Ukuu wa Dollar ya Marekani umefika mwisho?

Kama huwezi changia bora ukae kimya usome maoni ya wenzako.
 
Kama unaangalia mambo namna hii, tena kwa kupingana na sababu za kitaalam kabisa, basi una haki ya kuja na conclusion kama uliyoainisha kwenye thread yako.
Mkuu wewe ndiyo huangalii mambo kitaalamu. Mfano, unafikiri nchi nyingi kuwa na reserve ya dollar ndiko kunafanya dollar iwe sarafu ya dunia, au hayo ni matokeo ya dollar kuwa sarafu ya dunia?
 
Ku freeze pesa za Urusi kuna watisha sana mataifa mengine kwenye hifadhi hata kwenye uwekezaji.

Pia vikwazo vya mifumo ya kimataifa ya kifedha vinafanya mataifa mengine kuona namna ya kuanzisha mifumo yao mbadala.
 
Namba 3 na 4 kuna mtikisiko mkubwa hapa sikubaliani na wewe kwa sasa.

Namba 1 na 2 kuna uimara
Unadhani hawana utulivu wa kisiasa? Pengine neno utulivu wa kisiasa ni topic kubwa sana inayohitaji shule. NB: haya mambo ni kama nguzo nyingi zinazoshikilia jumba kubwa kwa juu. Nguzo moja au mbili na hata tatu kuwa weakened hakuwezi kuangusha jumba zima bali kunatoa fursa kwa mwenye nyumba kuimarisha zile nguzo.
 
Mkuu wewe ndiyo huangalii mambo kitaalamu. Mfano, unafikiri nchi nyingi kuwa na reserve ya dollar ndiko kunafanya dollar iwe sarafu ya dunia, au hayo ni matokeo ya dollar kuwa sarafu ya dunia?
Tafadhali nisome vizuri. Nimesema kuna factors nyingi na hiyo ni mojawapo tu. Hata hizo nilizoorodhesha ni chache sana. Nchi yoyote duniani success huja kwa sababu ya factors nyingi na siyo moja wala mbili wala tatu. Mkuu mbona unakuwa kama CCM wanaopiga porojo kuwa kila rais anayeingia ndiye mwenye ufunguo wa kuleta maendeleo ya nchi? Wamefikia hatua ya kusema baada ya mtume Muhamad na Yesu kushushwa, Samia ndiye anafuatia!
 
Mkuu chna n kama kitu anaweza n kuuza bizaa zake Africa ndy soko lake kubwa pamoja naizo kweny strong ya pesa top ten mchna pesa yake ya yuan aipo kama pesa enye nguvu dunian
Ndio maana nikikuambia jielimishe. Nini sasa hiki umeandika?!.
 
Si rahisi wala si kitu cha mwaka mmoja or ten years to come. in order uue US dollar kill itegemezi wa dollar europe, sub sahara, south america. And north america.
Otherwise dollar bado ipo sana
 
Ni kweli factors zipo nyingi mkuu. Ndiyo maana hata kwenye post yangu nilisema moja ya sababu ni dollar kutumika kununulia mafuta. Pia nimekubaliana na sababu yako ya utulivu wa kisiasa. Ila fahamu kuwa sababu ya kutumika kununua mafuta ni kubwa zaidi. Ndiyo maana dollar inaitwa petrodollar.

Baada ya US kuona kuwa si mzalishaji namba moja tena. Nakuona kuwa kwa kutokuwa mzalishaji namba moja mahitaji ya dollar yake yatapungua akaamua kufanya deal na Saudi Arabia ambaye alikuwa ndiyo mzalishaji mkubwa wa mafuta wakati huo. Deal ni kuwa SA auze mafuta kwa dollar tu. Kwa sababu mafuta ndiyo bidhaa inayonunuliwa sana basi kila nchi italazimika kuitafuta USD ili inunue mafuta. Wakati huo huo alihakikisha kuwa nchi zote zenye mafuta anazidhibiti, labda kwa makampuni yake kuwa ndiyo wachimbaji au kwa kichapo.

Sasa dili lao na Saudis limefika mwisho na Crown Prince anataka kuleta za kuleta. Huku BRICS wanaleta yao, mara nchi zinaingia bilateral agreements za kutumia pesa zao. Ndiyo maana naona kama anguko la dollar lipo karibu.
 
Na Marekani akitaka mafuta ya SA anunue Kwa Dirhamu. Huo ndio uadilifu
Uko sahihi, 1. Lakini yeye ana mafuta ya kutosha miaka elfu, ukimwekea sharti hilo anakataa maana dhiram ya SA ataifanyia nini, kununua mafuta tu toka SA?
 
US mkidhindwana mwezani anakutafutia zengwe km alivyofanya kwa waarabu wengine km Yemen,Syria,Iran,Iraq moja wapo nikusema unafadhili magaidi and Una siraha za nuklia,hii imewatesa sana waarabu as long as unapingana nae atakuletea zengwe tu hata km itachukua 20yrs lkn utaingia 18 zake tu
 
Sioni facts za maana kwemye hii bandiko lako
 
Industrial products hazipatikani U.S.A pekee kwanza U.S.A sio industrial powerhouse kwa sasa duniani hiyo nafasi imechukuliwa na China miaka mingi iliyopita labda ulete sababu tofauti na hii.
Us.a akiwa industrial power si tutauziwa tooth pick kwa shilingi 10000 kwao ikiwa kama 3.5 usd .ashukuriwe mchina kwa sis dunia ya tatu
 
SA aache ujinga auze bidhaa ya mafuta Kwa sarafu yake
Haya mambo ya uchumi ni tofauti kabisa na mafundisho ya madrassat, kwa mfano Tanzania inataka kununua mafuta Saudi Arabia watapataje Rial ya kununulia hayo mafuta.

Mambo mengine acheni ushabiki wa kipumbavu bwana na ushabiki wa kidini ambao kwa kawaida waga hauna mantiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…