Ukraine sasa iko katika vita kamili vya kujikomboa

Ukraine sasa iko katika vita kamili vya kujikomboa

Vita kati ya Russia na The US kamwe haiwezi kuwa na mbabe, hawa wakipigana hawawezi kutumia conventional weapons, watatumia ICBMs, Hypersonic nk, itakuwa ni "press button weapons war" sio infantry war na bila shaka Nuke weapons zitahusika, katika hali hiyo nani ataibuka mshindi??--- hakunaga mshindi katika matumuzi ya Nuke bombs.
Urusi ndo atakuwa wa kwanza kupeleka hizo Nukes na Hypersonic, USA yeye anaweza tumia boots maana wako hapo Germany wengi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukraine apigane kivyovyote vile Putin na nchi nyingine zinazodharau wenzao zijifunze.Putin pamoja na kuipiga Ukraine,nadhani hakutegemea kama atakutana na anayokutana nayo.Ukraine agharamike ila na Putin pia imgharimu sana.Ukraine atasaidiwa kujijenga,Putin atapambana na protest ndani na nje ya nchi na hatimaye anaweza akafa au kuuawa siku za mbeleni.
Putin kashangazwa na Ukrainians

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga ni kuamini kwamba hizo Hypersonic sijui Nuclear weapons anazo Russia pekee, NATO na Russia wakiingia vitamin hawachukui hata mwezi.. Russia haitabaki kitu. Russia hata kwa Germany hachomoki. Hapo tu Ukraine kapewa support ya vifaa sio ya Kijeshi na Russia kambwela.. akipata support ya kijeshi itakuwaje?

Kuwa na common sense kijana.
Poland anamtamani sana Urusi.
NATO na washirika walitamani sana kujua uwezo wa Urusi sasa washaujua, Urusi ana supply problem, kupitia Ukraine NATO wamepeleka ATGM nyingi ambazo zimeharibu zaidi ya 10pc ya vifaru vya Urusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matusi yote hayo ya nini??.

Russia na NATO & the US--- wanajuana kwa undani zaidi kuliko sisi tunavyowajua, Historia ya uhasama wao inaanzia tangu vita kuu ya pili, vita baridi, kuvunjika kwa Soviet na WARSAW, WARSAW ni counterpart ya NATO kabla ya kuvunjika kwa Soviet.

Mzozo huu chimbuko lake ni uhasama wa kihistoria uliokuwa unafukuta chini kwa chini na hatimaye kuibuka hivi karibuni.

Tuombe Mungu kwani harufu ya WW lll ndio inanukia kwani silaha zinazoingizwa Ukraine kutoka NATO na USA zitachochea vita kuwa kubwa na athari mbaya na hivyo kuanzisha WW lll, Putin hawezi kukubali kushindwa kirahisi atatumia Hypersonic zenye uwezo wa kubeba Nuke heads, hapo dunia itakuwa Finito.
Dunia haitaweza kwisha kamwe elewa hilo.
 
Hiyo hoja kuhusu "kuomba msaada" sidhani kama ina uzito wowote ukizingatia hata historia ya masuala ya vita duniani.

Wakati USSR inavamiwa na Hitler (Operation Barbarossa) kipindi cha Vita ya Pili ya Dunia, kina Stalin waliomba misaada kwa nchi zote washirika ili kumkabili Hitler.

Walipatiwa misaada ya namna mbalimbali ambayo ilikuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha kumuondoa Hitler.

Ni historia ambayo mpaka leo iko katika kumbukumbu za Urusi ya sasa, na inasherehekewa kila mwaka, kutokana na jinsi ambavyo mchango wa nchi washirika ulivyoweza kusaidia kupatikana kwa ushindi katika Vita ya Pili ya Dunia.
Hawa Warusi wa Kwa Mtongole wana shida, wao wana silaha nzito, Ukraine hana eti hawataki apewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wewe unajua Hypersonic ni kitu gani hadi imepewa hilo jina??--- usijifanye unajua kumbe hujui kitu.

Hypersonic ni kifaa au injini inayopaa angani na kukimbia mara 5 na Zaidi ya hapo kuliko mwendokasi wa sauti, ni Russia pekee ndiye mwenye Injini za uwezo huo duniani, ingine hizo zinauwezo wa kubeba silaha za Nyuklia na hakuna defensive shield yoyote kwa muda huu inayoweza kuizuia hiyo Hypersonic , hata defense za mrusi mwenyewe S-500 ambazo ni bora kuliko defensive zote haziwezi kuzuia Hypersonic, Mrusi kwa maana hiyo ana Upper hand dhidi ya nchi yoyote pindi ikitokea the "'press button war'.
Ivi kaka unajua unachoongea, kama ndege za kwenda hyper speed yani more than 5 mach( speed of sound zipo ila kombora lisiwepo)
Kila mtu anaweza kutengeneza hizo na ata marekani wanaweza, sema shida ni distance pamoja na accurace ya rong distance, ndo maana interms of nuclear warheads na ICBMs zake itabid trajectory iwe nje ya atmosphere ili kusiwe na friction na pia gravity iongeze msaada, engine zipo ila accuracy pamoja na exprossion power hupungua ikiwa kwenye huo mwendo( its physics)
 
Hii vita ni Russia vs west countries, battlefield ni ukraine,,, saa hizi ukraine wanapata support zote kuanzia intelligence, sattelite image za Russia military movements, etc,
Siku vita inaanza Russia walipanga kuuteka uwanja mkuu wa ndege wa Antonov ulio karibu na kiev, ili wakisha usecure , ndege za russia za mizigo zianze kushusha maelfu ya askari na magari ya delaya vifaru, etc tayari kwa kuuteka mji mkuu kiev,
Operation ilikua iishe ndani ya saa 24 kama walivyouteka crimea 2014,
Kilichotokea kumbe, wamarekani satelites zao zimenasa mpango wote, kwa maana ya movements za askari wa russia
Wakawapa information ukraine. Ikaandaliwa bonge ya Ambush ya hatari,
Warusi usiku wakaanza kuchupa kwa parachuti maeneo ya Antonov airport,, mamia ya paratroops,
Pale airport walikuwa wanajeshi wachache wa ukraine,, wakaweka challenge kidogo ya uongo na kweli kisha wakakimbia,,
Askari wa Russia wakajua tayari wameuteka uwanja wa antonov.
Kumbe bana jamaa wamewaotea,, basi askari wa Russia wakaanza kushuka kwa mamia. Kabla hawajakaa sawa wakaanza kushambuliwa kwa maroketi, katyusha,, mvua ya hatari ya rockets.
Hawajakaa sawa, wakazungukwa,, sasa ikaawa fighting for life,,
Russia kugundua wameingia mtego,, wakaitisha airstrike ili ziwasaidie,, zikaja helcopter karibu 50 kuwasaidia,
Shida ile vita, wamarekani wako wana monitor na kutoa direction ukraine wapige wapi,, adui yuko wapi, hivyo ukraine alenge wapi,
Zile helcopter zilionwa mapema kabla hata hazijakaribia,,, zikadunguliwa nyingi,,
Russia sasa wakapoteana, wamezungukwa na wako behind enemy line,,
Kwa ufupi, askari wengi wa Russia walikufa na kutekwa pia. Wachache sana waliokoka, karibu kikosi chite kilipotea,
Wakaupoteza uwanja,,,
Russia walikuja kuuteka tena siku tatu baadae baada ya mapigano makali sana,,
Japo majuzi waliuachia,, hivi sasa Russia kashausoma mchezo, anapambana na mataifa yote ya magharibi,
So kwa sasa anapiga kwa hesabu kubwa,, anaharibu maghala ya silaha na mafuta ya ukraine. ,kwa maana ni kuwa bila reserve za mafuta , ukraine military movements zitakuwa restricted,
Pia akiharibu maghara ya silaha na air defence system za ukraine hatimae ukraine atashindwa kupigana
Ingekuwa ni vita na West ungeona f22's au Abraham Tanks, au irone dome, au ungeona Patriot defensive missiles, au ata latest american guns, ila kama hizo hazionekani basi ni wanamsupport tu Ukraine, West sio wajinga waingie vita direct na Russia
 
Ivi kaka unajua unachoongea, kama ndege za kwenda hyper speed yani more than 5 mach( speed of sound zipo ila kombora lisiwepo)
Kila mtu anaweza kutengeneza hizo na ata marekani wanaweza, sema shida ni distance pamoja na accurace ya rong distance, ndo maana interms of nuclear warheads na ICBMs zake itabid trajectory iwe nje ya atmosphere ili kusiwe na friction na pia gravity iongeze msaada, engine zipo ila accuracy pamoja na exprossion power hupungua ikiwa kwenye huo mwendo( its physics)


Ndege inayobeba
Watu au fighter jets zenye rubani mmoja ni Supersonic yaani less than 5 mach na sio Hypersonic, Hypersonic ni jet engine inayobeba silaha ambazo nyingi ni guided, Hypersonic (silaha) za mrusi ni more than the 5 mach na zipo accurate vya kutosha kitu ambacho kinampa hofu America.

With Physics, lakini hayo yote ni ya kuzingatia.
 
Mambo mengi yako wazi sasa. Ukraine haombi tena no fly zone wala NATO kuingilia.

Ukraine anapewa silaha zote anazohitaji kumfurusha Mrusi. Ukraine kafika bei kuwa mzozo huu umalizikie ndani ya Ukraine.

Mrusi anakabiliwa na ukweli mpya ambao hakuutegemea.

Ndipo sasa kimbembe kilipo.
Hayo yote mliyajadili kwenye kikao kipi!?
Bonyokwa au Buza?

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom