Ukoo wetu wote ni masikini. Naombeni ushauri Nawezaje kukata huu mnyororo wa umaskini?

Ukoo wetu wote ni masikini. Naombeni ushauri Nawezaje kukata huu mnyororo wa umaskini?

Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege

Ni mtihani kujinasua, ikiwa hata ktk kazi hii ya kupalia mashamba na za zege watu wanashindwa kuona jinsi unavyotumia usomi wako kukamilisha vibarua hivyo.

Wanazuoni wanasema msomi siku zote hufanya na kutekeleza mambo tofauti na wale ambao hawajapata bahati ya elimu ya juu kama yako.

Jithamini nini kina kukwamisha hata kwa vitendo mbele wakati wa utekelezaji kazi za kupalia na kubeba zege kiasi huonekani kuongeza tija katika kazi yako ya sasa hivi unayoifanya .

Ukiweza kuonesha usomi wako unaleta tija ktk kazi yako ya sasa pamoja na genge zima la wabeba zege nao wana appreciate / sema 'yes' kwa mchango wako kivitendo kurahisisha kazi hiyo ya shuruba basi pasina shaka utapata maendeleo ya kiuchumi siku si nyingi zijazo.

Maana uwepo wapo hapo kibaruani unategemea utatatua changamoto na kupata uzoefu wa kufanya vizuri zaidi katika nafasi nyingine .
 
Mimi sio tajiri

Tushauriane tufanyie kazi wote mimi na wewe tufanikiwe wote mimi na wewe mkuu.. tutajirike

Cha kwanza kukikagua kizazi chako wadhaifu kwenye mambo yapi? Yaani wanapenda au walikuwa wanapenda mambo gani? Ambayo yanawafelisha.. na wewe uzikatae hizo tabia zilizo au zinazo wafelisha..na unabidi ujue wewe ndio mwanzo wa mafanikio kama hakuna mtu hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa/ kutajirika ki-kweli kweli

Yaani kwa mfano ; kwenu hakuna mtu mwenye uthubutu wa kuanzisha biashara.. “ wewe ndio unatakiwa ujifunze sana mambo ya biashara na uchukue hatua za maksudi “ hakuna nguvu itayokufelisha kama utazingatia kila hatua na utakuwa na moyo wa kuendelea..” au hata kama kwenye hakuna mwenye uthubutu wa kufanya kazi mahala kwa mda mrefu kwa lengo la kupata pesa yake ya mtaji na kuanza biashara wewe inabidi uwe kipaumbele “ uweke hakiba nyingi kuliko unachotakiwa kutumia “ hakuna kitachofanya ufeli kama una nia ya kweli ya kufanikiwa..

Kama kwenu wana tabia za wizi, ulevi, uzinzi, ujambazi, ulozi, na mjumuiko wa tabia mbaya zote unabidi uikatae DNA ya tabia hizo na uanze upya yaani usizifate tabia hizo na uanze tabia njema “ mpaka waanze kushangaa huyu mbona tofauti kabsa na ukoo wake ili tu uyavutie mafanikio.. hakuna utakachofeli kama ukiamua kuzikataa tabia mbaya zilizopita au zilizopo kwenu..

Tumalizie..

Anza leo kukataa tabia za kwenu “” uenda ukaona kwa macho babu/bibi baba/mama zako wana jitihada makazini au kufungua mabiashara na yanashindwa sio uchawi Kuna vitabia vya ndani kabsa ambavyo mtu hataki wengine wazijue anazifanya ambazo zinamfelisha.. zikatae kuanzia leo hakuna sababu ya kuishi masikini miaka yote na kama kuna laana katika ukoo wenu pia una nafasi kubwa ya kuikataa laana hiyo rahisi tu.. Muelekee M/Mungu mapema atakutoa kwenye vifungo ambavyo hauvitaki..

Hakikisha unakataa DNA ya tabia mbaya ya kwenu na chukua DNA ya tabia njema za kwenu uende nazo ili ufanikiwe.. zingatia “ chunguza tabia zilizowafelisha kwenu na uzikatae na uanze kujipambania uokoe wengine katika ukoo/familia yenu..

Asante mkuu
 
Mkuu,Uhai ni utajiri wa kwanza,Afya ni Utajiri wa pili,akili ni utajiri wa tatu,nguvu ni utajiri wa nne.
Fikra hasi ni umaskini wa kwanza.

Sasa nisikilize,You are responsible for yourself and not your clan.So habari za umaskini wa ukoo wako hazina uhusiano na utajiri wako ambao kwa kusoma andiko lako naona unao bali ukiendelea kuwaangalia basi utashangaa kweli na wewe unaendelea kuwa maskini.

Simama,Anza ulipo na ulicho nacho na Mungu wa Mbinguni atakuinua
 
Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.

Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.

Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.

NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.

Ahsanteni.

Ni ukweli kwamba umasikini wa kurisishana unaendana na ushirikina, na nuru uletwa na Imani.

Jaribu kufuata Yesu kwa moyo wa dhati, nina uhakika utakuwa ni mwanzo mwema wa kuelekea nuru.
 
Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.

Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.

Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.

NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.

Ahsanteni.
Mkuu umaskini ni laana, dawa yake ni kuachana nao.. Hivyo hatua ya kwanza ni kujitenga na hao ndugu zako yaani achahana nao kabisaa. Utakuja kunishukuru.
 
Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.

Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.

Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.

NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.

Ahsanteni.
Yaliyoliwa na nzige yameliwa na tunutu
 
Mambo ya ujamaa yametuharibu sana, ukiwa na pesa au kazi ndugu wanataka ziwe za ukoo au familia, mjomba shangazi, dada kaka n.k wote wanakutumbulia macho na lawama chungu nzima usipowasaidia.
Kabisa mm nimepambana mno na hilo na bado unajikuta huwezi.
Akiweza aende nje ya nje tu. Watu wanaishi huko na maisha yanaenda poa tu.
 
Utajiri ni hobby na sio KILA mtu ana dream kuwa tajiri.Pili ukimjua Mungu huwezi kuwa masikini.
Siri kubwa ya kufanikiwa ipo kwenye utoaji.
Jiulize kwann weupe usaidia Sana Afrika.
Kwahiyo masikini wote hawamjui MUNGU? we jamaa vipi? Tuondolee ujinga hapa.
 
Nimekuelewa viziri mkuu.

Mimi nipo tanga

Kama upo Tanga mjini fanya uondoke, ila pia kama upo popote pale ondoka nenda mkoa mwingine ukaanze maisha...potea kama miaka miwili mitatu hivi watu wakusahau kabisa na usiwe mwepesi ndugu na jamaa kujua uko wapi labda baba na mama, wengi wajue upo upo tu unahangaika...

huko utakapokuwa, jitahidi kupiga kazi sana na ibada, Muombe Mungu akulinde na uovu, fitna n ubaya wowote....hata ukipata mafanikio usijionyeshe kwenu, saidia baba na mama....wengine wajue wewe choka mbaya tu...

Mwisho kabisa ukitaka kuoa usioe kabisa huko kwenu nenda kaoe mikoa ya mbali huko hata ikiwezekana nchi nyingine... Ukizaa watoto usiwape majina toka ukoo wenu tafuta majina mapya kabisa ambayo hayapo kabisa kwenye ukoo wenu...
 
Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.

Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.

Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.

NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.

Ahsanteni.
Ni nini tofauti ya umasikini, ufukara na utajiri?
 
Ni nini tofauti ya umasikini, ufukara na utajiri?
Maskini akili anayo yaweza kuwa ya Omba Omba nk, fukara hata akili ya kuomba au kutafuta msaada kwa wenye uwezo hana ,Tajiri ni mtu anayejitosheleza kwa mahitaji yake yote muhimu bila kutegemea mtu kuanzia chakula, mavazi Malazi nk tofauti viwango tu ya utoshelevu mfano mwingine mwanae anasomesha Ulaya mwingine English Medium. TANZANIA
 
Njia nyingine ya kuondokana na umaskini kwenye ukoo ni ndoa za mchanganyiko

Mungu akikujalia kama wewe maasai kaoe mchaga Wanawake wa kichaga wanajua kuchacharika usioe maasai mwenzio au makabila yaliyozubaa
Ushauri wako 50% foolish! Wewe ni Mchagga?
 
Kwahiyo masikini wote hawamjui MUNGU? we jamaa vipi? Tuondolee ujinga hapa.
Una haja ya kuelewa,Kama Mungu ndie mmiliki wa mali zote pesa nk,Katu hawezi ruhusu watu wake wawe masikini.
Umasikini ni mpango wa shetani Ili watu wamkufuru Mungu,ukijiconnect na upande wa positive power huwezi kuwa masikini wa kukosa kabisa,Neema za Mwenyezi Mungu ni lazima zikutembelee , maisha ya kiMungu yana kanuni zake Ili upate.
 
Back
Top Bottom