GYNEOCOLOGIST
Senior Member
- Sep 13, 2016
- 171
- 110
Muundo wa Lugha nyingi duniani hutegemea lugha nyingine. Lugha ya kiswahili kwa kiasi kikubwa imetokana na maneno ya kiarabu mfanoJamani. Naomba kuuliza, neno MUBASHARA linalotumiwa na kituo cha luninga cha ITV ni la Kiswahili sanifu?[/
Ndiyo, ni neno la kiswahili toka ktk lugha ya kiarabu.Jamani. Naomba kuuliza, neno MUBASHARA linalotumiwa na kituo cha luninga cha ITV ni la Kiswahili sanifu?
Hili neno nimeliona mara ya kwanza ITVJamani. Naomba kuuliza, neno MUBASHARA linalotumiwa na kituo cha luninga cha ITV ni la Kiswahili sanifu?
Nashukuru kwa kunielemisha. Lakini tukubali ukweli mmoja kuwa maneno ya lugha nyingine huingia na juanza kutumika kwenye lugha nyingine kurokana na mazoea. Sio kwa kulazisha neno la lugha nyingine ambalo halitumiki popote na kulifanya neno rasmi.
Kutokana na ujio wa luninga, na kuanzishwa kwa matangazo ya moja kwa moja kwenye luninga na kwa sisi uelekeo wetu na mazoea ni kiingereza na neno la kiingereza linalotumika na tunaloliona ni LIVE, na kwa kuwa neno hili lina tafsiri rasmi ya kiswahili, HAI. Basi ingekuwa rahisi tu kugeuza neno LIVE na kuwa HAI. Kwa mfano ni rahisi kusema "tunawaletea matangazo hai ya mpira kutoka uwanja wa Kirumba..." kuliko kusema ".....matangazo mubashara..."
Kunyumbulisha tafsiri kutoka maneno ya lugha nyingine ambayo hayakuzoeleka kwa kiswahili ni kukifanya kiswahili kuwa kigumu zaidi.
Kutokana na hili ndio maana sio vituo vingi vinatumia neno hili.
Sijakataa kukopa lakini kopa neno ambalo ni rahisi kutumika au lililokuwepo. Halafu utaratibu wa kukopa kutoka lugha nyingine huwa hauji kwa kulazimishia. Kulingana na historia yetu, maneno mengi ya kwanza yalikopwa kutoka lugha ya kiarabu kwa kuwa ndio lugha iliyokuwa inatumika, lakini baadaye utaona wareno walipokuja tukakopa, wajerumani tukakopa na waingereza na kiingereza chao tumeendelea kukopa. Hapa suala lilikuwa la kungalia neno gani ambalo limezoeleka kwenye jamii kuliko kuanzisha neno jipya kisa limekopwa. Bado nafikiri kuwa neno hai lingekuwa bora zaidi kuliko mubasharaMkuu maelezo yako ni Kama hukubali ukweli kuwa lugha ya
Kiswahili imekopa maneno toka lugha ya kiarabu. Yafutayo ni maneno yaliyotokana na lugha ya kiarabu:
-Habari-habar; asubuhi-subhi; alasiri-l asri n.k
Nimekupata vilivyo Mkuu, all in all ndivyo lugha zinavyokuwa.........SHATI-SHIRT; RULA-RULER; MENEJIMENTI-MANAGEMENT....hahahaSijakataa kukopa lakini kopa neno ambalo ni rahisi kutumika au lililokuwepo. Halafu utaratibu wa kukopa kutoka lugha nyingine huwa hauji kwa kulazimishia. Kulingana na historia yetu, maneno mengi ya kwanza yalikopwa kutoka lugha ya kiarabu kwa kuwa ndio lugha iliyokuwa inatumika, lakini baadaye utaona wareno walipokuja tukakopa, wajerumani tukakopa na waingereza na kiingereza chao tumeendelea kukopa. Hapa suala lilikuwa la kungalia neno gani ambalo limezoeleka kwenye jamii kuliko kuanzisha neno jipya kisa limekopwa. Bado nafikiri kuwa neno hai lingekuwa bora zaidi kuliko mubashara
Safi sanaYaah!Mbona mi nimeanza mpaka kulitumia katka maongezi yangu ya kila siku!!!