Mkuu, ukiwa 40+ na ubao bado unasoma 5–0, labda kosa ni kuendelea kufikiria kwamba lazima ushinde ule mchezo uleule kwa matokeo ya 5–5. 😂😂
Kipindi cha pili kinaweza kuwa sio cha kusawazisha ila ni cha kucheza kwa akili
Zingatia yafuatayo kama upo 40+
1. Jikubali ulipo bila kujidharau.
2. Acha kutumia nguvu nyingi kwenye vitu ambavyo huwezi kuvibadilisha. 3.Chagua kile ambacho bado unaweza kukijenga; afya, ujuzi, biashara/kazi, mahusiano mazuri, nidhamu ya fedha na amani ya akili.
Na muhimu zaidi, usiingie kwenye mashindano ya maisha ya watu wengine.
Kuna mtu alianza 2–0, mwingine 5–0, mwingine 0–5. Hatuanzi sehemu moja
Kama huwezi kutoa sare, basi punguza tofauti. Kama huwezi kubadilisha matokeo yote, basi hakikisha watoto wako wanaanza mchezo wao wakiwa mbele kuliko ulipoanzia wewe
Kwa hiyo kwa wewe uliye 40+, sio lazima kumaliza 5–5”. Wakati mwingine ushindi ni kutoka 5–0 hadi kuacha uwanja ukiwa umejenga kitu ambacho hakikuwepo kabla 👏👏👏
Na bado mkuu… mpaka refa apulize filimbi ya mwisho, mchezo haujaisha