Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Katika historia ya awali, Biblia ilianzishwa katika lugha za asili kama Kiebrania (kwa Agano la Kale) na Kigiriki (kwa Agano Jipya).
Bila shaka hapo.kuna mchanganyiko.inakuwaje kitabu kimoja kiandikwe kwa lugha 2 tofauti?
 
Mleta mada biblia alipewa nabii gani?
Biblia inajumuisha maandiko yaliyoandikwa na waandishi mbalimbali katika kipindi tofauti cha historia ya dini ya Kiyahudi na Kikristo. Haijaandikwa moja kwa moja na nabii mmoja maalum. Badala yake, inajumuisha maandiko yaliyoandikwa na manabii, wataalamu wa dini, wanahistoria, na waandishi wengine, ambao waliandika kwa kuzingatia ufunuo, uzoefu wa kidini, na matukio ya kihistoria. Kwa mfano, katika Agano la Kale, vitabu vingi vinavyohusishwa na nabii kama vile Isaya, Yeremia, na Ezekieli, wanasemekana kuwa na sehemu ya maandiko yaliyojumuishwa katika Biblia. Katika Agano Jipya, vitabu vya Injili vilivyoandikwa na wanafunzi wa Yesu pamoja na barua za mitume ni sehemu ya maandiko yaliyojumuishwa katika Biblia.
 
Kama Adam alikuwa binadamu wa kwanza. Unabii alikuwa anaufanya kwankina nani?
Kwani lengo la kuleta nabii si kuilea jamii kwa kuipatia muongozo utokao kwa Mungu?

Adam alikuwa ni baba na kiongozi kwa familia yake na ndiye mtu wa kwanza. Unafikiri mwongozo wake juu ya malezi na kuiongoza familia yake na kuyatawala mazingira ulikuwa unatoka wapi? Ulikuwa unatoka kwa Mungu.

Na namna ya kuiongozo familia yake kiroho mwingozo alikuwa anaupata kutoka kwa nani? Jawabu ni kwa Mungu.

Hivyo akafanywa kuwa Nabii kwa familia yake. Ni kama manabii wengine walivyotumwa kwa watu wa jamii yao/eneo lao tu. Halikadhalika na yeye. Akifanywa kuwa nabii kwa ajili ya kuiongoza familia kwenye mazingira ambayo wao ndiyo viumbe wa kwanza wa aina yao kuishi. Yaani binadamu.
 
Biblia inajumuisha maandiko yaliyoandikwa na waandishi mbalimbali katika kipindi tofauti cha historia ya dini ya Kiyahudi na Kikristo. Haijaandikwa moja kwa moja na nabii mmoja maalum. Badala yake, inajumuisha maandiko yaliyoandikwa na manabii, wataalamu wa dini, wanahistoria, na waandishi wengine, ambao waliandika kwa kuzingatia ufunuo, uzoefu wa kidini, na matukio ya kihistoria. Kwa mfano, katika Agano la Kale, vitabu vingi vinavyohusishwa na nabii kama vile Isaya, Yeremia, na Ezekieli, wanasemekana kuwa na sehemu ya maandiko yaliyojumuishwa katika Biblia. Katika Agano Jipya, vitabu vya Injili vilivyoandikwa na wanafunzi wa Yesu pamoja na barua za mitume ni sehemu ya maandiko yaliyojumuishwa katika Biblia.
Una uhakika gani kuwa hao waliondika biblia walichokiandika ni sahihi?
 
Back
Top Bottom