Ukweli kuhusu Israel, Waarabu, na Ibrahim

Nani kasema Musa Pharaoh na Musa ni waarabu.... Acha kukurupuka, rudia soma kisha uelewe, ukichukua point bila kusoma kwa umakini lazima upuyange kama unavyopuyanga sasa
Kichwa chako ni kizito kama asili ya hiyo jina lako. hata mimi sikusema Musa ni Maarabu. Ulikuwa unatulazimisha kuwa Musa klazaliwa katika nchi ya waarabu wakati enzi za Musa Misri ilikuwa lkwa Mafarao weusi tii wa jamii za Kusubi. Nilichosema ni kuwa kama Hajiri ni Mmisri basi hawezi kuwa Muaarabu maana zama hizo misri haikuwa na waarabu.
 
Naomba kufahamu aliyekaribia kuchinjwa na Ibrahim ili kumtoa sadaka ni nani kati ya hao wawili?
Mara kadhaa nimesikia Masheikh wakisema katika ile sikukuu ya kuchinja kwamba Ismail alinusurika kuchinjwa kwaajili ya sadaka ya baba yake, wakristo wanasema Ismail aliondoka Israel kwenda kwao na Mama yake Hajir akiwa mdogo sana ikimaanisha Ibrahim hakuwa na huyo mtoto wakati akienda kutoa sadaka ya kuchinja. Je ukweli ni upi?
 
Uarabu kwa ismail unatokana na yeye kwenda kukaa huko kwenye Penisula ya uarabuni na akaoa huko uarabuni na kupitia ismail koo nyingi na kabila nyingi zilitengenezwa na kwa sababu Mungu aliweka agano na Abraham kuwa atakuwa Baba wa mataifa mengi basi Waarabu wao wakaona Taifa lao limetokana na ismail, wakamwita Baba wa waarabu
 
Sahihi kabisa. uwe unaleta masomo yanayojieleza vizuri kama hapa. big up!
 
Kwa mujibu wa kitabu cha Kiyahudi torati ambayo Biblia nayo ikiambatana.... Vinasema kuwa Ibrahim alikuwa na watoto wawili ambao ni Isaka na Ismail. Ismail ni mtoto aliyepatikana nje ya Ndoa baada ya kukaa muda mrefu bila Sara kupata ujauzito, hivyo hajir akachaguliwa na sara hili wapate mtoto. Lakini badae baada ya kilio cha muda mrefu Mungu akawabariki mtoto naye wakamwita Isaka, na Ibrahim akampenda sana huyo mtoto badae Mungu akataka Isaac atolewe sadaka kwa sababu alimtii Mungu ikabidi aende kumtoa Isaka sadaka kwa moyo mmoja, lakini badae akatokea malaika na kumuonesha kondoo kama mbadala... Kutokana na kitendo cha utiifu na imani kwa mungu na kuthubutu kwenda kumtoa Mwanae aliyempenda na aliyempata kwa shida basi Mungu akambariki na kumwambia utakuwa baba wa mataifa mengi na mataifa yatatoka kwako
 
Hajira alikua Mmisri kumbuka accient time Khemet waliishi Blacks soma historia vizuri
hajra alikua Mweusi tii kama hao South Sudan people ambao chimbuko lao ni Kemet na Kush kwa Nubian
waarabu walihamia hapo misri miaka ya juzi AD na sio BC!
mkuu Mhaya pitia madesa vizuri Ismail hajawahi kua Mwarabu ila ni Chotara la Babylon na Kemet na alikua half Black!
 
Hapa ndipo nashindwa kumuelewa Mungu, kwanini aliingiwa na tamaa hiyo ya kuua?
 
Natamani ningesikia kutoka kwa Shosti FaizaFoxy maana upande wake unazungumza tofauti haumtaji Isihaka unamtaja Ismail
 
Ibrahim hakuwa mwarabu wala myahudi bali alikuwa mkurudi kutoka Iraq.
 
Hapa ndipo nashindwa kumuelewa Mungu, kwanini aliingiwa na tamaa hiyo ya kuua?
Tamaa ngani... Tamaa ni kwa kitu kisicho chako, sisi sote ni wake... Uwezi kuwa na Tamaa na mali yako.

Pili Isaka kwa sababu alikuwa anapendwa sana na baba yake, hivyo Mungu alitaka kujua je Ibrahim anauwezo wa kupoteza kitu anachokipenda kwa kukitoa kwa Mungu. Lakini Ibrahim akaonesha hali ya juu ya utii na Imani kwa Mungu na akawa radhi kumtoa mwanae ampendaye kama sadaka. Mungu aliona uthubutu, utii na Imani ya Ibrahim akaamua na kumbariki kuwa baba wa mataifa mengi, kwamba kupitia hao watoto wake mataifa mengi yatapatikana

Lilikuwa ni fundisho kwamba unapotoa sadaka au msaada basi toa kitu kwa Imani, husiweke Duku duku kwamba nampa shati langu zuri atapendeza kunizidi. Ukitoa kwa moyo safi basi Mungu nae atakubariki mara dufu kama Ibrahim alivyobarikiwa kuwa na uzao mkubwa wa mataifa mengi
 
Sina uthibitisho wa moja kwa moja juu ya hilo... Yani vivid evidence, maana waarabu nao wanasema alikuwa muarabu
 
πŸ‘πŸ™
 
Kwa sababu chimbuko la uislamu linaanzia kwake
Kaka usipotoshe watu jifunze kwanza uislam uulewe,usiandike vitu usivyovijua ni Bora uachie watu wanaojua utaumbuka.chimbuko la uislam halianzii Kwa Ismael ndugu.
 
Kaka usipotoshe watu jifunze kwanza uislam uulewe,usiandike vitu usivyovijua ni Bora uachie watu wanaojua utaumbuka.chimbuko la uislam halianzii Kwa Ismael ndugu.
Waislamu wenyewe wanakuambia uislamu ulikuwepo tangu enzi za Adamu πŸ˜‚
 
Abraham,moses,saul,Daud,solomon hawa wote hawajawahi kuwepo ni hekaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…