Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Changamoto kubwa inayochangia mmonyoko wa maadili ni umaskini, malezi ya Mzazi mmoja, rushwa za ngono, utandawazi na kukosekana kwa Umoja katika malezi
 
Tatizo la ukosefu wa maadili kwenye jamii ni ubinafsi uliopitiliza wa siku hizi unaotokana na kuingia kwa sera za ubepari katika mataifa yetu. Leo hii mtoto wa kwako ni wa kwako, zamani mtoto alikuwa ni wa jamii nzima. Ukizingua mtaani mzazi au mtu mkubwa yoyote anakupa kichapo na taarifa zikifika home unaongezewa kichapo vilevile, leo hii mtoto akipigwa jirani tena kwa kufanya kosa fulani bhasi ujue kinaumana baina ya mzazi wa mtoto na huyu aliempiga. Wazazi wanalea watoto kama mayai. Mwisho kabisa, tumekuwa tukibeba kila kitu cha mtandaoni bila kuchuja. Utandawazi una mipaka yake lakini sisi tunabeba kila kitu. Kizazi cha 2030s kuendele sikipatii picha itakuwaje.
 
hatuongelei hapa 100% nikipata ja[o nusu percent ni ushindi mkubwa sana.

Kama ulikuwa huelewi, kumtumikia Mwenyezi Mungu ni kuitumikia jamii.

Mficha maradhi, kifo humuumbuwa.

Wewe ni shoga? Kama "ndiyo", tufahamishe ulianza vipi kuwa shoga ili iwasaidie wengine. Au kwa kuwa wewe shoga basi unataka wote wawe mashoga na au waupende ushoga?
 
Sasa rafiki yangu hapo pombe ni mmomonyoko wa maadili ? Yaani hamuoni raha bila kumnanga mzee pombe popote ilihali yeye hana shida na nyie .

Kaka pombe naomba itoe tafadhali mdogo wangu
 
Wewe kama mimi kasoro hapo kwenye pombe, japo si mlevi ni mnywaji huwa nakunywa kistaarabu na najua kipimo changu, huwa sinywi kulewa nakunywa for fun na ni mara moja moja sana
 
Hii ni battle kati ya millenials. Baby boomers na gen Z
Silent Gen na Baby Boomers hawahusiki sana hapa, kinachoshangaza Gen X na Millenials ndio wanaoongoza kuvilalamikia vizazi vya sasa, ambao ni Gen Z na Gen Alpha ilihali wao ndio wazazi wao respectively na ndio waliowalea
 
Vitabu vya dini ni muhimu sana, nyinyi wenyewe na watoto zenu wanyimeni vyote msiwanyime maadili mema, na hakuna pakuyapata maadii mema zaidi ya kwenye dini.
Itakua ni kwel kama baada ya dini kuletwa Africa maadili mema yaliongezeka, na kufika sasa tupo karibu kabisa na kilele cha maadili mema, kwasababu waumini wa dini ni wengi mno.
 
Sasa rafiki yangu hapo pombe ni mmomonyoko wa maadili ? Yaani hamuoni raha bila kumnanga mzee pombe popote ilihali yeye hana shida na nyie .

Kaka pombe naomba itoe tafadhali mdogo wangu
Ukitoa maji ,mbele ya maziwa pombe ndio kinywaji cha kale zaidi duniani, mtu kazaliwa 2003 anapigia kelel pombe.
 
Dini ndio msingi wa maadili mema kama ulikua hujui.
Kabla ya hizi dini zote Africa ilikuwa na maadili safi kabisa!


Baada ya hizi dini za kipumbavu kuja muafrica mkristo hawez kuoa muislam na kinyume chake!


Baada ya hizi dini kuja muafrica anakatazwa kula nguruwe.


Dini inamwambia mwafrica kuwa mwafrica mwingine asie muislam ni kafiri

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Kabla ya dini Africa mwanaume alikua mwanaume tu ,kulikua hakuna mwanaume mwanamke Africa.
 
Leo hii kumtafutia mtu, wakikwaruzana tu utasikia;

1. Kwanza hukuwa chaguo langu, ni fulani ndo kaniingiza chaka.

2. Pale mitaa ya kwenu nilikuwa namtaka fulani, wewe ukajipendekeza kwa niliyemtuma ukafanikiwa kuniingiza chaka

etc
 
Kabla ya dini Africa mwanaume alikua mwanaume tu ,kulikua hakuna mwanaume mwanamke Africa.
Haya matamaduni ya nje yamekuja kumuharibu muafrica badala ya kumjenga!

Boko Haram wanaua waafrica wenzao kisa dini


Alshabab wanaua ndugu zao kisa dini


Magaido ya msumbiji yanaua ndugu zao kisa dini


Na sijawahi kuona Muislam yoyote duniani akikemea mauaji ya hivi vikundi chini ya dini!



Dini za mwafrica, watu walikuwa wanaomba mvua na ukame unapotea kweli. Leo wamejaa wakina Mwamposa kazi kuuza chumvi na kutembea na wake za watu




Halafu Kuna mpuuzi anaona dini zina mchango.





Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Yote ya yote ila kina mwamposa mwakapesa πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Maadili ni nini??
Maadili gani yameporomoka Tanzania kwa sasa??
Mfano wako pia hauna mashiko.
 
Watu wanaachana na ujima
 
Ulitaka nieneze chuki za upagani?


Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.

Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?
Mbona wenye dini wengi ni wala Rushwa tangu karne na karne, pia huiba uchaguzi na kukandamiza wapinzani.
Haya ni maadili??
 
Tatizo kubwa zaidi la maadili katika nchi hii ni wizi wa pesa za umma na matumizi mabaya fedha za walipa kodi, mengine mengi ni Petty issues tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…