Ukraine ndani ya Urusi, inataka kumwondoa Putin Madarakani? Je hii ni dalili ya World War III?

We kilaza. Putin toka lini anaogopa haki za binadamu za NATO? dogo humjui Putin na hujui Russia. Yaani leo hii Putin ambaye alitakalo hakuna wa kumzuia anawaogopa hao Haki za Binadamu? Si ndo hao hao walisema ushoga. Akawaambia hataki kusikia huo upuuzi? Kuna mashtaka gani ya kumtisha Putin? Dogo hujui. Nyamaza. Kunywa uji ulale.. au.... 😁
Sio anaogopa anakiuka haki za kibinadamu...elewa hapo kwanza
 
Zelensky aliambiwa akimbie apewe hifadhi Poland jamaa alisema sihitaji hifadhi ntafia kwenye ardhi yangu naomba mnisaidie siraha tu huyu jamaa ni jasiri sana aisee kwa mazingira yale harafu akukimbia akaja kukumbia Putin kwenye mahandaki kwa kukimbia wakina Maghayo(Wagner) wakienda kuchukua Ikulu kwa miguu...
 
Habari yenyewe sky news hahhahah nyie tafuteni habari za maana hao wanajeshi wa Ukraine saivi wanajuta wanalia kilichowatuma kuingia kursk
Weka hiyo habari hapa.... Au ni ile umeambiwa na ustaadhi Kidimwi jana wakati tunakunywa kahawa? Usimsikilize yule Bwege alimlisha matango pori Ritz yeye na Sheikh Kundecha wakampa taarifa za uongo akaja kupost huku JF sasa anaona hata aibu.
 
Zelensky aliambiwa akimbie apewe hifadhi Poland jamaa alisema sihitaji hifadhi ntafia kwenye ardhi yangu naomba mnisaidie siraha tu huyu jamaa ni jasiri sana aisee kwa mazingira yale harafu akukimbia akaja kukumbia Putin kwenye mahandaki kwa kukimbia wakina Maghayo(Wagner) wakienda kuchukua Ikulu kwa miguu...
Ilinishangaza sana. Na ndo wanasema jamaa ni comedian. Yaani haya mambo sijui hata inakuaje. Mimi nliamini sana Russia. Lakini sasa inanipa wasiwasi sana. Huyu ndo Putin yule yule kweli?
 
We kilaza. Putin toka lini anaogopa haki za binadamu za NATO? dogo humjui Putin na hujui Russia. Yaani leo hii Putin ambaye alitakalo hakuna wa kumzuia anawaogopa hao Haki za Binadamu? Si ndo hao hao walisema ushoga. Akawaambia hataki kusikia huo upuuzi? Kuna mashtaka gani ya kumtisha Putin? Dogo hujui. Nyamaza. Kunywa uji ulale.. au.... 😁
Atakua kasahau kuwa ipo ndege ya abiria ilikua inafanana bendera na ya Ukraine ilipita anga la Russia Putin akaipiga bomu huko huko juu hakuna kitu kilisemwa na watu wa haki za binadamu...
 
Hiyo vita usifananishe na Simba na Yanga....wabongo wengi akili ndogo....nchi inaliwa na watu wa chache kwa kutumia jasho lenu la hizo kodi na tozo huko kwenye vocha nk ...sasa mambo ya nchi za nje utayajuwaje......wewe jikite huko simba na yanga ....zuchu....Kizimkazi.....kushadadia masisiemu
 
Kwanza utambue Urusi anapigana na NATO katika Ardhi ya Ukraine.

Hata hiyo oparesheni ya kushtukiza kuingia Jimbo la KURSK-Urusi, ni matokeo ya Intelijensia ya NATO kuwapa Ukraine na Majeshi ya NATO taarifa sahihi za Uwezo wa kijeshi wa Urusi KURSK.

Ukraine walitaka kuteka kinu Cha Nyukilia kilichopo KURSK ili kukitumia kufanya Negotiation.

Pili, kuilazimisha Urusi Kupunguza Majeshi Donbass kuyaleta KURSK baada ya kuona kule Donbass Urusi anatoa Kichapo na kuzidi kuchukua maeneo

Hata hivo, Urusi inajua hiyo NIA, Kichapo kitaendelea kote kote, iwe ni DONBASS, KURSK Kichapo Kiko pale pale

Inabidi ufaham, Urusi ni Nchi yenye Nyukilia , Kamwe NATO hawawezi kuishinda .

Kumwondoa Putin ni sawa na ndoto za Alinacha .
Kuna mengine uliyoandika ni 100% correct ila mengine uliyoyaandika hapo siyo halisia.

Kwa ujumla Russia inayapata matokeo ambayo hakuyatarajia kabisa. Na siyo kwa kupenda bali kwa kuzidiwa mbinu. Inaonekana intelijensia yake ni dhaifu. Vita viletegemewa viishe ndani ya siku 3, lakini kwa miezi miwili, Ukraine bila ya msaada wa nchi yoyote ilimfurusha Urusi kutoka Kyiv, na alipoteza askari wengi tena wenye ujuzi wa juu kabisa. Ile ilikuwa ni failare yake kubwa ya kwanza.
 
Atakua kasahau kuwa ipo ndege ya abiria ilikua inafanana bendera na ya Ukraine ilipita anga la Russia Putin akaipiga bomu huko huko juu hakuna kitu kilisemwa na watu wa haki za binadamu...
Leo anajisahaulisha anasema eti Putin anajali kelele za haki za binadamu.anasahau wapinzani wa Putin wanavyouawa na kukimbilia uhamishoni. Putin ni mbabe haambiliki. Tukubali ameshikwa pabaya. Hadi yule mhuni alitaka enda mwondoa Putin madarakan.na hakuwa na akili kihivyo zaidi ya kuwa na kundi la wahuni kama jeshi
 
Ilinishangaza sana. Na ndo wanasema jamaa ni comedian. Yaani haya mambo sijui hata inakuaje. Mimi nliamini sana Russia. Lakini sasa inanipa wasiwasi sana. Huyu ndo Putin yule yule kweli?
Putin ana nguvu sana ila wanajeshi wake wengi sio Wazalendo na kumbuka wengi wamelazimishwa kuingia Vitani yaani Russia ingekua wanajeshi wake ni Wazalendo kama wa Ukraine vita ingeisha muda mrefu angalia hata afya za hao wanajeshi wa kirusi na umri wao unaona ni wale machalii na wanaokotwa tu walinde sehemu swala la wao kutekwa ni kawaida tu na Putin bado utamuona kwenye TV yake kama yule waziri wa Iraq Ali Sahafu huku wahuni wakimega maeneo..
 
Leo anajisahaulisha anasema eti Putin anajali kelele za haki za binadamu.anasahau wapinzani wa Putin wanavyouawa na kukimbilia uhamishoni. Putin ni mbabe haambiliki. Tukubali ameshikwa pabaya. Hadi yule mhuni alitaka enda mwondoa Putin madarakan.na hakuwa na akili kihivyo zaidi ya kuwa na kundi la wahuni kama jeshi
Yule muhuni alikua mpishi wake kwa kuwa alikua anamwamini akampa dili la kusimamia biashara ya madini kutoka kwenye Nchi zenye vita Afrika baadae alipoanzisha vita akamrudisha kwa kuwachukua wafungwa na vijana ili wakapigane yaani muhuni akawa anapewa pesa baadae muhuni akaanza kelele kuwa hawapewi siraha za kutosha askari wake wanakufa hovyo na ndio kikawa chanzo cha muhuni kuitaka Ikulu ya Moscow...
 
Kuna mengine uliyoandika ni 100% correct ila mengine uliyoyaandika hapo siyo halisia.

Kwa ujumla Russia inayapata matokeo ambayo hakuyatarajia kabisa. Na siyo kwa kupenda bali kwa kuzidiwa mbinu. Inaonekana intelijensia yake ni dhaifu. Vita viletegemewa viishe ndani ya siku 3, lakini kwa miezi miwili, Ukraine bila ya msaada wa nchi yoyote ilimfurusha Urusi kutoka Kyiv, na alipoteza askari wengi tena wenye ujuzi wa juu kabisa. Ile ilikuwa ni failare yake kubwa ya kwanza.
Watu hawataki kukubali jambo hili. Na ikitokea NATO inaamua kwa miguu miwili kumwondoa Putin inamwondoa.inaonekana kama Putin hana ufuasi mkubwa ndani ya nchi yake.hakubaliki sana. Lakini hata upande wa silaha zaisi ya Nuklia ni wa kawaida si ile tuliaminishwa miaka na miaka ya karibuni.
 
Hili jambo lilinishangaza sana. Kundi tu la wahuni liliamua kuwa linataka kumwondoa na ikabidi akimbie kujificha. Kuna mambo nashindwa yaelewa kabisa kuhusu Putin. Jinsi ambavyo tumekuwa tumiaminishwa na uhalisia kwa sasa ulivyo. Kuna tatizo sehemu. Au huyu si Putin Original?
Tuliaminishwa Ukitoa USA mbabe mwengine wa kivita Duniani ni Urusi. Kwamba Dunia nzima anaemuweza USA ni Urusi tu. Na anaemuweza Urusi ni USA tu.

Hata kama Urusi huyu sio yule wa enzi za Mikhail Gorbachev lakini bado alibeba asilimia kubwa ya nguvu ya iliyokua USSR.

Kwamba USA akiamua kupiga mkono na nchi ingine ile Duniani isiyo USSR ni dakika tu mtu chali, vile vile Kwa Urusi. Hii vita ya Ukraine inafikirisha sana Kwa kweli.
 
Wataalam wa masuala ya kivita, baada ya Ukraine kuizuia Urusi kupata ushindi ilioutaka kwa kipindi cha miezi miwili, huku Ukraine ikipigana bila ya msaada wa nchi yoyote, na kufa ikiwa kuyafurisha majeshi toka Kyiv, walikiri kuwa uwezo wa kijeshi wa Urusi ulikuwa over-exagerated. Na hata Urusi yenyewe ilikuwa ikiamini ina uwezo mkubwa sana wa kivita, lakini vita hii imeifanya ijitafakari, na kuufahamu uwezo wake halisia.
 
Tuliaminishwa Ukitoa USA mbabe mwengine wa kivita Duniani ni Urusi. Kwamba Dunia nzima anaemuweza USA ni Urusi tu. Na anaemuweza Urusi ni USA tu.

Hata kama Urusi huyu sio yule wa enzi za Mikhail Gorbachev lakini bado alibeba asilimia kubwa ya nguvu ya iliyokua USSR.

Kwamba USA akiamua kupiga mkono na nchi ingine ile Duniani isiyo USSR ni dakika tu mtu chali, vile vile Kwa Urusi. Hii vita ya Ukraine inafikirisha sana Kwa kweli.
Mataifa mbalimbali, japo mengine ni madogo, baadhi yamejizatiti sana katika tekinolojia ya kivita. Hiki siyo kipindi cha kusema nchi kubwa inaweza kwenda nchi yoyote kwa sababu ni ndogo, ikaipiga ndani siku kadhaa. Israel , mwaka 1967 ilizipiga nchi 6 za Kiarabu kwa siku 6 tu. Lakini leo, kupambana tu na Hamas imechukua zaidi ya miezi 10, na bado haijaweza kupata matokea iliyoyahitaji kwa 100%.
 
Back
Top Bottom