Ukraine ndani ya Urusi, inataka kumwondoa Putin Madarakani? Je hii ni dalili ya World War III?

Unaongea kana kwamba russia kashindwa,kumbe kateka 20+%ya ukraine,huko kursk husikii CNN wakidai ukraine kusonga,jua kichapo siyo cha mchezo
Elewa.watu hawasemi Ukrain kashinda.ila tunashangaa why 2 yrs now?ilipaswa iwe ndani ya week au 72 hrs kama ambavyo alisema Putin. Hatukutegema Ukraine itaanza shambulia Russia.yaani Temeke Market inacheza na Barcelona au Man United.nayo inashambulia?ilipaswa ijilinde tu kupunguza idadi ya magoli.
 
We uliamini nchi yenye ukubwa wa ukraine kutekwa kea siku TATU?..vita vina propaganda zake,kwanza walisema ni smo,na lengo si kuiteka nchi yote,kuteka nchi siyo smo
Kwa hiyo Putin alikuwa anajitekenya na kucheka mwenyewe?tusipomuamini Putin tukuamini wewe sasa? Yaani Jasusi kama Putin asiaminike.
 
Dogo haya yote unalishwa na Ustaadhi Kitinku na Sheikh Kubemendea. Huelewi kitu. Nenda kawaulize jana kwa nini waligombana nami kwenye lile group letu. Za kuambiwa changanya na zako usiwe kama Mbayuwayu....
 
na ndio ukawa mwisho wake
 
Sawa bwana Putin πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ umeipata kijiwe gani mkuu
 
Unaweza kushangas hata mapambano hapo Kursk yakachukua miaka
 
Putin alibet, he did not expect Marekani ataisupport Ukraine kwa muda mrefu na hela nyingi.

Kumbe Marekani na Makoloni yake walikuwa wameiwaza vita Miaka mingi mbele
 
sasa we huoni hapo urusi anapigana na marekani na washirika wake wote,,angekua marekani peke ake vita ingekua imeisha asubuhi tu
 
Putin alibet, he did not expect Marekani ataisupport Ukraine kwa muda mrefu na hela nyingi.

Kumbe Marekani na Makoloni yake walikuwa wameiwaza vita Miaka mingi mbele
Ina maana hakuwa na taarifa nzuri za kiintelejensia.au alikuwa anadhani ule mkwara wake kuwa Ukraine wakisaidiwa atatumia Nuklia ungeendelea kuwaogopesha NATO? JAMAA WAME MJARIBU WAMEMUONA anawezekana kabisa.hata akimpiga Ukraine bado ame ji expose kuwa si wa kutisha kiasi hicho.
 
Mimi nimekuwa Pro Urusi na Irani kwa muda mpaka nilipoanza kupata akili. Nikagundua Marekani wana akili. Huwaoni wakionesha silaha zao hovyo hovyo. Wanazificha. Irani , Korea, Urusi, China wanapenda kuonesha Silaha kuwatisha watu.
Mkuu si unajua hata huku mtaani, ukiona mtu anatamba yeye mtemi hababaishwi na mtu mara nyingi anakuwa anajihami hana lolote!
 
Mkuu si unajua hata huku mtaani, ukiona mtu anatamba yeye mtemi hababaishwi ma mtu mara nyingi anakuwa anajihami jana lolote!
Nimejifunza kitu kwa kweli. Sasa tumechanganyikiwa hatujui tumshike nani. Urusi ametunyong'onyesha,China suala la Taiwan tulitegemea ingewasha moto.... Leo hii Urusi ya kusaidiwa silaha na Irani kweli?ya kukodi wanajeshi wahuni na wafungwa?
 
Lengo la russia siyo kuiteka nchi,smo haziwezi kuwa kuteka nchi nzima
 
Mbona haujawaza wahuni wa Israel walivyomuua kiongozi wa HAMAS ndani ya ardhi ya Iran, udhani Iran ni wanyonge kwa Israel
 
Sawa bwana Putin πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ umeipata kijiwe gani mkuu
Kijiwe gani kivipi!?
Kwani vyombo vya habari havikutangaza kuhusu kuhusu Russia kuiteka Mariupol,Donbas,Kharkiv na Donetsk??
Kwani vyombo vya habari havikutangaza kuhusu silaha za NATO kukamatwa na Russia hapo Ukraine??
Kwani vyombo vya habari havikutangaza kuhusu raia kulazimishwa Ukraine kuingizwa jeshini ili kupunguza uhaba wa askari jeshi!!???
Au unataka nikuletee proof!??
Such a dunder
 
Kipanki ndo anamdanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…