Ukizaa na mume wa mtu, jukumu la kulea mtoto ni lako mwenyewe!

Ukizaa na mume wa mtu, jukumu la kulea mtoto ni lako mwenyewe!

Umeongea Ukweli mtupu Taikon ,hakika hukoseagi kwenye maandiko Ungekuwa Le Mutuz ningesema Mzee wa Facts hakuna kupindisha maneno kitu black and white.
 
Ni wanaume wangapi humu ikitokea kapata mtoto nje ya ndoa atamwambia huyo mwanamke JUKUMU LA KULEA HUYO MTOTO NI LAKO? Yaani utamtelekeza mwanao?
mwnyw nmeshangaa aisee,
Michango ya hivi inastahili kutolewa na wavulana wanaobalehe,

Huwez kua mwanaume unaejitambua unajisifia kutelekeza damu yako, no matter what happened.
 
Someni TAARIFA YA SERIKALI NA. 134 ya tarehe 09/05/2014 TAFSIRI YA SHERIA YA MTOTO [SURA YA 13] TOLEO LA MWAKA, 2014, Sehemu ya 10. Inahusu haki ya mtoto kupata mali.
 
UKIZAA NA MUME WA MTU, JUKUMU LA KULEA MTOTO NI LAKO MWENYEWE!

Anaandika, Robert Heriel

Unajizima Data sio!

Ati ooh! Alinidanganya Hana MKE, ooh! Sikujua kama kaoa. Wanaume ni Umbwa Koko!

Kama alikuambia Hana MKE si ungemuambia Ukoe wewe sasa ili uwe Mke wake. Mwambie apeleke posa nyumbani, taratibu za kindoa zifuate, iwe ndoa ya kimila au kiserikali au kidini. Kimila utaratibu ni simple Sana. Ukishaenda kutoa posa ukakubali tayari hiyo ni Ndoa.

Binti yangu epuka kujizima data. Mabinti WA siku hizi wengi ni wale wa liwalo na liwe. Wanayachezea Maisha yao kijinga.

Wengi wanajua kabisa Fulani ni mume wa mtu lakini kwa tamaa ya Pesa wanajilengesha Makusudi, na kujibebesha mimba, kisha baadaye wanaanza kusumbua Watu.

Acheni ubinafsi, eleweni kuwa mnawatesa Watoto wenu. Mtoto wako hawezi kulingana kihadhi na mtoto wa kwenye Ndoa. Hawezi kupata thamani kama angezaliwa ndani ya Ndoa. Mtoto wako utakayemzaa badala ya kuwa baraka anakuwa mleta tafrani Duniani.

Kwa nini usitafute Mwanaume wako akakuoa ndipo upate mtoto, uone jinsi ilivyoraha mtoto kulelewa na Baba na Mama. Wewe unazaa na waume za Watu alafu kama chizi ATI unasema ATI alinidanganya hana MKE. Hana MKE ulienda kwao akakutambulisha na Akaja kwenu kutoa Mahari ili useme alikudanganya. Wewe ndiye ulijidanganya.

Jukumu la KULEA MTOTO uliyempata Kwa Mume WA MTU ni jukumu lako ewe Binti yangu.

Hakuna Mwanamke yeyote mwenye Akili, MKE kamili atakayekubali Mume wake akuhudumie wewe au huyo mtoto wako. Na hiyo ipo Naturally ili ujutie Makosa uliyoyafanya, sasa Kwa nini umtese mtoto wako kisa ujinga wako. Ni Bora ukaacha kuzaa na waume za Watu.

ATI ili mtoto wako ahudumiwe ni mpaka vikao, sijui kupelekana Mahakamani, sijui kutukana na mume WA MTU. Kwa nini ujipe Shida? Yaani mpaka Mwanaume apate Pesa ya ziada ndio akupe wewe Pesa ya matumizi ya Mtoto. Lakini mtoto wako hayupo kwenye hesabu za Baba yake kisa Baba anafamilia Kuu anayoiangalia.

Binti yangu, epuka kuzaa na mume WA MTU kama unataka mtoto wako apate mapenzi kamili ya Baba na Mama.

Mke anayomamlaka na Haki zote kumzuia mume wake kutotoa Pesa yoyote nje ya familia. Sio ajabu Wake wakiona Waume zao wanawatoto nje wakapandisha gharama za Maisha ndani ya familia kama kuwapeleka Watoto shule za gharama na matumizi mengi yawe juu kusudi mtoto wako akose kabisa Pesa ya mume wake.

Sarah alimshawishi Ibrahimu kumfukuza Hajiri na mtoto wake waondoke katika nyumba. Ibrahimu Baba wa Imani Kwa mujibu wa Dini ya Uyahudi, uislam na Ukristo akamfukuza Hajiri na mwanaye. Kama Hicho kisa haujapata picha jinsi Hali ilivyo endapo utazaa na Mume WA MTU basi utakuwa unamatatizo.

Acha kuharibu Maisha yako. Acha kuharibu Maisha ya mwanao utakayemzaa. Zaa na Mwanaume wako.

Acha kuvuruga nyumba za Watu. Usiwe Mkosi na janga katika Maisha yako.

Epuka kuolewa MKE mwenza, hakuna kitu kama Hicho. Ni kujidanganya tuu. Ni tamaa zetu wanaume na ubinafsi wetu. Hakunaga mambo ya hivyo. Ni kuharibu Maisha tuu.

Ni Bora uwe mvumilivu na subira. Mpaka mume wako atakapofika ndio ufanye Maisha na kuanzisha familia Naye. Dunia ya sasa sio lelemama.

Ukivunja Kanuni za asili hata ungeunda sheria Kali vipi lazima mambo yazidi kuwa magumu.

Hakunaga msamiati usemao alinidanganya hana MKE. Huo ni Uongo mkubwa. Ulithibitishaje maneno yake.
Mwanaume yeyote kama upo serious naye na unahitaji awe Mumeo sharti umpe Kanuni zako kupima Nia yake. Mwambie afanye hima akuoe.

Elewa kuwa Mwana mpumbavu ni mzigo Kwa Mamaye, na hii inatokana na sababu kuwa Mama ndiye amebeba dhamana ya mtoto.

Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Punguza ujuaji dogo unapomwagia ndani unategemea nini? tunza damu yako
 
Sio kila jambo ulizungumze hata kama hilifahamu unaonesha bado kijana mdogo sana ambaye huyajui mambo kiuhalisia wala maisha halisi ila unatumia mihemko na chuki dhidi ya wanawake,

Kifupi ulichoandika ni hisia na mtazamo wako wa chuki dhidi ya wanawake, ngono hatendi mwanamke pekee kama ni kosa limetendwa na wote mwanamke kwa mwanaume na hatia ni ya wote na ukitazama kwa umakini aliye na mke akazaa nje ametenda kosa la kuzaa na kusaliti mke anatakiwa kubeba hatia zaidi.

Jukumu la kulea ni la wazazi na si upuuzi uliondika hapo, acha kuhamasisha watoto kukosa haki zao za malezi kutoka kwa baba zao kisa kutafuta sifa ya kuandika maandiko mengi ya ajabu mitandaoni, Huna maana bro.
Huyu dogo ni mpumbavu sana nisha wahi kumushauri sio kila kitu lazima aandike , imagine mtu mzima una ndoa yako unaenda kulala na binti vichochoroni huko baadae unamwachia mwenzako mzigo , ni mpumbavu tu anae weza kula , kulala bila kuwaza damu yake inateseka mahali flani
 
Mbona sasa kwa huu uandishi wako unaonekana wewe uliye na experience na maisha hakuna unalolijua kuhusu maisha yenyewe.

Mleta uzi kasema wazi kuwa wanawake muwakalie mbali wanaume waliopo katika ndoa yaani wasijihusishe na wanaume za watu kimapenzi waishie salamu tu baasi.

Sasa wewe unakuja kumponda kuwa hayupo sahihi, haya sasa wewe uliye sahihi hebu tuambie vema unampango gani na watoto wa watu wa kike?!

Je unawasapoti wazae na wanaume za watu na kama hausapoti mbona umekuja kumkataza mleta uzi asikemee uovu wa kuzaa na wanaume za watu.
 
Mimi na wewe Nani ameandika hisia na mtazamo?
Unajua maana ya uhalisia?
Kwa Akili yako hata kama ni ndogo, ni Watoto wangapi hawatunzwi na Baba zao kisa na mkasa ni kuzaliwa nje ya mfumo wa Ndoa?

Lazima ujue zipo sheria, Maoni na mtazamo ambazo kamwe haziwezi kubadili Nature/asili.

Kiasili mtoto anatakiwa alelewe na Baba na Mama Full stop, kutokea Aina yoyote ya kutengana au kuingilia mahusiano ya Watu ni kumkosesha Haki mtoto atakayezaliwa nje ya mfumo.

Wewe Kwa Akili yako kisoda, badala uone andiko hili liwahamasishe Wanawake wawe Makini na waache kubeba mimba Kiholela pasipo ndoa wewe unaleta dhana zako za kipuuzi ati ninachuki.

Alafu tofautisha Kufanya ngono na Kupata mimba.
Jukumu la Kupata mimba lipo Chini ya Mwanamke na sio vinginevyo.

Hata Dunia ipinduke, Mwanamke ndiye Mhanga namba moja wa matokeo ya ngono.
Wewe hufai kuwa mwanaume chagua jinsia tofauti,uanaume ni majukumu
 
Huyu dogo ni mpumbavu sana nisha wahi kumushauri sio kila kitu lazima aandike , imagine mtu mzima una ndoa yako unaenda kulala na binti vichochoroni huko baadae unamwachia mwenzako mzigo , ni mpumbavu tu anae weza kula , kulala bila kuwaza damu yake inateseka mahali flani
Sahii kabisa,
Sio ujanja kutelekeza damu yako
Mwanaume lazima uwajibike kwa starehe zako
 
Mbona sasa kwa huu uandishi wako unaonekana wewe uliye na experience na maisha hakuna unalolijua kuhusu maisha yenyewe.

Mleta uzi kasema wazi kuwa wanawake muwakalie mbali wanaume waliopo katika ndoa yaani wasijihusishe na wanaume za watu kimapenzi waishie salamu tu baasi.

Sasa wewe unakuja kumponda kuwa hayupo sahihi, haya sasa wewe uliye sahihi hebu tuambie vema unampango gani na watoto wa watu wa kike?!

Je unawasapoti wazae na wanaume za watu na kama hausapoti mbona umekuja kumkataza mleta uzi asikemee uovu wa kuzaa na wanaume za watu.
Wewe ndio sufuri kabisa. Watoto wengi wa kike wanaingizwa mkenge kwa kudanganywa kuwa mwanaume aliezaa nae hana mke wengi wanakuja kujua badae.

Halafu hizi ndoa zina mambo mengi wengi wanaenda nje kutafuta faraja matokeo yake mwansume anapenda kweli mchepuko mpka anaamua kuzaa nae. Kwanini usitunze damu yako?
 
Tafsiri yake ukiwachepuko pambana mume wa mtu akumegee chako mapema
Nimesema huo kama mfano tu, wa kuwa mara nyingi wanawake tunakuwa wahanga kwa kujitakia. Unatoka na mume wa mtu na unajua. Anakuletea hela analala kwako unaona kama vile hampendi mke wake
unajiachia unabeba mimba kwa akili zako timamu halafu leo hii uende kwa mke mkubwa udai urithi inaingia akilini.Basi wawe wanajiongeza waombe mitaji wafanye japo biashara ili walee hao watoto . Lkn hakuna wanataka hela za mtelezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalenda ya uzazi Mungu kaiweka kwa mwanamke. Hivyo anapaswa kujijua na kuchukua tahadhari kuepuka mimba zisizo tarajiwa.

Utamlaani Mwanaume kukutelekeza lakini itakuwa kama dua la kuku lisilompata mwewe.
 
Back
Top Bottom