Ukizaa na mume wa mtu, jukumu la kulea mtoto ni lako mwenyewe!

Wanawake sijui wana akili gani kuna single mother mmoja kazaa na mume wa mtu tena huyo mume ana wake watatu, yani mpaka leo namshangaa sijui tamaa ya pesa mzee mwenyewe ni muislam tena umri kama wa baba yake

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mwanaume uzinzi ni starehe ambayo haimuathiri kama Dada zetu.
Ndio maana wazee wetu wa kale hawakuwa wajinga kumdhibiti Mwanamke dhidi ya kuziniwa ili Asipate madhara
Hata Mungu anajua hilo

Nyie endeleeni kuchagua dhambi zinazowafurahisha mnazilea
 
Kwani sex hufanyika kwaajili ya kutaka kuzaa tu ?

Je siyo kwaajili ya kupeana raha tu ?
Raha inayoweza kuleta watoto

Watu mjizuie ama muwajibike

Hata usipowajibika ni sawa pia
Mungu ana mkono mrefu sana
Narudia tumuogope Mungu sanaa
Usimkomoe mama wala mtoto
Waza mbele y Mungu utatoa utetezi gani
 
Watu wamekubaliana wakajifunika duvet moja
Mbona unaumia wewe?
 
Hata Mungu anajua hilo

Nyie endeleeni kuchagua dhambi zinazowafurahisha mnazilea

Sio kila MTU anaamini habari za Mungu
Ila linapokuja suala la madhara halisi halitochagua muamini na asiye Amini.

Yule anayedhurika ndiye anapaswa kujikinga na kukingwa zaidi, hiyo ni kanuni ya Asili.
 
Raha inayoweza kuleta watoto

Watu mjizuie ama muwajibike

Hata usipowajibika ni sawa pia
Mungu ana mkono mrefu sana
Narudia tumuogope Mungu sanaa
Usimkomoe mama wala mtoto
Waza mbele y Mungu utatoa utetezi gani

Mungu hahusiki na maujinga yetu.
Mfanye maujinga alafu mumuingize Mungu kwenye upumbavu wenu.

Raha inapaswa uwe ndani ya Ndoa,
Nje ya hapo Mwanamke anajiingiza katika jina Baya la ukahaba au umalaya.
Na Matokeo yake atawajibika yeye zaidi, kiasili
 
Mwanamke aliyezaa na mume wa mtu hafai kuwa mke, uyo ni mtafuta maisha....... " alisikika jamaa mmoja katikati ya kundi la vijana"
 
Mungu hahusiki na maujinga yetu.
Mfanye maujinga alafu mumuingize Mungu kwenye upumbavu wenu.

Raha inapaswa uwe ndani ya Ndoa,
Nje ya hapo Mwanamke anajiingiza katika jina Baya la ukahaba au umalaya.
Na Matokeo yake atawajibika yeye zaidi, kiasili
Kwa muktadha wa mada hii aliye katika ndoa ni mume
Hivyo atulie na mkewe maisha yake yote
 
Sio kila MTU anaamini habari za Mungu
Ila linapokuja suala la madhara halisi halitochagua muamini na asiye Amini.

Yule anayedhurika ndiye anapaswa kujikinga na kukingwa zaidi, hiyo ni kanuni ya Asili.
Kama unapenda kumkinga himiza wenye viapo vya ndoa watulie ndani ya ndoa
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Hatari sana wapambane na hali yao
 
Watu wamekubaliana wakajifunika duvet moja
Mbona unaumia wewe?
Mtoto anaumia kwa kukosa maisha ya furaha kutoka kwa wazazi na upande wa ndugu wa Baba tena omba Baba mtoto hasiwe muislamu yani mtoto hawezi kupendwa na ndugu wa Baba na Bibi zake, yani mfano Baba yake amefariki siku kuzika wakitaja wasifu wa marehemu wakifika kipengere cha kutaja idadi ya watoto watatajwa watoto wake aliozaa nje ya ndoa kama anawatoto kumi wa ndoa wanatajwa hao tu, hao wa nje ya ndoa hawa tambuliki.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Ni upuuzi tu
Uzuri kila mtu atatoa hesabu ya ujinga wake
Starehe zako mwenyewe afu unakuja kutesa watoto
 
Nawezaje kumchukua mtoto wangu ambar nina muhidumia lakini mama mtoto hataki kunipa nikae naee??
 
Nawezaje kumchukua mtoto wangu ambar nina muhidumia lakini mama mtoto hataki kunipa nikae naee??

Anajua akikupatia ruzuku ya malezi na matunzo ya mtoto itakata kisha yeye atakula nini?!

Hao ndio hutegesha mimba kuzaa watoto kuwafanya kitega uchumi.

Kama hataki achana nae kama mtoto ni damu yako akikua atakutafuta mwenyewe!
 
Hakuna Baba anaweza kuona mtoto wake akiteseka! Awe wa nje au wa ndani ya ndoa.
Msiwatishe mabinti waacheni tuzae nao. Mtoto ni blessings
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…