Ukoo wetu wote ni masikini. Naombeni ushauri Nawezaje kukata huu mnyororo wa umaskini?

Ukoo wetu wote ni masikini. Naombeni ushauri Nawezaje kukata huu mnyororo wa umaskini?

Habari na Amani ya Mungu iwe juu yako;
wengi wamesema mengi lakini sio wote wamegusa sababu hasa ni nini na nn chakufanya.

nitakueleza ukweli ingawa sio wote watanielewa na kukubali kwasababu asiyejua na hajui hajui kama hajui mpaka atakapojua ( samahani kwa lugha ngumu)

Maisha ni rohoni na yanadhihirka (yanatokea) mwilini. namaanisha kila kitu kinaanza katika ulimwengu wa roho kwanza kabla hujaona yakitukia katika ulimwengu tunao ouna. Ulimwengu wa roho una miaka mingi mno kuliko maisha tunayo ishi, pia unasiri za kutosha.
kabla chochote hakijafanyika kinaaza rohoni kwanza, mfano unaposema kwenu wote ni masikini na mnapitia mambo magumu... hiyo ni tendo liko katika ulimwengu wa roho. hata mmoja wenu akijitahidi anaweza enda juu kidogo na akaanguka chini kwa nguvu sana.

kinachosababisha ni nguvu ya giza/ shetani/ kupitia ama uchawi ama mizimu ambayo wamefanya maagano fulani na kuweka mipaka fulanifulani. Ukifuatilia ukoo wenu utagundua, kwamba wazee walitumikia na kujihusisha na miungu na waliweka maagano fulanifulani, wakitoa sadaka na matambiko.na waliishi maisha fulani ambapo inawalazimisha ukoo wote waishi maisha hayohayo. waliweka madhabahu pia, ama kwenye miti ama milima ama sehemu nyinginezo.

Namna ya kutoka katika mnyororo huo ni kuvunja maagano na kuangusha hizo madhabahu, vingenevyo hamna namna. Kulipa sadaka ambazo zilitolewa ni kwa kutoa sadaka kubwa zaidi ya zile zilitolea. Habari njema ni kwamba DAMU YA YESU ni SADAKA iliyo kubwa kuliko sadaka zote na popote na kwa wakati wowote. kwa hiyo njia pekee ya kupoke auponyaji wako ni kukutana na YESU atakutoa wewe na ndugu zako na ukoo wako.

inasomeka kama ni rahisi, ni kweli - rahisi lakini ina gharama ya IMANI na UVUMILIVU kwa maana ya muda na BIDII, UTII na SHAUKU.

nakazi tu kwamba, hata kama utaweka juhudi kaktka mikakati ye yote ile, huwezi toboa mpaka utengeneze hapo kwanza. haimaanishi uache fanya kazi kabisa ila elekeza nguvu kufunguluwa kwanza, baada ya hapo utafanikiwa

naamini nimesaidia kwa sehemu;
Umenena vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.

Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.

Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.

NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.

Ahsanteni.
Piga dili za magendo, wizi, jipendekeze kwa watawala (kuwa CHAWA wao), jiunge na Freemason, mtoe kafara mzazi wako mmoja, uza bangi/madawa ya kulevya! Faster utatoka na shida zote zitakwisha katika familia yako.

NB: Akili za mbayu wayu.......!!! Maana kwa upande wangu naamini maisha ni vita! Hivyo ni lazima kupambana mwanzo, mwisho!
 
Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.

Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.

Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.

NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.

Ahsanteni.
Saidia ukoo wako na familia Kwa vinavyowezekana usijilazimishe ... umaskini unaanziaga Hapo ...
 
Piga dili za magendo, wizi, jipendekeze kwa watawala (kuwa CHAWA wao), jiunge na Freemason, mtoe kafara mzazi wako mmoja, uza bangi/madawa ya kulevya! Faster utatoka na shida zote zitakwisha katika familia yako.

NB: Akili za mbayu wayu.......!!! Maana kwa upande wangu naamini maisha ni vita! Hivyo ni lazima kupambana mpaka mwisho.
Huo ni utajiri wa majuto.Hata kwa Mungu mafanikio yapo.
 
Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.
 
Marekani ilifanikiwa sana kuondoa umaskini kupitia ndoa za mchanganyiko

Wazungu vijana wa kiume marekani mfano ndoa zao waliooana sana wanawake wa kiyahudi na wanaume wa kiyahudi wakaoa wanawake wazungu wa Marekani

Matokeo ndio wakazaliwa mitoto yenye akili nyingi duniani kama Albert Einstein nk

Maasai kuoa na kuolewa na maasai mwenzie au mgogo kuolewa au kuoa mgogo mwenzie au muha kuoa au kuolewa na muha mwenzie au mndengereko kuoa au kuolewa na mndengereko mwenzie au mpimbwe kuoa au kuolewa na mpimbwe mwenzie au msafwa kuoa na kuolewa na msafwa mwenzie nk kama ukoo ni maskini uwezekano wa kutoka kwenye lindi la umaskini kiukoo pagumu ukoo huo ukitoboa ni neema ya Mungu!!!
 
Invest na uwe na akili ya kujiongeza

Kuwa na malengo ya mda mrefu sio Leo kesho unataka utoboe

Uwe mdadisi na mchumi haswa

Kuwa na mawazo yenye tija

Mchawi ni uzembe wa kufikiri

Nina mengi Ila chukua hayo
yani ingekuwa ivo bas mtaani hakuna ambaye angekuwa masikini maana umasikini ni mbaya na hauzoeleki
 
Marekani ilifanikiwa sana kuondoa umaskini kupitia ndoa za mchanganyiko

Wazungu vijana wa kiume marekani mfano ndoa zao waliooana sana wanawake wa kiyahudi na wanawake wa kiyahudi wakaolewa na wazungu wa Marekani

Matokeo ndio wakazaliwa mitoto yenye akili kama Albert Einstein nk

Maasai kuoa na kuolewa na maasai mwenzie au mgogo kuolewa au kuoa mgogo mwenzie au muha kuoa au kuolewa na muha mwenzie nk kama ukoo maskini uwezekano wa kutoka kwenye lindi la umaskini kiukoo pagumu ukitoboa ni neema ya Mungu
Ukiwekeza kwenye akili/ skill umasikini unakukimbia
 
Usijaribu huku mkuu, maagano ya huku ni mabaya.

Simama na Yesu. Soma Neno, sali sana, pia hama huo mkoa. kuwa karibu sana na Mungu. Kila kitu anza na Mungu, utamuona
ulishawahi kuwa tajiri alafu hayo maagano yakakushindwa? Na kama ulikuwa tajiri bus zako mbele uliandikaje?(onyo vigezo na masharti kuzingatiwa unaponijibu usiniambie ulimshúhudia kaka mjomba nk nataka ww)
 
Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.
Mkuu sehemu nyingi uliyonishauri nimepokea ushauri wako kwa mikono miwili. Lakini kwa hili ni kama unanihamasisha beyond the reality
 
Back
Top Bottom