YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Kumjua Mungu si rahisi mtu utasikia mimi namjua Mungu sana hakuna akili ya kibinadamu hata mtu asome theolojia digrii zote duniani aweza kumjua Mungu ni kuomba tu Mungu atusaidie kumjua sababu akili zake hazichunguzikiKumcha Mungu Ni dawa kubwa Sana, hasa ukiwa na Imani thabiti, ondoa unafiki ktk kumcha Mungu, mf. Ukiwa peke yako gizani ona km Mungu anakuona
Hebu fikiria wakati dunia ilijaa Dhambi kila kona Biblia Inasema Mungu akamtuma Yesu aje kwa ajili ya wenye dhambi sio watakatifu wawe kanisa takatifu pekee la mitume katoliki au walokole Pentecoste!!
Naungana na Mtume Paulo alienda kwa wagiriki wakamwalika kuhubiri .Jengo lao waliandika kwa Mungu asiyejulikana!! Akawasifu kuwa walionyesha wako vizuri.
Kumjua Mungu hata mimi kila siku naomba tu anisaidie kumjua zaidi naimba sana wimbo wa kitabu cha nyimbo cha KKKT cha Mwmbieni Bwana unaosema Nataka nimjue Yesu nizidi kumfahamu...huwa nauimba kwa kumaanisha sababu kwa akili zangu sidhani kama naweza mjua Mungu au Yesu au Roho Roho Mtakatifu akili yangu finyu na ya kila binadamu finyu inahitaji neema tu ya Mungu kumjua kwa sehemu ndogo
Hata Eliya Alitaka kumjua Mungu aliishia tu kamuona kasehemu kadogo sijui. mgongoni
Ayubu alihoji kitabu cha Ayubu akaulizwa utanijuaje wakati hukuwepo nilipoumba mbingu na nchi?
Sidhani kama kuna yeyote aweza kumjua Mungu kikamilifu na kumpendeza Mia kwa Mia tuombeane
Yesu pekee ndie sauti ilitoka mbinguni kusema huyu ndie mwanangu mpendwa ninayependezwa Naye!!
Tuliobaki duniani ukiwemo wewe sauti hiyo haijawahi kuja kusema huyu mwenye ID ya Twende Wote wa jamii forums ndie mwanangu mpendwa ninayependezwa naye unajigesabia haki mwenyewe !!!