Sifahamu uelewa wako kuhusu uchumi wa dunia, inaonekana unataka kubishana, nimesema hapo juu, dola itaanguka kwani hakuna kitu kisichokuwa na mwisho hapa duniani.
Ila kwa sasa na kwa baadaye ni ngumu kutokea huu ni ukweli mchungu, huwezi kusema dunia itaachana na dola hata kwa miaka 50 ijayo, au wewe kwa kutumia akili yako unaliona hilo??
Walijaribu Mjapani, Mwingereza, Mchina na EU walikutana na ugumu coz ya uchumi wa kushikamanishwa na dola.
Kasome kwa nini world reserve currency iwe dola na siyo sarafu nyingine pamoja na manyanyaso yote dunia inayoyapata.
Ukweli mchungu: Dunia inahiitaji sana dola kwa sasa kuliko dola inavyohiitaji dunia!
Nb: Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, itakuja kuanguka ni suala la wakati na tunahitaji kuvumilia!