Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Hivi havichambui fani za hadithi bali vimekusanya hadithi.

Tafuta vitabu vya kuanzia kama vile Mustwalahul Hadithi cha Sheikh Uthaymiin, tafuta Mandhumat al Bayquniyyah, Tafuta Risala al-Birkiwi hiivi kama msingi na viko viko, hizo miuswanafat na Sunan, hivyo hukhti fani kama fani ya Hadithi.

Umethibitsha mwenyewe ya kuwa huna dani ya hadithi. Fathu al-bari ya Ibn Hajar ni sherehe ya Sahihul al Bukhari.
 
Vitabu vyote ulivyotaja Ninavyo na sio kuwa navyo tu navisoma..

Umesema Nikuwekee Hadithi ambazo sio sahihi kwenye Sahihi Bukhari naomba nikupe Tano..

kwanza nikukumbushe Bwana Kisai..

Ili Hadithi iwe sahihi,Imam Al Shafi'i anasema kuhusiana na Hadith ambayo si Mutawattir kukubalika usahihi wake inabidi: ‘Mpokeaji wake awe ni mwenye kuaminika katika dini yake, awe anajulikana kua hasemi uongo katika kunukuu kwake, awe mwenye kufahamu anachokinukuu, awe mwenye kufahamu kwa kiasi gani mabadiliko ya maneno anayoyanuu yanaweza kubadilisha maana ya anachokinukuu, kimaana na kimaneno’.

Lakini kwa Hadithi kadhaa Ndani ya Bukhari Msimuliaji maarufu ni Abu Huraira ambaye Amesema Uongo mara kadhaa..

Uongo wa Kwanza Alisema kwamba alisali swala ya uoga na ilhali swala hiyo ilifanyika mahala panapoitwa Nakhl katika mwaka wa 5 wa utume ; Abu Huraira alikuwa hajasilimu kwa sababu alisilimu mwaka wa 7 wakati ilipotekwa ngome kuu ya Mayahudi Khaibar [kama Km 80 kaskazini mwa Madina]...

Hadithi inayothibitisha Uongo wake ni hadithi no 4137..


Sasa Tunaanza makosa machache sitataka ypte kwenye Bukhari maana ni mengi..

Sahihi Bukhari Juzzu ya 4 Hadithi no 3330..
Kuhusu Kuoza kwa Nyama..

Nyama Inaoza kwa sababu ya Waisrael


Abu Huraira alisimulia Hadithi na akainasibisha na Mtume kasema ila alipobanwa sana alisema ni mawazo yake mwenyewe na sio mtume...
So kama ukiona anatumia Neno mtume alisema..
Ila baadae walipombana akasema ni maneno yake mwenyewe..

Juzzu ya 7 Hadithi no 5355


Aya zilizokuwepo zamani kwenye Quran Kisha Zikaondolewa..
Sahihi Bukhari hadithi 4090, na Hadithi no 6830..

Mkuu ziko nyinhi sana Hizo ni chache
 
Mkuu hadithi nimeshasoma na najua na japo siwezi kujiita Mwanazuoni au Muhadithina na hapo nimekuonyesha Uchambuzi wa Hizo hadithi zilizokusanywa Na hata ukisoma Bulughul Maram..
Kwa wale wanaoanza kujifunza kuchambua Imechambua vizuri hadithi..

Na hata Hapa nipo nasoma Musnad Ya Iman Hanbal..
Karibu Mkuu..

 
Vitabu vyote ulivyotaja Ninavyo na sio kuwa navyo tu navisoma..

Sasa kama unavyo unashindwaje kuviweka hivyo ambavyo vinaelezea fani ya Hadithi, na wewe unatuwekea vilivyo kusanya Hadithi ?

Kuna Hadithi ambazo rawi wake ni Thika, yaani wakweli, waadilifu, sachamungu pia. Soma maana ya Hadithi Hassan.

Mpaka hapa wewe ndio hujui kuzichzmbua Hadithi. Maswahaba wote ni waadilifu na hawasemi uongo. Nani amekwambia hadithi inatiwa udhaifu kwa mtindo huu ? Nakuuliza swali kwani mtume ameswali sala ya Khofu mara ngapi ? Mpaka ukatae ya kuwa Abuu Huraira hajaswali swala ya Khofu ?

Hapa bado hujakosoa hii Hadithi.

Kingine katika Hadithi kuna fani inayo jishughulisha na Riwaya yaani matini ya Hadithi na Diraya inayo jishughulisha na Sanadi. Katika ukosoaji wa HADITHI, hapo ulitakiwa kwanza uanze kuichambua sanadi ya wapokezi, kisha uje uangalie je Mtume alisali mara ngapi sala ya Khofu ?
 

Bulughu al Maraam haichambui hadithi kama fani au kwa mtindo wa fani, bali imekusanya hadithi za hukmu za kisheria. Bado fani ya Hadithi hujaisoma bali huenda una vitabu vya Hadithi.

Kingine namna yako ya Uchambuzi wa hadithi haiko sawa, hap onapo kumezidi kuonyesha ni kwa namna gani huijui hiyo fani. Kuna hadithi nyingi ambazo maswahaba wamesingiziwa kadhalika. Kwahiyo ili sasa tuseme wewe umeichambua hadithi na kujua ni sahihi kabla ya kumuelekezea swahaba, lazima kwanza uangalie sanadi ya wapokezi husika. Ili tujue je ni kweli Abuu Huraira hayo maneno alimsikia Mtume ?

Kwahiyo ili uchambuzi wako uwe na mashiko kwanza, lazima uje kutelezea wapokezi wa hiyo hadithi mpaka kwa Abuu Huraira kisha mpaka kwa Mtume, kinyume chake ni makosa kumuita swahaba Muongo kwa mtindo huo.

Sasa nasubiri utuletee kwanza uchambuzi wa wapokezi na utupe sifa zao.

Namna hii huwa wanaitumia sana MASHIA kuwatusi maswahaba, huku elimu ya Rijali wa hadithi hawana.
 

Ngoja nikusaidie kitu kimoja, kwanza huu ulioweka sio uchambuzi wa kihadithi. Ili uchambuzi wako uwe sahihi, lazima kwanza uanze kuchambua wapokezi wa hiyo hadithi, hii sio habari za pauka pakawa, yaani from no where.

Sababu Imamu Bukhari ana sanadi rudi uje kuzichambua hizo sanadi na kama huwezi kufanya rudi katika vitabu vya Takhriji za Hadithi. Yaani tunataka kwanza tujue kweli masimulizi hayo ameyasimulia Swahaba Mtukufu Abuu Huraira ?
 
Shida yenu waislamu mnalazmisha mambo yenu na sisi tuyafuate.... Quran haina Amri 10 alizopewa Musa, amri 10 za Mungu ni nguzo za maadili katika ukristo... Usizini, usiibe, usiue, mpende baba yako na mama yako, na zote nyinginezo
Swali langu linataka uthibitisho ya kuwa alikuwa kweli ni mwanafunzi wa Yesu ? Katika wale wanafunzi 12 wa Yesu Matayo alikuwa ni miongoni mwao ?
Ndio, katika Injili nne za Biblia (Mathayo, Marko, Luka, na Yohana), Mathayo anatajwa kama mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu.
 
Vimeshushwaje bwana wakati vilikuwepo toka kitambo.... Yani yesu mwenye aliishita Torati, alafu miaka buku 7 baadae anakuja mtu na kusema alishushiwa torati na nyie mnaamini

Ni sawasawa atokee mtu leo hii asema ameshushiwa katiba ya Tanzania, alafu ukisoma hiyo katiba yake iwe inafanana na katiba iliyokuwepo mwanzo... Je kashushiwa kweli au kakopi
 
Dogo hawa watu unaowazungumzia humu kwenye Quran sio wanaozungumziwa kwenye Biblia... Historia za hawa watu ni tofauti... Ibrahim wa Quran na Abrahamu wa Biblia ni watu tofauti kimatukio
 
Wewe umesoma Biblia au Quran... Aliyesoma Biblia hawezi kubisha kuwa Mathayo, Luka, Yohana waliandika Injili... Sisi Biblia haikushushwa kama nyie na Quran, sisi biblia iliandikwa kwa mujibu wa historia na matukio yaliyotokea
 
Kiama ndiyo kitu gani?
 
Sikuona Faida ya Kuichambua kwa kina hadithi hiyo..

Ila kwa sanadi haina shida shida yangu ni matini zake hizo hadithi..

Huwezi kuIpa Hadithi usahihi kwa sanadi pake yake..
Ikiwa ina matini ya Uongo..

Nimekupa hadithi nyingi umeshikilia Moja kwa kuwa umeshikilia hiyo Moja sasa ngoja tuichambue matini zake..

Kwanza Umesema kuwa Mtume alifanya Sala ya hofu kwa vita vingi lakini kwa bahati mbaya ama nzuri hadithi kwenye matini yake imetaja hadi Vita iliyofanyika..Sijui kama unasoma kujibu au unasoma kilichoandikwa..


Narudia Tena swala hiyo ilifanyika mahala panapoitwa Nakhl katika mwaka wa 5 wa utume ; Abu Huraira alikuwa hajasilimu kwa sababu alisilimu mwaka wa 7 wakati ilipotekwa ngome kuu ya Mayahudi Khaibar [kama Km 80 kaskazini mwa Madina]. Bado unabisha???

Haya tuache hapo twende kwenye Kumzulia Mtume, abu huraira kamzushia Mtume kasema kitu ilihali mtume hakusema Unataka muislam aisifie hiyo hadithi..

Au aseme kile Mnachojifunga nacho kuwa maswahaba wote ni wema???

Mwanzoni kwenye hadithi hii alisema kuwa Mtume alisema baada ya watu kumbana sana akasema ni maneno yake!..

Bado unataka Huyo mtu Nimuamini je vipi kadanganya kama hicho kasema watu wakashtuka je vingapi ambavyo hawakushtuka??


Najua sunni mnafundishwa kuheshimu maswahaba nafahamu nilikuwa huko ila Usiwape hadhi ya Utume kama Shia wanavomfanya Ally..

Nataka Tuzungumzie matini ya Hadithi na sio Sanad kwa sababu naamini Bukhari ana sanad isiyo na shaka je hadithi zake (Kimatini "Kiriwaya")

Najua Kigezo unachotaka ni tuxungumzie kulingana na maumbile ya Matn na Isnad ya Hadith, kwamba hadithi ni Munkar au Mudraj..

Najua kwamba Hadithi nyingi za Sahih al bukhar Zina isnad nzuri kabisa na zenye mnyororo usiokatika mpaka kwa mtume..

Ila swali matini yake inaLeta maana na sio Mudraj..
 
Hakuna mahali nimesema nimechambua ila umeniomba Hadithi Ambazo haziko.sahihi na ziko.kwenye Usahihi...

Na nimekupa Ila bado mpaka sasa hivi hujaniprove wrong kuwa hadithi hizo ni sahihi au sio sahihi?
UMeomba hadithi nimekupa sasa hivi umeanza sasa kuleta blah blah za Bukhar hana sanad nani kasema buhari ana sanadi..

Bukhar ni Mujitahidi tu na hata Level ya Taqlid hajafika..kwa hiyo atabaki kuwa Imam wa Hadithi tu..
 
Inawezekana huyo aliyeumba kila kitu yupo kweli..... lakini sio huyu wa kwenye hekaya za Bibilia na Quran na scriptures za dini nyingine
We know nothing about “god”
Nadharia yako ya hakuna kinachojiumba chenyewe inatengeneza infinity..... nani kamuumba Mungu, na aliye muumba Mungu kaumbwa na nani?
 
Shida yenu waislamu mnalazmisha mambo yenu na sisi tuyafuate.... Quran haina Amri 10 alizopewa Musa, amri 10 za Mungu ni nguzo za maadili katika ukristo... Usizini, usiibe, usiue, mpende baba yako na mama yako, na zote nyinginezo

Ndio maana nikasema hivi UKRISTO ni dini ambayo Haina misingi, inatumia mafundisho ya mitume wengine kuendesha dini yao. Hili liweke akilini, Mtume Musa alitumwa kwa watu wa Israeli, kadhalika Yesu. Yesu ameondoka hakuacha Ukristo.

Qur'an inazo amri tena kwa ufafanuzi mzuri na hukumu zake.
Ndio, katika Injili nne za Biblia (Mathayo, Marko, Luka, na Yohana), Mathayo anatajwa kama mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu.

Sasa ndio uthibitishe ya kuwa kweli alikuwa ni katika wale wanafunzi 12 wa Yesu.
 

Tuwekee ushahidi wa kuwa Yesu aliishika Taurati. Toa mfano ambao ni hai, nani aje aseme ameshshiwa Taurati na Taurati ili shapita tayari ?

Maana ya kushushwa ni kwa maana mitume husika wanapewa au wanafunuliwa ujumbe toka Mbinguni.

Kufanana sio hoja, Qur'an haifanani na vitabu, ila ina habari kuhusu vitabu vya zamani katika hali ya kuthibitisha ukweli wa Qur'an na kujibu hoja za wapingaji.

Ndio maana katika sababu ambazo ziliwafanya watu wamkubali Mtume ni kuwaelezea habari za kale, na wakastaajabu na kumsadikisha.
 
Sasa huwezi kumsema swahaba kuwa ni muongo muda ambao hujaiweka wazi sanadi.

Uchambuzi huanzia katika Sanadi kwanza kisha unaingia katika matini kwa kurejea wanazuoni wa zamani wameizungumzia vipi hadithi husika.

Kwahiyo wewe utakuwa muongo na ni mzushi.
 

Sio lazima useme kwamba umechambua, ila ulichokofanya ni uchambuzi wa uongo ambao haujakaa kielimu.

Sio jukumu langu kukuonyesha ya kuwa ni sahihi au dhaifu, bali nakukosoa wewe kutumia njia ambayo sio sahihi kudai swahaba Abuu Huraira kuwa ni muongo.

Naam nimeomba hadithi, ambayo kwa misingi ya elimu ya Hadithi bado hujaonyesha udhaifu au kutokuwa sahihi kwa hadithi hiyo, zaidi ya kuonyesha huna elimu ya Hadithi.

Wapi nimeandika ya kuwa Bukhari Hana sanadi ? Nimesema anazo sanadi, huwezi kudhoofisha hadithi bila kuwaangalia rawi wa hadithi husika.

Lakini vile vile unaweza kudhoofisha hadithi ikienda kinyume na itikadi sahihi ya Uislamu au ikienda kinyume na Qur'an. Sababu maswahaba wote ni waadilifu, unaweza kuhitimisha ya kuwa swahaba Abuu Huraira hawezi kusema maneno kinyume na mafundisho ya Mtume au kinyume na Qur'an.

Unajua maana ya Taqlid jifunze kutumia haya maneno vizuri.
 
MKuu unazunguka ila Sijaona Kuhusu Jibu kuhusu Hadithi nilizokupa...maana Ziko wazi kabisa..
zijibu kwanza Hadithi hizo..

Maana nimeshakujibu Sanadi zao Hazina shaka ila matini ndo yana mashaka sasa hebu zijibu hizo matini acha Kuzunguka..

Je, Abu hurairah aliposema Mtume amesema na baadae watu walipomzonga kumuuliza Akiri mtu kasema na akabadilisha na kussma kassma yeye sio mtume hakudanganya?

Je, Abu hurarah aliposema aliswali swala ya Hofu na mtume mwaka wa 5 wa utume wakati Abu Huraira alikuwa hajasilimu kwa sababu alisilimu mwaka wa 7 wakati ilipotekwa ngome kuu ya Mayahudi Khaibar hakusema Uongo???

Au unaogopa Kusema Abu huraira Alisema uongo kwa sababu ndo anaongoza kwa isnad za Hadithi nyingi zaidi?
 
Kwanza siwezi kuzungumza maneno nisiyoyajua maana yake..

Pili Hadithi zote zinazosema Quran Imepunguzwa Aya Unaona ni sawa?

Hadithi zinazosema Quran Kulikuwa na Aya zingine ambazo Zilikuwepo na sasa hazipo zipo sawa?

Twende Kwenye Matini ya Hadithi hizo acha mbwembwe..

Nimekuambia katika Sanadi sheria Inafunga kusema kuwa Abu huraira Hadithi yake sio sahihi ila kwa matini yanatia shaka

ila Kuhusiana na utaalamu wa Hadith basi Imam Abu Ahmad Al Hasan bn Abd Rahman Ibn Khalal Al Farsy Al Ramhurmuzi ambae ni mtaalamu mkubwa wa mfumo wa makundi ya I’lm ya Hadith anasema kua ‘Abd Ar Rahman Ibn Al Mahdi amesema kua:

Wanahadith wako aina tatu: Aina ya kwanza ni wale ambao wenye kumbukumbu nzuri na wenye uangalifu, hawa hua hamna kutokukubaliana juu yao, wa pili ni wale ambao wanafanya makosa lakini Hadith zao ni Sahih na za uhakika, hawa hua haziachwi Hadith zao, na wa tatu ni wale ambao wanafanya makosa mengi sana katika Hadith zao na hawa Hadith zao hukataliwa (matrook).’

na Unataka Kujua maana ya Taqlid 😅😅..


MAANA YA TAQLID maana yake ni kufuata ushauri wa kisharia kutoka kwa mtu (ambae ushauri wake si uthibitisho katika Sharia’h ya kiislam) bila kutaka uthibitisho kutoka kwa mtu umfuatae. (Maana hiyo imetolewa kwenye Al-Mustasfa min usul al-Fiqh, Imam Al Ghazal)

Hii ina maana kua mtu afanyae Taqlid ambae kwa kilugha huitwa Muqallid hachukui ushauri wa yule aliefanya Ijtihad kua ni chanzo cha Sharia’h za Kiislam, kwani chanzo cha Sharia’h za kiislam ni Qur’an na Sunnah.

Sababu inayomfanya Muqallid kumfuata Mujtahid ni kuamini kua Mujtahid ana elimu na uwezo wa kuchambua Qur’an na Hadith ambao yeye Muqalid hua hana. Taqlid hufanywa katika mambo ya Fiqh.

Na Usisahau Fiqh imetokana Na Sunna na Quran Na Hadithi huwezi kuiacha


Bado narudia Tena Jibu maswali acha kukwepa Maswali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…