Ukraine ndani ya Urusi, inataka kumwondoa Putin Madarakani? Je hii ni dalili ya World War III?

Sio anaogopa anakiuka haki za kibinadamu...elewa hapo kwanza
 
Zelensky aliambiwa akimbie apewe hifadhi Poland jamaa alisema sihitaji hifadhi ntafia kwenye ardhi yangu naomba mnisaidie siraha tu huyu jamaa ni jasiri sana aisee kwa mazingira yale harafu akukimbia akaja kukumbia Putin kwenye mahandaki kwa kukimbia wakina Maghayo(Wagner) wakienda kuchukua Ikulu kwa miguu...
 
Habari yenyewe sky news hahhahah nyie tafuteni habari za maana hao wanajeshi wa Ukraine saivi wanajuta wanalia kilichowatuma kuingia kursk
Weka hiyo habari hapa.... Au ni ile umeambiwa na ustaadhi Kidimwi jana wakati tunakunywa kahawa? Usimsikilize yule Bwege alimlisha matango pori Ritz yeye na Sheikh Kundecha wakampa taarifa za uongo akaja kupost huku JF sasa anaona hata aibu.
 
Ilinishangaza sana. Na ndo wanasema jamaa ni comedian. Yaani haya mambo sijui hata inakuaje. Mimi nliamini sana Russia. Lakini sasa inanipa wasiwasi sana. Huyu ndo Putin yule yule kweli?
 
Atakua kasahau kuwa ipo ndege ya abiria ilikua inafanana bendera na ya Ukraine ilipita anga la Russia Putin akaipiga bomu huko huko juu hakuna kitu kilisemwa na watu wa haki za binadamu...
 
Hiyo vita usifananishe na Simba na Yanga....wabongo wengi akili ndogo....nchi inaliwa na watu wa chache kwa kutumia jasho lenu la hizo kodi na tozo huko kwenye vocha nk ...sasa mambo ya nchi za nje utayajuwaje......wewe jikite huko simba na yanga ....zuchu....Kizimkazi.....kushadadia masisiemu
 
Kuna mengine uliyoandika ni 100% correct ila mengine uliyoyaandika hapo siyo halisia.

Kwa ujumla Russia inayapata matokeo ambayo hakuyatarajia kabisa. Na siyo kwa kupenda bali kwa kuzidiwa mbinu. Inaonekana intelijensia yake ni dhaifu. Vita viletegemewa viishe ndani ya siku 3, lakini kwa miezi miwili, Ukraine bila ya msaada wa nchi yoyote ilimfurusha Urusi kutoka Kyiv, na alipoteza askari wengi tena wenye ujuzi wa juu kabisa. Ile ilikuwa ni failare yake kubwa ya kwanza.
 
Atakua kasahau kuwa ipo ndege ya abiria ilikua inafanana bendera na ya Ukraine ilipita anga la Russia Putin akaipiga bomu huko huko juu hakuna kitu kilisemwa na watu wa haki za binadamu...
Leo anajisahaulisha anasema eti Putin anajali kelele za haki za binadamu.anasahau wapinzani wa Putin wanavyouawa na kukimbilia uhamishoni. Putin ni mbabe haambiliki. Tukubali ameshikwa pabaya. Hadi yule mhuni alitaka enda mwondoa Putin madarakan.na hakuwa na akili kihivyo zaidi ya kuwa na kundi la wahuni kama jeshi
 
Ilinishangaza sana. Na ndo wanasema jamaa ni comedian. Yaani haya mambo sijui hata inakuaje. Mimi nliamini sana Russia. Lakini sasa inanipa wasiwasi sana. Huyu ndo Putin yule yule kweli?
Putin ana nguvu sana ila wanajeshi wake wengi sio Wazalendo na kumbuka wengi wamelazimishwa kuingia Vitani yaani Russia ingekua wanajeshi wake ni Wazalendo kama wa Ukraine vita ingeisha muda mrefu angalia hata afya za hao wanajeshi wa kirusi na umri wao unaona ni wale machalii na wanaokotwa tu walinde sehemu swala la wao kutekwa ni kawaida tu na Putin bado utamuona kwenye TV yake kama yule waziri wa Iraq Ali Sahafu huku wahuni wakimega maeneo..
 
Yule muhuni alikua mpishi wake kwa kuwa alikua anamwamini akampa dili la kusimamia biashara ya madini kutoka kwenye Nchi zenye vita Afrika baadae alipoanzisha vita akamrudisha kwa kuwachukua wafungwa na vijana ili wakapigane yaani muhuni akawa anapewa pesa baadae muhuni akaanza kelele kuwa hawapewi siraha za kutosha askari wake wanakufa hovyo na ndio kikawa chanzo cha muhuni kuitaka Ikulu ya Moscow...
 
Watu hawataki kukubali jambo hili. Na ikitokea NATO inaamua kwa miguu miwili kumwondoa Putin inamwondoa.inaonekana kama Putin hana ufuasi mkubwa ndani ya nchi yake.hakubaliki sana. Lakini hata upande wa silaha zaisi ya Nuklia ni wa kawaida si ile tuliaminishwa miaka na miaka ya karibuni.
 
Tuliaminishwa Ukitoa USA mbabe mwengine wa kivita Duniani ni Urusi. Kwamba Dunia nzima anaemuweza USA ni Urusi tu. Na anaemuweza Urusi ni USA tu.

Hata kama Urusi huyu sio yule wa enzi za Mikhail Gorbachev lakini bado alibeba asilimia kubwa ya nguvu ya iliyokua USSR.

Kwamba USA akiamua kupiga mkono na nchi ingine ile Duniani isiyo USSR ni dakika tu mtu chali, vile vile Kwa Urusi. Hii vita ya Ukraine inafikirisha sana Kwa kweli.
 
Wataalam wa masuala ya kivita, baada ya Ukraine kuizuia Urusi kupata ushindi ilioutaka kwa kipindi cha miezi miwili, huku Ukraine ikipigana bila ya msaada wa nchi yoyote, na kufa ikiwa kuyafurisha majeshi toka Kyiv, walikiri kuwa uwezo wa kijeshi wa Urusi ulikuwa over-exagerated. Na hata Urusi yenyewe ilikuwa ikiamini ina uwezo mkubwa sana wa kivita, lakini vita hii imeifanya ijitafakari, na kuufahamu uwezo wake halisia.
 
Mataifa mbalimbali, japo mengine ni madogo, baadhi yamejizatiti sana katika tekinolojia ya kivita. Hiki siyo kipindi cha kusema nchi kubwa inaweza kwenda nchi yoyote kwa sababu ni ndogo, ikaipiga ndani siku kadhaa. Israel , mwaka 1967 ilizipiga nchi 6 za Kiarabu kwa siku 6 tu. Lakini leo, kupambana tu na Hamas imechukua zaidi ya miezi 10, na bado haijaweza kupata matokea iliyoyahitaji kwa 100%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…