Ukweli kuhusu Israel, Waarabu, na Ibrahim

Ukweli kuhusu Israel, Waarabu, na Ibrahim

Mama yake hakuwa mwarabu alikuwa kijakazi mwenye asili ya Afrika huko habeshi(Sasa Ethiopia)soma kwanza historia kabla ya kukurupuka
Sikupingi... Ila Ibrahim alibarikiwa kuwa baba wa mataifa mengi na ismail alienda kuishi uarabuni huko ndiko alikooa na kuzaa koo mbalimbali ndipo waarabu wakamuita baba wa waarabu
 
Waarabu ni marufuku kabisa kufata ukoo wa mama,kwanza mwanamke kule hatakiwi hata kusogea mbele za watu.
Sawa je unafahamu mamake yakobo ni syrian?na kwamba ili aoe Yakobo ilibidi arudi syria kwa mjombake Laban kwa ajili ya kuoa?,kwahiyo kiufupi uzao wa yakobo wote wale wana 12 ni syrian kwa mujinu wa DNA
 
Tupeane elimu kidogo, kuna watu wanachanganya mambo. Hapa tufundishane jambo moja. Kitu cha kwanza kabisa watu wanachokichanganya ni kuhusu Ibrahim, wengi wanasema Ibrahim alikuwa Mwarabu, ndugu yangu, nikwambie tu kwamba jamaa hakuwa Mwarabu.

Ibrahim baada ya kuzaa na kijakazi ambaye alikuwa Mwarabu, inamaanisha damu yake ilichanganyika na ya Kiarabu na ndiyo maana tunasema Ishmael ni baba wa Waarabu kwa sababu mama yake alikuwa Mwarabu.

Nchi za Kiarabu ambazo zipo kwenye umoja ni hizi, Algeria, Bahrain, Iraq, Jordan, Kuwait, Djibout, Saudi Arabia, Tunisia, United Arab Emirates, Yemen, Somalia, Sudan, Syria, Comoros, Misri, Maurtania, Qatar na Palestina.

Kwa nini Waarabu wanamchukia Israel? Ni kwa sababu si Mwarabu mwenzao. Na hao ndiyo wa kizazi cha Ibrahim. Kwa hiyo kama ulikuwa unahisi Ibrahim alikuwa Mwarabu, futa hiyo akilini mwako.

Hata Iran sio Waarabu, najua wengine mtakuwa hamlijui hili kwa undani. Miongoni mwa nchi za Kiarabu, Iran hayupo kwa sababu yeye si Mwarabu.

So Israel na Waarabu ni baba mmoja ila mama tofauti. Ibrahim alizaa na Muisrael mwenzake kwa kipindi hicho ilikuwa bado haijaitwa Israel na mtoto wake kuitwa Isaka ila yule aliyezaa na kijakazi ambaye ni Mwarabu anaitwa Ishmael. Tatizo kubwa la vita baina ya Mwarabu na Israel ni hapa.

Kama Israel angekuwa Mwarabu, leo usingesikia vita vinavyoendelea huko. Na mara zote Israel anawaambiaga kwamba nchi zote za Uarabuni ni mali ya Israel na ndiyo maana kila anapokwenda kupiga, anachukua ardhi na kutanua nchi yake.

Israel walipewa nchi ndogo sana wakae baada ya kutawanywa na Adolf Hitler, baada ya kuanza kurudi, wakaitaka nchi yao, lakini kwa bahati mbaya waliwaona Waarabu washajigawia ardhi yao. Walichokifanya ni kuanza kupigana nao.

Kama unakumbuka Umoja wa Mataifa uliingilia kati, ulichukizwa na kitendo cha Israel kuwapiga Waarabu, walichokifanya, wakawapelekea Biblia ambayo kwa nyuma kuna ramani ya Israel tangu enzi za Musa. Wakawaonyesha na kuwaambia kwamba nchi zote za Uarabuni ni Israel, tutakapokuwa wengi, tutaendelea kupiga na kuirudisha nchi yetu.

So jua hili. Ibrahim hakuwa Mwarabu. Musa hakuwa Mwarabu. Suleimani mtoto wa Daudi na baba yake huyo hawakuwa Waarabu. Ni Waisrael ambao bado wanaendelea kupigana na Waarabu ili wachukue nchi yao iliyowafanya waondoke Misri.

Uzao wa Ibrahim ndiyo uliomleta Yusufu ambaye akawachukua Waisrael kwenda kuishi Misri. Maisha yalikuwa ya raha sana, watu waliionjoi maisha lakini baada ya mfalme huyo kufa, ndipo akaja mfalme mwingine ambaye sasa hakuwataka Waisrael, akawafanya watumwa wake.

Wakafanyishwa kazi. Baadaye ndipo Musa akazaliwa ndani ya ardhi ya Kiarabu. Akapewa jukumu la kuwatoa Israel kutoka hapo Misri kwenda kwao. Wakati huo ndio ambao nao Waarabu walikuwa wamejinyakulia nchi, tena walikuwa ni watu wakubwa kimuonekano.

Musa akaanza mchakato wa kuwatoa Israel Uarabuni na kuwapelekea Israel. Waliishi Misri kwa miaka 400. Wakaondoka na kwenda Misri, na walitumia miaka 40.

Musa hakuingia Israel, alikufa jangwani na Mungu kumzika. Wale waliofanikiwa kuingia huko Israel ndio walioendelea kuipambania ardhi yao mpaka leo hii.

Hapa kuna jambo moja.

Vita ya Israel na Waarabu itapamba moto hapo baadaye. Itapigwa vita kali sana. Sasa kwa kuwa Israel ataonekana kuwa kiburi na mwenye nguvu sana, dunia nzima itaanza kumcharaza. Huyu Marekani anayeonekana kuwa karibu na Israel naye atamgeuka, kila nchi duniani itamgeuka na kumpiga.

Mwisho wa siku baada ya kuona wanapigwa sana, watakimbilia mpaka kwenye mlima ule aliopaa Yesu, wataomboleza na kulia, hapo ndipo Yesu atashuka kuimaliza vita hiyo, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa kila kitu.
Hu "umoja wa nchi za Kiarabu" ulikuwepo wakati wa Ibrahim?
 
Israeli ni utaifa ambapo ndani ya Israel kuna wayahudi, Wakristo, waislamu, freemason, wapagani.
Naona una maanisha myahudi
 
Unaongelea nchi "israel", ilikuwepo wakati wa Ibrahim?
 
Waisrael halisi hawapo hapo mashariki ya kati wenyewe ni weusi kabisa na wapo tabora igunga na soon watarud ku claim nchi Yao hao wapalestina na hao mamluki apo TelAviv watafute pakwenda
 
Nipe kifungu kuwa Musa ni mweusi
Sasa hiyo ndo tunaita ki 'psychology denial' 🤣🤣
Umeomba kifungu kama suleiman mweusi nimekupa ngoja namaliza kuandika jibu la waraka wako wote hapa nitautuma...
 
Nchi ilikuwepo ila jina ndio limekuja hapo badae

Ni kama unavyosema Chief Mkwawa au Kinjeketile alikuwa Mtanzania wakati miaka hiyo jina Tanzania au nchi hiyo haikuwepo
Iliitwa caanan,,caanan ilikuwa ni moja ya majimbo ya Egypt kingdom
 
/storage/emulated/0/Download/ANCIENT_FICTIONALITY_Moses_Exodus_and_th.docx
 
Back
Top Bottom