Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Quran imeandikwa kiarabu biblia iliandikwa kwa lugha gani?
Mi nimezungumzia stori zilizo kwenye hivo vitabu sio lugha. Kwani we hapo huwezi kukopi kitabu cha kitaliano na kuandika kwa kiswahili Kisha ukakiEdit kwa namna unayoitaka mwenyewe?
 
Kama Adam alikuwa binadamu wa kwanza. Unabii alikuwa anaufanya kwankina nani?
Katika imani za dini ya Kiyahudi na Ukristo, Adam na Hawa, mke wake, walikuwa wazazi wa kwanza wa wanadamu wote.

Katika imani za dini ya Kiyahudi na Ukristo, Adam na Hawa, mke wake, walikuwa wazazi wa kwanza wa wanadamu wote. Adam anajulikana kama binadamu wa kwanza aliyeumbwa na Mungu. Hakuna rekodi ya moja kwa moja kuhusu unabii alioufanya. Hata hivyo, katika baadhi ya mafundisho ya kidini, Adam anajulikana kama mtu wa kwanza ambaye alipewa ujuzi na uelewa wa kuweza kumtambua Mungu na kufanya mapenzi yake.

Katika Uislamu, Adam anatambulika kama nabii na kama mtu wa kwanza aliyeumbwa na Mungu. Anaonekana kama kiongozi na mwanzilishi wa binadamu wote na inasemekana kwamba waliishi katika bustani ya Peponi kabla ya kutolewa kwao kuja duniani. Ingawa Qurani haielezi unabii maalum alioufanya Adam, inamzungumzia kama mtu aliyeletwa duniani na Mungu na aliyepewa heshima na uwezo wa kumwabudu Mungu. Hadithi za Mtume Muhammad pia zinamzungumzia Adam kama nabii na kiongozi wa kwanza wa binadamu.
 
Mi nimezungumzia stori zilizo kwenye hivo vitabu sio lugha. Kwani we hapo huwezi kukopi kitabu cha kitaliano na kuandika kwa kiswahili Kisha ukakiEdit kwa namna unayoitaka mwenyewe?
Yeremia 8-8.
Waandishi wameifsnya nini taurati?
 
Attachments

  • Screenshot_20240407_171528_Biblia Takatifu.jpg
    Screenshot_20240407_171528_Biblia Takatifu.jpg
    504 KB · Views: 12
Waislamu wana vitabu vyao! Unaweza kutusaidia ushahidi kutoka kwenye vitabu vyao ili tusiwe tukaonekana tunawasingizia kwa hili?
Defensive machinsm at work.
Ngoja nikufuate huku huko unakotaka kujificha, nifyeke hicho kichaka chako cha Karanga unachotaka kukitumia.

Kati ya manabii laki 2 na 24 wanaotambulika na uislamu na vitabu vya kiislamu kama ulivyo sema, nitajie manabii wawili ama watatu wanaosema Mungu hana Mwana then huu mjadala utakuwa umeisha.

upande wangu mimi naweza kukupa verse za akina:-
KING DAVID.
SULEIMAN.
MUSA.
ISAYA.
JEREMIA ETC WANAKUBALI KUWA MUNGU ANA MWANA NA UNAWEZA SEMA VITABU VYAO HAVITAMBULIKI KATIKA ISLAM.
SO TUJADILI KUPITIA VITABU VYA KIISLAM TU.
 
Hivi ww jamaa ukikaa bila kujadili mambo ya dini utakufa ?
Ww ni mtu hatari kwa jamii yako iliyo kuzunguka.
 
Bila shaka hapo.kuna mchanganyiko.inakuwaje kitabu kimoja kiandikwe kwa lugha 2 tofauti?
Mchanganyiko wa lugha katika Biblia unatokana na historia na muktadha wa utamaduni na lugha za kipindi cha uandishi wake. Biblia ilikusanya maandiko mengi kutoka kwa waandishi tofauti kwa kipindi kirefu cha muda na katika maeneo mbalimbali. Kwa mfano, Agano la Kale lililoandikwa kwa Kiebrania na Agano Jipya lililoandikwa kwa Kigiriki.

Agano la Kale liliandikwa kwa Kiebrania (pamoja na sehemu za Aramaic), na baadaye, tafsiri zilifanyika katika lugha tofauti kama vile Kigiriki (Septuagint) na Kilatini (Vulgata) ili kufikia wasomaji wa lugha hizo.

Agano Jipya la Biblia liliandikwa hasa katika Kigiriki kwa sababu Kigiriki ilikuwa lugha rasmi, au lugha ya kawaida ya eneo la Mashariki ya Mediterania wakati wa Yesu na kanisa la kwanza la Kikristo. Kigiriki kilizungumzwa na kueleweka kotekote katika Milki ya Roma, ukijumuisha maeneo ambayo wanafunzi na wafuasi wa Yesu walieneza mafundisho yake.

Wayahudi wengi katika enzi hiyo walikuwa na lugha mbili, wakielewa Kiebrania na Kigiriki. Hata hivyo, lugha ya kila siku ya mawasiliano na biashara katika maeneo kama Yudea, Galilaya, na maeneo mengine ambako Yesu alihubiri mara nyingi ilikuwa ya Kigiriki, kwa sababu ya uvutano wa utamaduni wa Kigiriki na ushindi wa vita ya The Great Alexander.

Kwa sababu hiyo, wakati waandishi wa Agano Jipya walipoandika mafundisho ya Yesu na jumuiya ya Wakristo wa mapema, walifanya hivyo katika lugha ambayo ingewafikia watu wengi zaidi na kupatikana zaidi kwa watu wa wakati huo - Kigiriki. Zaidi ya hayo, iliruhusu mafundisho ya Yesu kuenea kwa urahisi zaidi kwa watu wasio Wayahudi, na hivyo kuchangia kuenea kwa haraka kwa Ukristo katika karne zilizofuata.
 
Hivi ww jamaa ukikaa bila kujadili mambo ya dini utakufa ?
Ww ni mtu hatari kwa jamii yako iliyo kuzunguka.
Dini ni sehemu za maisha yetu ya kila siku
 
Biblia inajumuisha maandiko yaliyoandikwa na waandishi mbalimbali katika kipindi tofauti cha historia ya dini ya Kiyahudi na Kikristo. Haijaandikwa moja kwa moja na nabii mmoja maalum. Badala yake, inajumuisha maandiko yaliyoandikwa na manabii, wataalamu wa dini, wanahistoria, na waandishi wengine, ambao waliandika kwa kuzingatia ufunuo, uzoefu wa kidini, na matukio ya kihistoria. Kwa mfano, katika Agano la Kale, vitabu vingi vinavyohusishwa na nabii kama vile Isaya, Yeremia, na Ezekieli, wanasemekana kuwa na sehemu ya maandiko yaliyojumuishwa katika Biblia. Katika Agano Jipya, vitabu vya Injili vilivyoandikwa na wanafunzi wa Yesu pamoja na barua za mitume ni sehemu ya maandiko yaliyojumuishwa katika Biblia.
Kwa maelezo haya ni wazi kabisa Biblia siyo kitabu kitakatifu.

Sababu maelezo yake au maneno yake hayafiki moja kwa moja kwa mitume husika, mfano Yesu na Musa.
 
Mchanganyiko wa lugha katika Biblia unatokana na historia na muktadha wa utamaduni na lugha za kipindi cha uandishi wake. Biblia ilikusanya maandiko mengi kutoka kwa waandishi tofauti kwa kipindi kirefu cha muda na katika maeneo mbalimbali. Kwa mfano, Agano la Kale lililoandikwa kwa Kiebrania na Agano Jipya lililoandikwa kwa Kigiriki.

Agano la Kale liliandikwa kwa Kiebrania (pamoja na sehemu za Aramaic), na baadaye, tafsiri zilifanyika katika lugha tofauti kama vile Kigiriki (Septuagint) na Kilatini (Vulgata) ili kufikia wasomaji wa lugha hizo.

Agano Jipya la Biblia liliandikwa hasa katika Kigiriki kwa sababu Kigiriki ilikuwa lugha rasmi, au lugha ya kawaida ya eneo la Mashariki ya Mediterania wakati wa Yesu na kanisa la kwanza la Kikristo. Kigiriki kilizungumzwa na kueleweka kotekote katika Milki ya Roma, ukijumuisha maeneo ambayo wanafunzi na wafuasi wa Yesu walieneza mafundisho yake.

Wayahudi wengi katika enzi hiyo walikuwa na lugha mbili, wakielewa Kiebrania na Kigiriki. Hata hivyo, lugha ya kila siku ya mawasiliano na biashara katika maeneo kama Yudea, Galilaya, na maeneo mengine ambako Yesu alihubiri mara nyingi ilikuwa ya Kigiriki, kwa sababu ya uvutano wa utamaduni wa Kigiriki na ushindi wa vita ya The Great Alexander.

Kwa sababu hiyo, wakati waandishi wa Agano Jipya walipoandika mafundisho ya Yesu na jumuiya ya Wakristo wa mapema, walifanya hivyo katika lugha ambayo ingewafikia watu wengi zaidi na kupatikana zaidi kwa watu wa wakati huo - Kigiriki. Zaidi ya hayo, iliruhusu mafundisho ya Yesu kuenea kwa urahisi zaidi kwa watu wasio Wayahudi, na hivyo kuchangia kuenea kwa haraka kwa Ukristo katika karne zilizofuata.
Yeremia 8-8.waandishi wameifanya nini taurati?
 
Attachments

  • Screenshot_20240407_171528_Biblia Takatifu.jpg
    Screenshot_20240407_171528_Biblia Takatifu.jpg
    504 KB · Views: 13
Qur'an Ina matatizo zaidi ya kiuandishi, iliandikwa au kukusanywa miaka zaidi ya 100 baada ya Mtume kufariki, wakati Biblia ilikuwa imekamilika au baadhi ya vitabu vyake viliandikwa miaka 30-40 baada ya Yesu kupaa. N walioandika waliishi naye; walimjua na kimfahamu Yesu.
Ndiyo maana Qur'an Waislamu and wengine hawaijui , kazi yao ni kufunga na kuswali na kusikiliza mawaidha tu. Hata waliotafsiri mengine wamepotosha baadhi ya maandiko. Mtu mwenybhekima atasoma na kuchambua. Mwislamunhna uhakika kam akifa atakwenda mbinguni, sababu hata Mtume mwenyewe hajui. Angalia Yesu alizungumza kwa ujasiri sana. " Nilipo Mimi nanyi mtakiwepo"
 
Una uhakika gani kuwa hao waliondika biblia walichokiandika ni sahihi?
Biblia inachukuliwa kama Neno la Mungu la kweli na kuaminika, na imani ya kikristo inaamini kwamba maandishi yaliyo katika Biblia yalikuwa chini ya uongozi na uwezo wa Roho Mtakatifu wakati wa uandishi wake. Kupitia manabii mbalimbali na wanafunzi wa yesu na wafuasi wake waliongozwa kuandika habari za Mungu. Na habari za yote yaliyotendeka zilikuwa wazi kwa sababu zilishuhudiwa na watu wengi. Mfano Injili ya Yesu imeandikwa katika Agano Jipya kwenye kitabu cha Mathayo, Luka, Yohana na wote maandiko yao yanafanana na wote walikuwa wanafunzi wa Yesu

Ni kama wewe unavyoamini kwamba Mohamad alishushiwa Koran, na wakati hakuna shahidi juu ya hilo aliyekuwepo akiona Mohamad akipokea Quran
 
Back
Top Bottom