Elias K
JF-Expert Member
- Oct 9, 2021
- 213
- 607
Familia yetu yote hakuna mwenye unafuu wa kiuchumi. Nikaangazia macho ndugu wa baba na mama, na wao wote ni masikini sana. Nikafuatilia historia ya mababu na wao walikuwa mafukara kabisa.
Nina shahada ya kwanza ila ninakaribia kumaliza mwaka tangu nimalize chuo lakini sijawahi kuifanyia kazi. Nafanya vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na za zege.
Najua hapa kuna watu wa namna mbalimbali. Naombeni msaada wa kujinasua katika hili wimbi la ufukara angalau niwe na unafuu wa maisha. Niweze kujikimu kwa uhakika wa chakula na malazi tu.
NB: siombi msaada wa pesa, naomba msaada wa Mawazo.
Ahsanteni.