Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Ni hakilipi kwa Tanzania pekee au Dunia nzima? Shida iko hapo, Ukifuatilia Wakenya wanakimbizana na Parachichi balaa.
 
Amna kilimo rahisi mkuu,ukishaamua kuwa mkulima we kuwa chizi kilimo,lima mazao mengi tofauti tofauti,lima katani,lima korosho,lima parachichi,lima machungwa utatoboa tu moja likizingua lingine linakulipa maisha yanasonga.

Kilimo ni dynamic just imagine unazalisha kitu usicho kuwa na uwezo wa kuconsume in any how...sasa si kamali hiyo
 
Binafsi huwa sina imani sana na mazao yanayotegemea mnunuzi mmoja tena wa nnje ya nchi,mazao ya chakula soko lake liko huru sana, ni nguvuzako tu mwenyewe.
 
Binafsi huwa sina imani sana na mazao yanayotegemea mnunuzi mmoja tena wa nnje ya nchi,mazao ya chakula soko lake liko huru sana, ni nguvuzako tu mwenyewe.
Mbona bado Parachichi linahitaji hata huku nchini. Binafsi nimepanda huku Rungwe na kule Kilolo Iringa. Mengi umesema kweli hususan kwenye gharama za kulihudumia. Kuhusu soko, linacheza kwa kulingana na mwaka/msimu na soko la Dunia. Binafsi nimeyatrain maparachichi yangu so huwa naona mwezi wa 9 hadi 11 (OFF SEASON) ambapo duniani hakuna Parachichi so soko huwa la uhakika na ninapiga Bingo hapo. Kikubwa uwe na source ya maji ya uhakika tu mkuu.
 
Nchi za wenzetu zinajali sana walaji.

Tanzania ni nchi ambayo haijali walaji ndio maana Matunda huanguliwa na kupakiwa kwenye mafuso

Nchi zingine mf Marekani nimewahi fatilia youtube kila bidhaa lazima ipite kiwandani kusafishwa na kuwa packed kuanzia machungwa hadi vitunguu lazima viwe packed.

Huku kwetu nenda pale Mahakama ya Ndizi Mabibo utaweza acha kula ndizi

Nenda Temeke, Tegeta Nyuki hakika huwezi kula.

Madawa mengi sana hutumika muda mfupi kabla ya kuvuna, nina Nyanya nimekaa nazo Mwezi na siku 2 haziozi hadi nikazitupa hazina funza wala nini
 
Theories za supply na demand ndizo zimeyumbisha hiyo biashara kwa kiasi kikubwa,
The higher the supply the lower the demand
 
Tuliwaonya Rungwe walipokua wanakata migomba ili kuanzisha kilimo cha parachichi. Binafsi niliwaambia waww makini, wasikimbilie wote huko , kwani kwa wingi wanaoenda nao itapelekea zao hilo lipatikane kwa wingi na hivyo kushuka thamani.
Zaidi kwa kuwa hawana access na soko, wao wanajikuta wanalima ili kujazilizia demands za yule mzungu mwenye access na soko, na wakishakuwa wenggi wataishia kumfaidisha huku wao wakudumaa
 
Migomba ilifyekwa mno, misitu ikachomwa moto na kuvunwa hovyo ili wapande maparachichi.

Kwa maana waliopanda mwaka juzi saivi wanalia tu,parachichi liliwafaidisha wale watu wa mwanzo kabisa miaka ya 2011 kidogo mpaka mwaka juzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…