Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 8,013
- 14,263
mbegu za kisasa zinapatikana wapi mkuuSio hizo za kienyeji mkuu,zinazonunuliwa na mabeberu ni za kisasa.
nipate japo miche mitatu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mbegu za kisasa zinapatikana wapi mkuuSio hizo za kienyeji mkuu,zinazonunuliwa na mabeberu ni za kisasa.
For Export?tarime parachichi zinajiotea tu, mti mmojammoja kwa kila kaya na ni mengi mno
tunakula wenyewe na mbwa na ng'ombe pia wanajillia
akija mchuuzi unamuuzia ndoo nzima elf 3
Ni hakilipi kwa Tanzania pekee au Dunia nzima? Shida iko hapo, Ukifuatilia Wakenya wanakimbizana na Parachichi balaa.Nimefanya kilimo cha parachichi kwa miaka nane sasa, nilichokiona ni haya;
1. Kilimo kina mzunguko wake ni mdogo parachichi huzaa kidogo kidogo kadri miaka inavyoenda, unatumia million 10 unapata million mbili.
2. Bei hazijadiliki anayeamua ni mnunuzi unless uwe na mtaji mkubwa ambayo unakuruhusu ku export mwenyewe, na uwe na uwezo wa kuwa na cold room Ili zikikomaa uchume uzihifadhi kama bei hueilewi kwa kipindi hicho (hii mitaji watanzania wengi hatuna). 3. Management ya parachichi ni ngumu sana linahitaji maji kidogo (hapa unaweza manage kumwagilia) linahitaji mbolea za chumvi na mbolea za majani, sumu. Kila nk kwa kiasi kidogo, linahitaji muda Kwa wingi, upatikanaji wa Samadi ni mtihani sana (wengi wamejikuta parachichi zimedumaa na wengine wanazalisha reject kwa wingi) kisa tu wameshindwa kuwa na Samadi, udhibiti wa nyasi (ukweli ni kuwa Ili miti iwe Bora unahitaji kulima badala ya kufyeka nyasi)
Nimefanya observation shambani kwangu panapolimwa pana matokeo kuliko panapofyekwa, distance kati ya mti na mti inamua sana miti iliyokaribu inasumbua sana na mingi huwa haizai vizuri. Hizi issue zimefanya watu tukimbie mashamba yetu, hata kiwango cha pesa kinachotajwa wengi hawapati ni figure za uwongo Ili kujifariji, njoo na hoja zako kupinga zangu hapo juu, zangu ni hizo.
Nashauri kama una pesa zako kidogo lima mazao ya chakula tu viazi, mpunga, mahindi nk hivi vinalipa. Huku pesa ipo na kama location ulipo ni nzuri lima mazao yanayohifadhika like kahawa, miaka miwili inazaa, management yake rahisi. Nalima kahawa makete pia ni mwaka wa tatu tayari nimeanza kuvuna.
NB: Mazao ya chakula ndio kila kitu hizi nyingine tabu umezitafuta.
Inategemeana na mahali ulipo mkuu, ukiona wataalamu wa kilimo hicho utaabiwa utumie mbegu gani.mbegu za kisasa zinapatikana wapi mkuu
nipate japo miche mitatu
Ila si ameshashitakiwa?? Dah kawaumiza watu sana JATUHakuna tofauti Kati ya kulima parachichi na kujiunga na JATU PLC
Binafsi huwa sina imani sana na mazao yanayotegemea mnunuzi mmoja tena wa nnje ya nchi,mazao ya chakula soko lake liko huru sana, ni nguvuzako tu mwenyewe.Nimefanya kilimo cha parachichi kwa miaka nane sasa, nilichokiona ni haya;
1. Kilimo kina mzunguko wake ni mdogo parachichi huzaa kidogo kidogo kadri miaka inavyoenda, unatumia million 10 unapata million mbili.
2. Bei hazijadiliki anayeamua ni mnunuzi unless uwe na mtaji mkubwa ambayo unakuruhusu ku export mwenyewe, na uwe na uwezo wa kuwa na cold room Ili zikikomaa uchume uzihifadhi kama bei hueilewi kwa kipindi hicho (hii mitaji watanzania wengi hatuna). 3. Management ya parachichi ni ngumu sana linahitaji maji kidogo (hapa unaweza manage kumwagilia) linahitaji mbolea za chumvi na mbolea za majani, sumu. Kila nk kwa kiasi kidogo, linahitaji muda Kwa wingi, upatikanaji wa Samadi ni mtihani sana (wengi wamejikuta parachichi zimedumaa na wengine wanazalisha reject kwa wingi) kisa tu wameshindwa kuwa na Samadi, udhibiti wa nyasi (ukweli ni kuwa Ili miti iwe Bora unahitaji kulima badala ya kufyeka nyasi)
Nimefanya observation shambani kwangu panapolimwa pana matokeo kuliko panapofyekwa, distance kati ya mti na mti inamua sana miti iliyokaribu inasumbua sana na mingi huwa haizai vizuri. Hizi issue zimefanya watu tukimbie mashamba yetu, hata kiwango cha pesa kinachotajwa wengi hawapati ni figure za uwongo Ili kujifariji, njoo na hoja zako kupinga zangu hapo juu, zangu ni hizo.
Nashauri kama una pesa zako kidogo lima mazao ya chakula tu viazi, mpunga, mahindi nk hivi vinalipa. Huku pesa ipo na kama location ulipo ni nzuri lima mazao yanayohifadhika like kahawa, miaka miwili inazaa, management yake rahisi. Nalima kahawa makete pia ni mwaka wa tatu tayari nimeanza kuvuna.
NB: Mazao ya chakula ndio kila kitu hizi nyingine tabu umezitafuta.
Mbona bado Parachichi linahitaji hata huku nchini. Binafsi nimepanda huku Rungwe na kule Kilolo Iringa. Mengi umesema kweli hususan kwenye gharama za kulihudumia. Kuhusu soko, linacheza kwa kulingana na mwaka/msimu na soko la Dunia. Binafsi nimeyatrain maparachichi yangu so huwa naona mwezi wa 9 hadi 11 (OFF SEASON) ambapo duniani hakuna Parachichi so soko huwa la uhakika na ninapiga Bingo hapo. Kikubwa uwe na source ya maji ya uhakika tu mkuu.Binafsi huwa sina imani sana na mazao yanayotegemea mnunuzi mmoja tena wa nnje ya nchi,mazao ya chakula soko lake liko huru sana, ni nguvuzako tu mwenyewe.
Nchi za wenzetu zinajali sana walaji.Ukitumia akili kwenye jambo lolote unalofanya utakwepa mishale kama hii. Nimesoma na kufuatilia sana parachichi kwa China na nimekubali ni biashara ngumu sana.
1. Soko lake kubwa hasa hizo Hass ni China ambapo wao soko lao linapanda na kushuka kutokana na supply wanayopata kutoka Mexico, Kenya, Australia na zaidi ya nusu kutoka Peru. Ikitokea ni msimu wa Peru huko kwingineko bei inashuka sana, muda wa kupiga hela ni pale nchi nyingine zinapokuwa sio msimu.
China iko busy kujitosheleza kwenye parachichi kwahiyo soko litazidi kupungua, na uzuri wa China ni nchi kubwa yenye usawa wa bahari tofauti sana kila eneo hivyo kila upande unaweza zalisha kwa msimu wake na zikawa sokoni mwaka mzima.
2. Teknolojia hatuna. Unavuna parachichi unapakia kwenye fuso utamuuzia nani uko nje? Hamna cold rooms, hamna grading, hakuna refrigerated trucks, hamna kupima quality, water content, protein, texture, ile nyama ya ndani, mbolea haipimwi, ardhi wanatifua tu hata hawajui ardhi gani ina nini na inakosa nini. Tunaenda kienyeji.
3. Serikali inasubiri kutoza ushuru na kodi, yenyewe hata haijui hiyo biashara na kilimo chake inafanyikaje. Hakuna support kabisa sababu parachichi zikiachwa nchi haitokufa njaa.
4. Ni zao lenye usumbufu na linataka mtaji mkubwa. Wakati huo haliuziki ndani, ukikosa soko la nje ukauza ndani unakula hasara kutokana na gharama kubwa za uendeshaji.
5. Ni zao gumu sana kuuzwa, yani hawa walanguzi wetu wakienda nje uko wanapigwa za uso kirahisi sana. Unatafuta certifications za ubora na kila kitu unapeleka msimu huu, msimu ujao unaweka mtaji wote then Wachina wanapima wanakuta water content kubwa kisa mvua zilizidi uko Niombe. Zinamwagwa, huyo mfanyabiashara atarudi?
Mwaka juzi Wakenya walizuiwa na TFDA ya China kwamba kuna mlipuko wa fruit flies parachichi zao zinaenda na mayai yake. Wakaambiwa ukitaka kuuza menya uuze ile nyama ya ndani. Sasa process ya kumenya na kuuza nyama ya ndani alafu hiyo nyama isiwe nyeusi hata kidogo sio kazi ya kitoto.
Haya yote nimeyajua nikiwa sina mpango wa kulima, ningetaka kulima ningejua mengi zaidi. Sasa mkulima yeye akisikia kwenye redio anaamka na kufyeka eneo atengeneze shamba. Content creators ile ndio kazi yao, kuongea. Usikubali kushikwa masikio
Theories za supply na demand ndizo zimeyumbisha hiyo biashara kwa kiasi kikubwa,Nadhani ni mwaka juzi, wilaya ya Rungwe walipatapata kidogo kilo ilikua bei.
Ila mwaka huu ni kulia na kisaga meno, unaambiwa parachichi linauzwa kwa viroba na sio kilo tena.
Parachichi sio kilimo cha kukimbilia saivi, wengi walifyeka mapori walime parachichi ila ndo ivo wamepigwa za uso.
Tuliwaonya Rungwe walipokua wanakata migomba ili kuanzisha kilimo cha parachichi. Binafsi niliwaambia waww makini, wasikimbilie wote huko , kwani kwa wingi wanaoenda nao itapelekea zao hilo lipatikane kwa wingi na hivyo kushuka thamani.Nadhani ni mwaka juzi, wilaya ya Rungwe walipatapata kidogo kilo ilikua bei.
Ila mwaka huu ni kulia na kisaga meno, unaambiwa parachichi linauzwa kwa viroba na sio kilo tena.
Parachichi sio kilimo cha kukimbilia saivi, wengi walifyeka mapori walime parachichi ila ndo ivo wamepigwa za uso.
Migomba ilifyekwa mno, misitu ikachomwa moto na kuvunwa hovyo ili wapande maparachichi.Tuliwaonya Rungwe walipokua wanakata migomba ili kuanzisha kilimo cha parachichi. Binafsi niliwaambia waww makini, wasikimbilie wote huko , kwani kwa wingi wanaoenda nao itapelekea zao hilo lipatikane kwa wingi na hivyo kushuka thamani.
Zaidi kwa kuwa hawana access na soko, wao wanajikuta wanalima ili kujazilizia demands za yule mzungu mwenye access na soko, na wakishakuwa wenggi wataishia kumfaidisha huku wao wakudumaa
Unafahamy kitu kinaitwa tracebility?Na hayo maparachichi yoote mkivuna na kuuza huko Ulaya yameandikwa Made in Kenya[emoji16].
Nimeyaona juzi tu Belgium.