Ukweli kuhusu Mradi wa NSSF wa Dege Beach Kigamboni

Mimi sielewi aliyesema uongo ni gazeti au report ya CAG?
Mtajitetea sana mwaka huu. Tumechoka story mtajitete mahakamani
 
Mkuu Samvulachole,

Mie naona huna hoja hapa, kama NSSF haijanunua hiyo ardhi sawa lakini huwezi kusema imepewa bure.

Ngoja nikupe mfano mdogo tu, tunataka kujenga Nyumba ya Biashara mimi Shark na wewe Samvulachole. Gharama za ujenzi wa nyumba hiyo ambazo mimi nitazitumia labda ni 60mil. Wewe unatoa kiwanja (unachokiita cha bure) unasema kina value ya 40mil. Hivyo gharama za ujenzi za Jumla hapa zitakua 100mil hivyo mimi nitakua nimetumia 60% ya ujenzi wote huku wewe ukidai umetumia 40% ya ujenzi wote (Capital invested). Na makubaliano ni kugawana faida kulingana na % ya uwekezaji (60:40)

Ukute kumbe wewe kiwanja chako market value yake ni labda 10mil tu na sio 40mil kama ulivyotaja awali, hivyo umewekeza 10mil/(60mil +10mil) = 14.3% ambayo ungestahili kama mgawo/hisa zako na sio 40% za awali, huoni kama hapa wewe Samvulachole /Azimio unanidhulumu mimi Shark /NSSF??

Sawa, mimi sijanunua kiwanja kwako kwa hiyo 40mil lakini ndio mtaji ulioutaja, na kwenye mgawo nawe utakuwepo sababu umetoa mtaji wa kiwanja. Lakini huoni kama kwa wewe kutaja value kubwa ya mtaji wako wakati sio itakupelekea wewe kupata mgawo mkubwa zaidi ya unaostahili??
 
Kwa taarifa yako tu, Management letter iliyoliyoleak ilikuwa bado mikononi mwa Ernest n Young ambao walikuwa ndio principal auditors. Hawa ndio walio audit Financial statments za NSSF na kutoa opinion. CAG kazi yake ni kusign tu report cuz kazi yote ya audit ilifanywa na EY.

Kumbuka pia unqualified opinion iliyotolewa na EY ilibase kwenye presentation ya financials informations kuwa hazikuwa na any material misstatement. Kazi yao haikuwa kudetect fraud.

Ndio maana EY walisight tu issue ya fraud kwenye hizo project kwenye ML yao na hawakuwa na mandate yoyote ya kuendelea zaidi.
 
Mimi kiwanja changu mtu hanipangii bei,hakuna cha market value wala nini,ukitaka kuwekeza kiwanjani kwangu unafuata masharti yangu,hutaki acha....



Ha ha ha.

Hata hivyo hiyo hesabu ya 800 kwa hekali ni hesabu za mtandaoni na wameipata kama sikosei kwa kugawanya gharama za mradi,gawa kwa idadi ya heka,wakapata milion 800.
Sasa sijui wameconsider na ile 35% ya gharama ambazo azimio angechanga katika ujenzi wa mradi hadi unakamilika,

kiuhalisia huyo mwenye ardhi kama mradi ukikamilika na kuanza kazi na ufanye kazi kwa miaka 100 tuseme,
mapato yake ni maradufu ya hizo milion 800 kwa heka,
 
ametoa kiwanja chake kwa kuhesabiwa kama 20%.
Atatoa pesa 35% ya gharama za mradi.

Kwanini asiwe majority shareholder?
 
kwa mawazo yako unadhani hiyo azimio ni kampuni ngeni sana katika mambo ya real estate.

Hakuna hela ambayo nssf wamelipa kununua kiwanja kwa bei ya milion 800 kwa heka,mmekaririshwa,
kile kiwanja ni mali ya hiyo kampuni ya azimio

Wewe una akili kuliko CAG,EY NA woote wanaofuatilia hili swala,hongera mlamba miguu
 

Nenda katoe ufafanuzi wako bungeni
 
 
Ukaguzi ulifanyika dau akiwa DG,ila wakati wa exit meeting dau alijifanya mjanja ili awashikishe vijana wa CAG(EY) ila vijana walikomaa,dau kuona hivyo ktk kile kikao akawaondoa wakurugenzi wote kikaoni ili awa contain wale auditors lakini wapi hadi anaondolewa Nssf bado exit meeting ilikuwa haijafanyakazi na ndipo board mpya alipoteuliwa ngoma ikafika mezani na kuidadavua,
Ila dharau za dau hasa kwa viongozi na hasa kwa wanasiasa kwa mgongo wa mkwere vimem cost sana.
 
dawa ya magonjwa yote haya ni upinzani kushika dola. basi.

kuendelea kuwa-recycle watu wale wale kwa kuwapa chokaa is a f....g waste of space!
 
mi hata sielewi. mnataja mabilioni kwa mamilioni wakati raia wa kawaida buku mfukoni sina. watizis.?
 

Aisee! Hii post imenikumbusha mwanaJF mmoja akijulikana kwa jina la Game Theory. Alikuwa mtetezi sana wa hii kitu ya NSSF. Halafu kapotea. Re-surfaced?
 
huyo mkurugenzi mpya atakuwa ni wale wenye PHD za kuunga unga,maana haingii akilini asijue hasa nini maana ya land equity,au usikute alikua mhandisi wa mabalabala,anachojua ni kutandaza lami tu
Unanunua Land equity kwa gharama ya milioni 800 kwa acre Kigamboni!!!
 
YAANI HAWA NSSF WANA MIRADI MINGI SANA KISHA BADO WANATAKA KUZUIA PESA ZETU HADI TUFIKISHE MIAKA 55!!!!!! PTYUUUUUUU!!!!!!!!!!

MIRADI YOTE HII INAINGIZA PESA NA WAJANJA WANAKULA TU. WANACHAM HATUNA FAIDA NAYO.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!!!!!
 
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni

Leo Magazeti mengi yameandika kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Hasa Mradi wa Dege Beach Huko Kigamboni ambapo imeelezwa Kuwa Katika Kila Kiwanja Kimoja kati ya Viwanja 300 vilivyoko Katika hatua ya kwanza ya Mradi thamani ya Kiwanja imezidishwa Kwa zaidi ya Shilingi Milioni 775. Ikielezwa Kuwa thamani ya Kila Kiwanja Ni Shilingi Milioni 25 Tofauti na Milioni 800 ambazo NSSF imenunua Kwa Kila Kiwanja Kimoja Kwa Mujibu wa Mkataba kati yake Na Kampuni ya Azimio.

Taarifa Hizi ni za Uongo. Ukweli ni Kuwa NSSF haikununua Ardhi eneo la Dege Beach, Kigamboni Kwa thamani ya Milioni 800 Kwa Kiwanja, imepewa Ardhi Bure Ili iwekeze Kwa kuingia Ushirika wa Mradi Katika Ardhi ya Mtu Binafsi (Kampuni ya Azimio).

Aina hiyo ya Ushirika hujulikana Kwa wataalam wa Sekta ya Majengo (Real Estate) Kama Utaratibu wa "Land for Equity" (Yaani Ardhi Kwa Hisa). Ambapo Katika Makubaliano ya Mradi, Mbia Mmoja wa Mradi anatoa Ardhi Na Mbia mwengine anatoa Fedha za Uwekezaji. Na kisha Hisa za Mradi hugawanywa kulingana Na mtaji wa Kila Mmoja (Ardhi Kwa Mbia wa kwanza, Na Fedha Kwa Mbia mwengine).

Na hili si Jambo jipya nchini. Uchunguzi unathibitisha kuwa kilichofanywa na NSSF (Katika Mradi wa Dege Beach Kigamboni) ndicho kinachofanywa na taasisi mbalimbali nchini (wakiwemo NSSF wenyewe), katika Miradi mbalimbali ya Uwekezaji wa Ushirikiano kati sekta ya Majengo.

Baadhi ya mifano ya Miradi ya namna hiyo ni kama ifuatavyo:

• Miaka ya 90 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliingia makubaliano na Shirika la Mafuta la Taifa (TPDC) kujenga Jengo la Mafuta House kwenye ardhi inayomilikiwa na NHC katika eneo ambalo sasa pamejengwa Jengo la Banjamin Mkapa Towers. Katika Ujenzi Huo NHC walipewa asilimia 25 ya thamani ya mradi kwa kutoa ardhi (Land for Equity) ambayo mwaka 1995 ilikuwa ni Shilingi bilioni 19 bilioni. Kwa mujibu wa mkataba huo thamani ya ardhi ile mwaka huo ilikuwa shs 4.75 bilioni.

Mwaka 1995 thamani ya ardhi katikati ya jiji la Dar es salaam ilikuwa ni shilingi 62,500 kwa kila mita ya mraba na kiwanja kile kina mita za mraba 6,221 sawa na ekari moja na nusu. Kwa kutumia mahesabu ya kawaida thamani ya ardhi ya NHC ingekuwa shilingi 388 milioni Na si hiyo 4.75 Bilioni ambayo inaonyesha bei kukuzwa Kwa nyongeza ya shilingi 4.35 bilioni.

• NSSF ni mfaidika wa Utaratibu wa "Land for Equity" Katika mradi Mpya wa Umeme Mkuranga. Mwaka 2014 NSSF ilinunua ardhi kwa thamani ya shilingi 100 milioni, ardhi hiyo ilikuwa Ni jumla ya ekari 100.

Mwaka 2015 Wawekezaji waliingia ubia na Shirika la NSSF Ili kujenga Mtambo wa Umeme Katika ardhi Husika. Mchango wa NSSF Katika Mradi Huo ulikuwa ni ardhi yake ya Ekari 100 ambayo iliinunua Kwa Shilingi Milioni 100 Tu Mwaka Mmoja nyuma. Lakini Katika Mkataba wa Mradi Huo NSSF imepata asilimia 10 ya thamani ya Mradi Mzima wa Uwekezaji ambayo ni Dola za Kimarekani 450 Milioni Sawa na zaidi ya Shilingi 900 Bilioni.

Katika Mradi huu wa Mkuranga NSSF ndani ya mwaka mmoja iliweza kupandisha thamani ya ardhi ile kutoka shilingi 100 milioni mpaka shilingi 90 Bilioni ambayo ni Asilimia 10 ya thamani ya Mradi Wote. Kama zingetumika Hesabu Za kawaida Tu thamani ya Uwekezaji wa NSSF kwenye Mradi Husika ilipaswa Kuwa Asilia 0.06 Tu Na Sio Asilimia 10 walizopewa.

• Mradi mwengine uliofuata Utaratibu wa "Land for Equity" (Ardhi Kwa Hisa) ni Taarifa Juu ya makubaliano kati ya NHC na PPF Katika Ujenzi wa Jengo la PPF Tower Mwanza, ambapo NHC walitoa ardhi na kupewa Aslimia 25 ya hisa za mradi husika. Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni 258, Lakini Ukubwa wa ardhi waliyotoa NHC ni Kiwanja cha ekari moja tu.

Kamwe huwezi kusikia ikisemwa kuwa PPF wamenunua Kiwanja Cha Ekari Moja Kwa thamani ya Shilingi Bilioni 64 Kwa Kuwa Ni Ushirika wa Pamoja.

• NSSF imejenga jengo RITA, eneo la Posta jirani Kabisa na Jengo la Klabu ya Billicanas Jijini Dar es salaam. Katika Mradi Huo RITA iliyojengewa Jengo Husika, Na Kwa Kutoa ardhi hiyo wamepata hisa Asilimia 25 ya thamani ya mradi mzima wa Jengo Hilo, ambayo ni hilingi Bilioni 198.

Lakini Ukubwa wa Kiwanja cha RITA ni nusu ekari tu. Kamwe huwezi kusikia NSSF wamenunua nusu ekari kwa Shilingi bilioni 49 Katika Mradi wa Jengo la RITA.

• Miradi mengine iliyofuata Utaratibu huu wa "Land for Equity"
* Mradi kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Fida-Hussein Katika Jengo lililoko Maeneo ya Jirani Na Hospitali ya Ocean Road.
* Mradi wa Jengo la UVCCM eneo la Fire Jijini Dar es salaam.
* Mradi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation eneo la Posta.
* Mradi wa Jengo la UWT (Makao makuu ya Airtel) eneo la Morocco nk.

• Hitimisho:

NSSF iliingia ubia na kampuni ya Azimio Kwaajili ya Uendelezwaji wa Ardhi Katika Mradi wa Dege Beach Kule Kigamboni. Kampuni ya Azimio Kwa Kutoa Ardhi ya Mradi Husika ilipewa asilimia 20 ya thamani ya mradi wa Dege Eco Village.

Lakini Pia kwenye Mkataba wa Mradi Azimio wanapaswa Kutoa 35% ya Fedha za thamani ya Mradi, Hivyo kuwafanya wawe na 55% ya Mradi Husika Huku NSSF wakiwa na 45 ya Mradi Kwa Fedha watakazotoa.
 
Wangekuwa wamefanya kazi zao binafsi wangeachwa wapumzike, lakini kwa bahati mbaya sana ni kazi za Watu, wananchi wana haki ya kujua, wakishajua watakaa kimya. Iwe uongo au ukweli tusubiri tuone! Tulia Mpwa unatumia nguvu nyingi sana sana kukanusha haya mambo, kwanini? Documents kama zipi si zitaeleza? Relax
 
Hatuwez kuwaacha mkipotosha sasa

Ukweli uelezwe jamii ijue
 

Wamekufanyia wewe kwa kuwa wewe ni mnufaika,dau hakuna cha kupumzika aletwe kisutu akapumzishwe ukonga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…