Tajiri Kichwa
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 9,021
- 22,016
Sawa, nashukuru mkuuUtaondoka kwenye mnyororo huo kwa kufanya maamuzi katika mambo yako. Mtaji wa fedha kwako ni changamoto ila tambua, MUDA, UJUZI, NGUVU pia unaweza tumia kujipatia kipato.
Kikubwa kua na plan ndogo. Jifunze kuingiza shillingi mia 200 baada ya mida ifike 400, endelea ikuza na kuikuza.
Nimekuelewa viziri mkuu.Kama ushauri wangu utakuwa na maana uchukue, kama hauna maana tupa kapuni!
✓ jitenge na mnyororo wa ukoo wenu kiroho, hapa mtafute sheikh akupigie dua, anakutenganisha! Ukoo wako unaanza rasmi kuanzia kwako! Make issue kama hii hurithishwa (sometimes) ungelikuwa Mwanza ningelikupa address ya sheikh!
✓Au, tafuta mtaji! Anza biashara yako hata kama ni ya kawaida tu, kisha njoo Kawe uchukue mafuta ya Arise and Shine! (Nimeshuhudia wengi wente situation kama yako, wengine nimekuwa majirani nao), kama huamini uko, tafuta mafuta ya masheikh sanasana ya Qudra! tumia!
✓ukifanya biashara sahau kabisa kuwa mimi nina degree, hutoendelea kamwe, ikiwezekana kaishi mkoa mwingine mbali na huo ulikosomea chuo ili kuwa huru kufanya biashara zako!
Umasikini mbaya sana, fanya kazi zenye risk kubwa utatoboa vinginevyo utabaki kuwa mtu wa simulizi tu za maisha ya watuFamilia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.
Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.
Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.
NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo. Ahsanteni.
Habari na Amani ya Mungu iwe juu yako;Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.
Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.
Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.
NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo. Ahsanteni.
toka umasaini acha mila zote jichanganye mikoa mingine ishi kichanganyikeni usitafte ndugu hata mmoja katafte pesa mpk malengo yatimie oa endeleza pesa hakikisha ndugu hao wakutafte wewe sio wewe uwatafte vingnevyo unatafta kurejea km wao.Maasai. Lakini imagine sina hata mbuzi
usiishie kwenye ucha Mungu tu ongeza na kufanya kazi kwa bidii na maarifa pia ishi kwa malengo na heshimu unachokipataMkuu ni kweli kwamba nikiwa mcha-Mungu sana itasaidia?!
Nataka nianze hili zoezi
Nimekuelewa vuzuri mkuu. Nimeokoka na ninasali Pentecost. Naomba muongozo wa kuvunja maagano na kuangusha hizo madhabahu. AhsanteHabari na Amani ya Mungu iwe juu yako;
wengi wamesema mengi lakini sio wote wamegusa sababu hasa ni nini na nn chakufanya.
nitakueleza ukweli ingawa sio wote watanielewa na kukubali kwasababu asiyejua na hajui hajui kama hajui mpaka atakapojua ( samahani kwa lugha ngumu)
Maisha ni rohoni na yanadhihirka (yanatokea) mwilini. namaanisha kila kitu kinaanza katika ulimwengu wa roho kwanza kabla hujaona yakitukia katika ulimwengu tunao ouna. Ulimwengu wa roho una miaka mingi mno kuliko maisha tunayo ishi, pia unasiri za kutosha.
kabla chochote hakijafanyika kinaaza rohoni kwanza, mfano unaposema kwenu wote ni masikini na mnapitia mambo magumu... hiyo ni tendo liko katika ulimwengu wa roho. hata mmoja wenu akijitahidi anaweza enda juu kidogo na akaanguka chini kwa nguvu sana.
kinachosababisha ni nguvu ya giza/ shetani/ kupitia ama uchawi ama mizimu ambayo wamefanya maagano fulani na kuweka mipaka fulanifulani. Ukifuatilia ukoo wenu utagundua, kwamba wazee walitumikia na kujihusisha na miungu na waliweka maagano fulanifulani, wakitoa sadaka na matambiko.na waliishi maisha fulani ambapo inawalazimisha ukoo wote waishi maisha hayohayo. waliweka madhabahu pia, ama kwenye miti ama milima ama sehemu nyinginezo.
Namna ya kutoka katika mnyororo huo ni abahu, vingenevyo hamna namna. Kulipa sadaka ambazo zilitolewa ni kwa kutoa sadaka kubwa zaidi ya zile zilitolea. Habari njema ni kwamba DAMU YA YESU ni SADAKA iliyo kubwa kuliko sadaka zote na popote na kwa wakati wowote. kwa hiyo njia pekee ya kupoke auponyaji wako ni kukutana na YESU atakutoa wewe na ndugu zako na ukoo wako.
inasomeka kama ni rahisi, ni kweli - rahisi lakini ina gharama ya IMANI na UVUMILIVU kwa maana ya muda na BIDII, UTII na SHAUKU.
naamini nimesaidia kwa sehemu;
Ahsante sana mkuutoka umasaini acha mila zote jichanganye mikoa mingine ishi kichanganyikeni usitafte ndugu hata mmoja katafte pesa mpk malengo yatimie oa endeleza pesa hakikisha ndugu hao wakutafte wewe sio wewe uwatafte vingnevyo unatafta kurejea km wao.
Ahsante mkuuusiishie kwenye ucha Mungu tu ongeza na kufanya kazi kwa bidii na maarifa pia ishi kwa malengo na heshimu unachokipata
Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Kalumanzila?!Kwa njia gani! Anza na kalumanzila ambae sio tapeli! Ila sitaki sana kuingia kwa undani nisije nikachafue imani yako. Mimi ni mlala hoi ila marafiki zangu waliothubutu wapo juu, matawi ya juu.
Sent using Jamii Forums mobile app