YOHANA 14 :6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
MIMI SIWEZI KUJIBU ILA NITAMUULIZA YESU ANASEMAJE.
ANASEMA YEYE NDIO NJIA NA KWELI NA UZIMA . MTU HAENDI KWA MUNGU ILA KWA KUMFUATA YESU.
TAZAMENI NIMEKWISHA KUWAONYA.
Habar?
Kwanza tuangalie history tunazoziita dini na mitume yao (kwa kuzingatia mafundisho ya kiislamu)
1. Uyahudi, mtume wanaemfuata ni Mussa A. W (Jesus) ambae utume wake ulikuja kabla ya Masihi Issa A. W,
2. Christian, mtume wake ni Issa (Jesus) ambae utume wake ulikuja baada ya Mussa na kabla ya Muhammad S. W
3. Islam mtume wake ni Muhamad ambae alitanguliwa na Mussa na Issa
Kwanini dini hizi zinafanana?
Dini hizi zinafanana kwa sababu zifuatazo:
1. Dini zote zinafuata vitabu vilivyoshushwa na Muungu, Tautart for wafuasi wa Mussa ie Uyahudi, injil wafuasi wa Issa ie Christian na Quran wafuasi wa Muhammad ie Islam.
2. Kwa kuwa msingi wa vitabu vyake umetoka kwa Muumba mbingu na Ardhi nk, nilazima kwaasilimia kubwa zitakuwa na mafundisho yanayolingana au kufanana.
3. Mitume wote hao ni wateule wa Muungu na wamekuja kufundisha jamii zao namna ya kumtambua Muungu wao na kuweka mahusiano baina ya binaadamu na Muumba wao ie Ibada.
Kwanini dini hizi zinatafautiana?
Dini hizi zinatofauutiana kwenye baadhi ya mambo ya Ibada na sheria lakini hazitafautiani kwenye misingi mikuu ya dini kama vile Kuwepo muungu, malengo ya kuumbwa binaadamu nk. Tofauti kubwa imekuja kwenye baadhi ya sheria kwamfano kipindi cha Mussa unapoingia najisi kwenye mwili unatakiwa ukate eneo la mwili kwa kutoa nyama ya mwili kwa sehemu iliongia, wakati wa Muhammad unatakiwa usafishe tu kwa kutumia maji au mchanga, idadi ya swala, namna ya kufunga, adhabu za wizi na uzinzi nk
Kwanini kuna upinzani baina ya dini hizi?
Upinzani wa dini hizi umekuja kutokana na wafuasi wa dini zenyewe kwamfano wafuasi wa Mussa ie uyahudi waliendelea kufuata mafundisho ya Mussa kwenye wakati ambao sio awamu ya mussa ie awamu ya Jesus, wakati hawakutakiwa kufanya hivyo na ubaya zaidi ukaidi huu ulipelekea kubadilisha baadhi ya maandiko ya kitabu kitabu chao ie Taurat ili kujenga hoja ya kutakumfuata mtume Jesus.
Vile vile wafuasi wa Jesus waliendelea kufuata mafundisho ya Jesus katika kipindi cha Muhamad, ambacho hawastahiki kufanya hivyo na ubaya zaidi katika kufanikisha lengo la kutokumfuata na wao wakalazimika kubadilisha baadhi ya maandiko yao ili kupata hoja za kutokumfuata mtume wa awamu mpya ya kiutume.
Kwa upande wa mitume awamu iliohai kwa sasa ni ya Muhamad kwani hakujaletwa mtume mwengine baada ya kwake.
Kwanini hoja ya kuwa Islamu umewekwa na christian?
Majibu, wanaosema hevyo wameoanisha feature nyingi zilizopo kwenye christian ambazo vile vile zimechukuliwa kwenye mafundisho ya uislamu, na kwa kuwa mafundisho ya christian au uyahudi yalitoka kwa muungu lakini binaadamu eidha kwa kusahau au kukusudia kupotosha baadhi yamafunzo hayafanywi kwa usahihi au yanafanywa kwa usahihi kwa kulinganisha na yalipo teremka kwenye awamu husika, ila kwa awamu ya Muhamad ambae ndio current in power yameimarishwa na kutekelezwa kwanjia bora zaidi (nb mafundisho ya dini ya uislamu sio behaviour za waislamu ninachokizungumzia hapa)
Conclusion.
Kwa kuwa dini ni mwenendo wa maisha yakila siku yanayoongozwa na itikadi ya kuwepo kwa Muungu, na kuwepomajukumu yaviumbe vilivyoumbwa kwa muumba wao, na ikiwa utaamini kuwa Muungu huyo ni mmoja na hana mshirika kwenye uungu wake, ukiamini hivyo haijalishi nimfuasi wa mussa, issa au mitume ilipita nyuma zaidi kama adam, nuh, yussuf nk imani hio inaitwa ni uislamu ie kujisalimisha (surrendered kwa Muungu), kwa hio issue sio jina issue ni sifa za jina, ikikwa jina lolote la dini ikiwa na feature tulizoeleza unaweza ukaita uislamu au jina jingine.
Naomba kuwasilisha