Ukoo wetu wote ni masikini. Naombeni ushauri Nawezaje kukata huu mnyororo wa umaskini?

Ukoo wetu wote ni masikini. Naombeni ushauri Nawezaje kukata huu mnyororo wa umaskini?

Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.

Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.

Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.

NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.

Ahsanteni.
Usikute kuna ndugu ama jamaa wamewafunga msifanikiwe kwani wameona kitu kwenu.
 
Mimi sio tajiri

Tushauriane tufanyie kazi wote mimi na wewe tufanikiwe wote mimi na wewe mkuu.. tutajirike

Cha kwanza kukikagua kizazi chako wadhaifu kwenye mambo yapi? Yaani wanapenda au walikuwa wanapenda mambo gani? Ambayo yanawafelisha.. na wewe uzikatae hizo tabia zilizo au zinazo wafelisha..na unabidi ujue wewe ndio mwanzo wa mafanikio kama hakuna mtu hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa/ kutajirika ki-kweli kweli

Yaani kwa mfano ; kwenu hakuna mtu mwenye uthubutu wa kuanzisha biashara.. “ wewe ndio unatakiwa ujifunze sana mambo ya biashara na uchukue hatua za maksudi “ hakuna nguvu itayokufelisha kama utazingatia kila hatua na utakuwa na moyo wa kuendelea..” au hata kama kwenye hakuna mwenye uthubutu wa kufanya kazi mahala kwa mda mrefu kwa lengo la kupata pesa yake ya mtaji na kuanza biashara wewe inabidi uwe kipaumbele “ uweke hakiba nyingi kuliko unachotakiwa kutumia “ hakuna kitachofanya ufeli kama una nia ya kweli ya kufanikiwa..

Kama kwenu wana tabia za wizi, ulevi, uzinzi, ujambazi, ulozi, na mjumuiko wa tabia mbaya zote unabidi uikatae DNA ya tabia hizo na uanze upya yaani usizifate tabia hizo na uanze tabia njema “ mpaka waanze kushangaa huyu mbona tofauti kabsa na ukoo wake ili tu uyavutie mafanikio.. hakuna utakachofeli kama ukiamua kuzikataa tabia mbaya zilizopita au zilizopo kwenu..

Tumalizie..

Anza leo kukataa tabia za kwenu “” uenda ukaona kwa macho babu/bibi baba/mama zako wana jitihada makazini au kufungua mabiashara na yanashindwa sio uchawi Kuna vitabia vya ndani kabsa ambavyo mtu hataki wengine wazijue anazifanya ambazo zinamfelisha.. zikatae kuanzia leo hakuna sababu ya kuishi masikini miaka yote na kama kuna laana katika ukoo wenu pia una nafasi kubwa ya kuikataa laana hiyo rahisi tu.. Muelekee M/Mungu mapema atakutoa kwenye vifungo ambavyo hauvitaki..

Hakikisha unakataa DNA ya tabia mbaya ya kwenu na chukua DNA ya tabia njema za kwenu uende nazo ili ufanikiwe.. zingatia “ chunguza tabia zilizowafelisha kwenu na uzikatae na uanze kujipambania uokoe wengine katika ukoo/familia yenu..

Asante mkuu
Hii kuhusu tabia ni kweli kabisa...

Uvivu, kutaka makuu/makubwa bila kuanzia padogo, umbea, wivu, uchoyo, uvivu tena, kiburi kudhani unajua Kila kitu hutaki kusikiliza wengine, dharau, kudhulumu haki za wengine, bad spending, uvivu tena na tena n.k
 
Hii kuhusu tabia ni kweli kabisa...

Uvivu, kutaka makuu/makubwa bila kuanzia padogo, umbea, wivu, uchoyo, uvivu tena, kiburi kudhani unajua Kila kitu hutaki kusikiliza wengine, dharau, kudhulumu haki za wengine, bad spending, uvivu tena na tena n.k
Eeeh tuambie wewe rafiki wa GSM, BAKHRESA na MO DEWJI umepata kifungua kinywa gani hapo Serena Hotel??

Hivi huu ujuaji unasaidia nini?? Kwako wewe mtu masikini basi hasikilizi watu, mjuaji, mbishi, hajitumi, nk au sio??
 
Eeeh tuambie wewe rafiki wa GSM, BAKHRESA na MO DEWJI umepata kifungua kinywa gani hapo Serena Hotel??

Hivi huu ujuaji unasaidia nini?? Kwako wewe mtu masikini basi hasikilizi watu, mjuaji, mbishi, hajitumi, nk au sio??
Eeeish look at this one!!!
Ndo ulichopata kwenye andiko langu?? You have a comprehension problem!

Sasa mtoa mada uwe na akili kama za huyu unaachaje kuwa maskini...
 
Pole, Kwanza kuwa mcha Mungu sana

Pili Uombe Mungu akuondolee hilo kongwa la umaskini

Tatu toka kwenye mkoa wa kabila yako nenda mikoa mingine kaanze kutafuta maisha nimeona wengi wenye tatizo kama lako wakifanikiwa walipoenda mikoa mingine

Hata kwenye Biblia Ibrahim aliambiwa kama anataka maendeleo atoke nchi alikozaliwa aende mbali. Kuna maeneo ukiishi kama ni mwenyeji hufanikiwi akija mgeni anafanikiwa ondoka hilo eneo ukiona haliko vizuri kwako na ukoo wako.
Kwa Nini umshauri mtu kwa kutumia vifungu vya biblia kwani kakuambia Ni mkristo?
 
[emoji375][emoji375][emoji375][emoji375]
Kila kitu wanatumia reference ya vitabu vyao vya miaka 2000 iliyopita kwenye karne hii wanaona yesu kutembea juu ya maji Ni muujiza mkubwa , hawaoni ndege kuruka juu ikiwa na abiria 300 kma Ni maajabu makubwa[emoji849]
 
Nachukua nafasi hii kuwashukuru wale wote mliotenga muda wenu na kunipa ushauri ambao umenifumbua macho na kwa sehemu kubwa nimejifunza kwamba kuna mambo ya msingi napaswa kuyazingatia ili nijivue huu mnyororo wa umasikini. Ushauri pekee nilioupuuza ni ule wa kunitaka nijitafutie utajiri kwa njia zinazokwenda kinyume na sheria za nchi au kupitia nguvu za giza. Lakini kwa vyovyote vile nimenufaika na ushauri wenu. Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom