata ajira polisi dar es salaam huku kule kigoma walikuwa ni majambazii yanayo tafutwa na polisi kwa miaka mingi .. jeshi la polisi linaongozwa kipumbavu sana ...mtu yoyote anaye ingia kituo cha polici ni lazima system zimtambue kikompyuta kabla ya kupatiwa huduma yoyote iwe ni kushitaki au kushitakiwa nk na mifumo yote ya serikali hadi mahospitalini ilitakiwa iwe connected na usalama wa taifa hivyo mambo ya PF3 yasinge itajika sana maana ukifika hospital unaingizwa kwenye system kutambulika ...kama ni muhalifu polisi inapokea alert πŸ“’ kuwa hupo hospitalini wanatia team kuku aresti nk
 
Baadhi ya mifumo ipo tayari ila baadhi kweli hadi tuweze kuifikia itahitaji miaka mingi sana kwa hapa tulipo.

Mfano hili la DNA kwa sasa tu kupata majibu ya DNA inachukua muda, hivyo bado swala la muda hatutakuwa tumelitatua.

Ishu kama ya kuibiwa simu, hapa kuna mambo mengi sana zaidi hata ya hao polisi. Kwanza simu iwe na settings za uhakika na taarifa zake mwenye simu husika awe nazo.

Simu inaweza kupatikana hata bila ya kuwatumia polisi lakini bado ni changamoto sababu ya settings na uwepo wa data ya internet.

Ebu fikiria tu watu wengi wana simu janja na bado hata hawafahamu emails zao walizosajilia hizo simu.

Bado tunahitaji kuwa na elimu kwa jamii hasa ya masuala ya ulinzi wa taarifa binafsi, matumizi ya vifaa kama simu janja na mambo yanayohusiana navyo.

Ila ni kweli pia jeshi letu la polisi linahitaji maboresho hasa ili kuendana na wakati huu wa uhalifu wa kidigitali
 
Umenichekesha sana Hahaha 🀣
Hivi yule jamaa alishakamilisha ule mradi wake ??!
Dunia ina mambo ya ajabu 😱
Amekamilisha na ameshanunua Jeneza na kuteua Mwenyekiti wa kamati ya Mazishi. Kiufupi anateswa na Spirit haunting! Yani nafsi za watu zinamlilia jinsi alivyozikatili! Nimekutana na mwanafamilia mmoja akanidokeza kwamba, mke ameshaondoka nyumbani sababu jamaa ni mkorofi kuliko anavyoonekana kwenye screen!
 
Naunga mkono hoja hii.....hasa kufanya overhaul ya jeshi la Polisi hilo ni muhimu Sasa.
 
Mifumo mingi haisomani hata huko forodha tulimsikia mkubwa mmoja analalamika !!
πŸ™πŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈ
 
Hatari sana 😱
 
😳😱 !!
 

Naunga mkono hoja kwa asilimia 100. Halijaandaliwa kufanya kazi kwenye dunia ya sasa.
Lina structure ambayo ni rigid na hair hairuhusu creativity.
Lina promote kulindana wao kwa wao hata kama kuna wengine wahalifu.
Halijaandaliwa kufanya policing kwenye mfumo wa siasa wa vyama vingi.
Sijui KPI zake, ila nachoka sana napoona matatizo yamekuwa mengi ila viongozi wamesheheni bashasha
 
Umesema mengi kiongozi

Ila AKILI ni tofauti na ELIMU Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…