Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

Je mtu akibatizwa ama kuslimu anakuwa hana haki ya kubadili jina lake?
Msanii,
Hawa wazalendo hawakumuomba father wa Peramiho aje awabatize.
Father alikwenda pale kuwabatiza akiwaambia kuwa ikiwa watakubali kubatizwa hawatanyongwa.

Father ndiye aliyeeleza kuwa kawabatiza Waislam na kuwapa majina mapya ya Kikristo lakini wenyewe walikuwa tayari wameshakufa.
 
Mohamed,
Naomba nikuulize kitu kimoja hao walionyongwa uislamu wao waliupataje, sababu wengi wao ni masalia ya Wangoni waliotoka South na Wangoni waliotoka kule hawakuwa waislamu wengi walikuwa ni ATR believers, Sasa hawa uislamu wao waliupataje?
 
Vita vya majimaji ni vita vilivyopiganwa na wazee wa kiislam kupinga utawala wa kimabavu wa kijerumani, lakini kwa makusudi vita hivi historia yake imechafuliwa kwa makusudi kuonesha kuwa vilikuwa vita vilivyopiganwa kwa imani za kishirikina.
Ina maana Kinjekitile hakuongopa kuhusu uwepo wa dawa ya maajabu yenye kuzibadili risasi kuwa maji ?... Mohamed Said
 
Jiwe ..
Hujafanikiwa kunipuuza.
Huwezi kuwa unaniandikia halafu useme unanipuuza.

Kama una nia ya kunipuuza ni wewe kutoingia kwenye mjadala wangu.
Huko ndiko kupuuza.

Humu nadhani utakuwa unaona kuna watu wakiniandikia huwa siwajibu nakuwa kimya.
 
Vishu...
Huu Uzi nini maudhui yake?
 
Mohamed,
Naomba nikuulize kitu kimoja hao walionyongwa uislamu wao waliupataje, sababu wengi wao ni masalia ya Wangoni waliotoka South na Wangoni waliotoka kule hawakuwa waislamu wengi walikuwa ni ATR believers, Sasa hawa uislamu wao waliupataje?
Mazigga,
Uislam umeingia Pwani ya Afrika Mashariki zaidi ya miaka 1000 iliyopita na kutokea pwani ukasambaa kote.

Maji Maji imepiganwa kati ya 1905 - 1907.
Jiulize Wangoni waliingia lini nchini.

Uislam haukuwa mgeni katika German Ostafrika.
Ndiyo unakuta Mngoni jina lake Abdulrauf Songea Mbano, Khadija Mkomanile.

Unawakuta Wayao kote huko kusini Waislam ndipo unampata Suleiman Mamba, Hassan bin Omar Makunganya.

Kubwa ni kuwa si Uislam tu utakutananao huko utakuta na Tariqa Quadiriyya na Makhalifa wake hii leo mwaka wa 2022.
 
Ina maana Kinjekitile hakuongopa kuhusu uwepo wa dawa ya maajabu yenye kuzibadili risasi kuwa maji ?... Mohamed Said
Proved,
Mimi hupenda watu wakatumia akili zao wenyewe kujua ukweli.

Mimi ningependa sana kukusikia wewe unasemaje kuhusu suala la maji kugeuka risasi.

Mimi hapa nitakuongezea jambo ili uongee maarifa yako.
Baadhi ya viongozi wa vita walifanyia majaribio dawa hiyo kwa mbwa.

Mbwa alikufa.
Hapa katika mitandao kuna elimu kubwa sana.

Jisomee historia ya Maji Maji kupata ukweli.
 
Mzee Mohamed Said inawezekana pia walihitimisha kuwa inafanya kazi kwa binadamu tu na sio mbwa.

Ila inawezekana upinzani wa Abushiri dhidi ya wajerumani ndio ulichukua msukumo wa kidini zaidi maana ulijikita huko Pangani kuliko Vita ya majimaji ambao ilihusisha uzalendo wa kiasili/tamaduni zaidi kuliko dini.
 
Kwa upande mmoja huo ni ukatili wa ajabu kabisa. Kwa upande wa pili ni wazi kulikuwa na hadaa nyingi zenye matumaini yasiyo na nuru kwenye hii issue.

Lakini leo tunaibadilije hiatoria wakati waandishi wake ni hao hao waliotufanyia unyama?
 
Je hawa wapiganaji wa Majimaji ktk picha toka makabila ya Wangindo, Wagoni, Wapogolo n.k zinaakisi uislamu au makabila yao ?




Picha machifu wa kiafrika waliohukumiwa adhabu ya kifo kufuatia vuguvugu la kupinga utawala wa Kijerumani almaaruf vita ya Kinjekitile Ngwale kuwaaminisha yakuwa kwa kuongeshwa maji na kuwachanja 'chale' za kufanya risasi kugeuka maji, je imani hii ni ya kiAfrika au ya kiIslamu ?




MajiMaji ilichagizwa na wenyeji kulazimishwa kulima zao la Pamba ili litumike kama zao la kulipisha kodi ya kichwa na pamba kusafirishwa kwenda nje kutumika ktk viwanda vya Ujerumani. Je katika imani na utamaduni wa kimapokeo wa dini ya KiIslamu mtawala kukusanya kodi ni haramu? Je mjerumani alilazimisha imani za kilugaluga imani zetu adhimu kabisa za kiAfrika nani alitaka kuzifuta ni wote Wajerumani kupitia Ukristo na UIslamu kupitia Waarabu au kuna mmoja kati ya hao wakuja waliwaacha wazawa waendelee na tamaduni, majina, desturi, matunguli n.k ya kienyeji yaendelee



Katika watawala hawa wawili waliowasili toka nchi za mbali kwa majahazi na merikebu ni kweli waliheshimu miungu yetu ya asili ya ZoleLanga Masika, Kinyamkela na majina yetu ya kienyeji ya Chakumwenda bin Msumari au wote walitugilibu kushawishi kwa hadaa au mtutu wa bunduki tufuate yale yote mageni waliyokuja nayo toka huko watokako kwa kuvuka bahari mpaka maeneo ya kwetu?

Picha chini : Askari 'Wamatumbi' wa jeshi la Jerumani ya Afrika Mashariki



Source : What Was the Maji Maji Rebellion?

Tujiulize ukoloni mkongwe una tofauti yoyote uwe umetoka bara Ulaya, bara Arabu au Mongolia ? Je mikakati ya kutengeneza dola ya kiJerumani, dola ya kiArabu au kiMongol n.k hata ya sasa ya KiMarekani au kiChina zinautofauti wowote tukasema bora kutwezwa(humiliated) au kulazimishwa majina mageni, tamaduni ngeni, asili ngeni (subjected), uhuru wa ahera huku uhuru wa duniani tumepokwa na wageni wakuja n.k na hivyo tujipige kifua kuwa mkoloni yule ni mbora kuliko huyu ?

 
Waafrika miaka hii baada ya uhuru wamechanganyikiwa kabisa wanaona ufahari kujitambulisha kwa kutumia dini za kitapeli za kigeni kama Uislamu na Ukristo [emoji30][emoji30][emoji30][emoji30]
 
Hamna sehemu yoyote watazidishiwa adhamu wakati hamtaki fanya kazi mmekalia ufisadi na wizi wa mali za uma
 
Kwa upande mmoja huo ni ukatili wa ajabu kabisa. Kwa upande wa pili ni wazi kulikuwa na hadaa nyingi zenye matumaini yasiyo na nuru kwenye hii issue.

Lakini leo tunaibadilije hiatoria wakati waandishi wake ni hao hao waliotufanyia unyama?
Msanii,
Historia tumeshaibadili miaka mingi iliyopita.
Unaona hapa watu wanavyohemkwa kwa kueezwa kuwa Mkwawa aliuwa Muislam.

Wenye kusema hayo ni wao wenyewe waliokuwa na Mkwawa na wameandika na kuonyesha barua alizokuwa akiandika Mkwawa kwa hati za Kiarabu.

Wameeleza urafiki baina ya Mkwawa na Abushiri bin Salim na wameonyesha na bunduki ambayo Abushiri alimpa Mkwawa.

Leo katika historia hii mimi huisomesha kupitia maisha ya Abdulrauf Songea Mbano.
 
Kwahiyo mf. Hilo la Dominic ndo la asili eti eh!
 
Mwache afanye au kuandika anachojisikia maana uhuru huo anao,,!! Wewe lete andiko lako hapa la namna yako tulisome pia..
 
Ukitaka kuona shida ya kutumia jina lisilo lako fanya hivi.. mwambie mzazi wako wakike(mama yako) abadilishe pale kwenye jina la baba yako yaani kama wewe unaitwa dindili chuma basi aseme kuanzia leo wewe ni dindili komwe.. alafu huyu komwe awe ni jirani yenu pale mtaani,, baada ya hapo wewe uje urejeshe mrejesho hapa kama Kuna shida au laaa
 
kujitambulisha kwa kutumia dini za kitapeli za kigeni kama Uislamu na Ukristo

Kabisa hawataki kusikia mazingombwe ya Kinjekitile Ngwale jina halisi la Ki-Rufiji likitumika kuwa ndiye aliwahamashisha waafrika kupambana na ukoloni mkongwe ambao hatujali kama ni wa ki-Jerumani, kiKristo, KiArabu, KiIslamu uliokuwa na nia siyo ya kututawala tu bali kufuata asili zetu za majina, mazingaombwe, destruri, mila, elimu na tamaduni zetu ili tufuate za kigeni.

Ni aibu hata wamatumbi wadai kuwa jando ni Uislamu au Uyahudi wakati mababu zetu tendo hilo lilikuwepo kabla ya wageni kutua ktk pwani ya pande hizi za dunia yetu.

Tutakataa kuuita watoto wetu Chausiku na kuwabatiza Kieran na kadhalika kama vile Afrika watoto hawazaliwi usiku au kuwaita Stella badala ya Nyota wakati pia mtoto anaweza zaliwa wakati nyota inaonekana angani.

Hii ni mifano lukuki ya kuiga ya wakuja kama vile matukio, elimu, majina ya mashujaa, viongozi wa kiimani wa kiAfrika hawakuwepo n.k n.k
 
Vita ya majimaji ambao ilihusisha uzalendo wa kiasili/tamaduni zaidi kuliko dini

Yaani najisika fahari hatimaye kuona kuwa mababu walionesha uzalendo wa kiasili / tamaduni kumkabili mkoloni mkongwe aliyekuja kwa vyombo vinavyosafiri katika bahari kubwa.

Wazee hawa hawakupigania kufia imani ya kingeni bali utu na uhuru wao wa kuzaliwa watu huru eneo hili la Afrika.

Propaganda zikawa kuwa ni Uislamu dhidi ya Jerumani au kodi ya kichwa dhidi ya Jerumani.

Hapo jambo kubwa la hadaa kuficha joho au kanzu la ukoloni wa kila aina uwe wa kidini, kibiashara ulitumika katika kuandika historia.

Na mara nyingi mshindi mwenye mabavu yaliyopitiliza ndiyo anaamua historia hiyo iandikwe vipi kwa manufaa mapana ya mkoloni awe ametoka Arabuni, Ulaya, Marekani ya Kaskazini n.k
 
Utawala wa kijerumani ulikuwa wa moja kwa moja 'direct rule' tena uliambatana na matumizi makubwa ya nguvu na ukatili ndio chanzo hasa cha kuzuka migogoro na watawala wa kijadi.

Waingereza waliona athari wa aina hiyo huko Kenya (baada ya kupambana na Wanandi), Zimbabwe na kwingineko hivyo waliwatumia viongozi hao hao wa kijadi kama daraja la utawala (indirect rule).

Kwa Sasa kusema Marekani, China n.k zina ukoloni huenda ni sahihi au sio sahihi pia, isitoshe hawa wa Sasa tumeingiliana mno kibiashara tofauti na enzi hizo na baadhi ya makampuni na mashirika yao huendesha kazi zao huku Africa na kutoa ajira, kulipa Kodi, japo wanaweza kushawishi siasa ila itategemea na nyie wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…