Hii vita mrusi atanyoosha mikono juu na atapata fundisho next time asiwe na kimbelembele maana mrusi kama kuvumiliwa amevumiliwa sana na Ukraine think alichukua crimea akanyamaziwa then akaja kubeba na yale majimbo mawili tena akanyamaziwa kimya, now akaona kanogewa sasa akaingia mazima kuiteka Ukraine nzima iwe chini ya Russia hahaha , ndio maana hata mataifa ya mangaribi yamejiingiza kwenye hii vita kwa kumwaga silaha maana hata wao wameshtuka kwamba Russia akiiteka Ukraine hataishia hapo sababu kashanogewa atalivamia taifa lingine ulaya kama akinyamaziwa
Nyerere Mwenyewe aliwahi kusema endapo Idamin angenyamaziwa basi angemaliza kuiteka Tanzania kesho angefuata Kenya, ndio maana Idiamini akatembezewa kipigo chap , na anayoyafanya Putin ni yale yale ya Idamin kuiteka kagera, sasa kama Nyerere alicharuka kuingia vitani kutetea ardhi yetu iweje Zelensky akubali yaishe eti ajisalimishe kama sio wehu nyie?
Putin kwa sasa anapambana na Ulaya na marekani nzima maana washamchoka na Ulaya imeshtuka kuwa anaweza akavamia mataifa kila kukicha kama akinyamaziwa, kwa sasa Urusi atapigwa ambush kila kikicha hadi atarudi kwenye nchi yake
Maana ameingia kwenye Taifa ambalo raia wamegoma kuisaliti nchi yao na wamemwagiwa silaha na wanapigania ardhi yao yaani hata mamluki wa kuisaliti nchi hamna , Russia atakuwa anapigwa mashambulizi ya kushtukiza hadi akome na ataikimbia ukraine ni swala la muda tu, na hii vita ikiisha Putin atakuwa amepata fundisho kuwa sio kila sehem ni ya kuvamia hovyo hovyo
Na kunapoelekea kama hii vita haitoisha kwa Diplomasia au mrusi kuondosha majeshi yake Ukraine basi inaweza kuja kutokea Vita ya kutisha pale Ulaya sababu kila kukicha Ukraine anapitishiwa silaha nzito kutoka kwa majirani zake na baadhi ya majirani zake ni memba wa Nato
Sasa ipo Siku Russia atarusha kombora kwenye moja ya nchi iliyojiunga na NATO kwa kisingizio cha kuzuia kupishwa kwa silaha na hapo ndio itaibuka vita ya kutisha na tuombe sana isifikie huko ila kuna kila Dalili mrusi atakuja kushambulia nchi zinazompitishia silaha Ukraine na hapo ndio itaibuka vita kubwa ya kutisha
Hata Hitler kipindi anatabia ya kuvamia vamia nchi jirani hakuwahi kujua kuwa kuna siku atakuja kukutana na upinzani mkali , mwisho wake wengi mnaujua
Sent from my SM-A217F using
JamiiForums mobile app