Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

Maelezo yako Mzee kuna sehemu sijaelewa au yanajichanganya ni kwamba hao walionyongwa waliambiwa kwamba wakikubali kubatizwa hawatanyongwa bali wataachwa, sasa imekuaje wakanyongwa wakati majina yao yanaonesha walikubali kubatizwa na kubadili baadhi ya majina yao?

Mji wa Songea una wakazi mchanganyiko toka kitambo sana, ila hilo jambo utakua umesimuliwa Mzee nenda Songea leo waulize Wazee wenyewe,,

Mimi jirani yangu alikua Mzee Mpambalioto ila bahati mbaya amefariki mwaka huu (huyu alikua ni mjukuu wa Mpambalioto ambae ni Mtemi wa kipindi hicho walipatikana katika moja ya safu za milima Matogoro) hawa ni waislamu kabisa toka zama hizo.

Mzee huyu amewai niambia kuwa wapo machifu wengi walikua wakristo na wengine waislamu mfano ukoo wa Mbano hawa wapo tena wanapatikana eneo moja linaitwa Mwengemshindo nenda pale utakutana na mbano na wengine nimesoma nao wote ni wakristo alafu kuna Gama nao ni wakristo kabla hata ya kunyongwa.

Ila wapo wengine walibatizwa kabla ya kunyongwa wengine kwa ridhaa wengine kwa lazima ila sio kama ilivyoandikwa na Mzee hapo juu
Umemnukuu ustadh ILUNGA HASSAN KAPUNGU mwenyezi Mungu amrehemu
 
Kama walibatizwa wakapewa majina mapya nashindwa kuelewa wanapoyatumia majina hayo kuna kua na shida Gani.
Pia tunaweza kutazama Koo zao sasa hivi ni watu wa dini Gani?
Huenda familia za wahusika ndio waliotaka marekebisho ya majina kwa kuona kwamba yamekosewa na wao wanajua jamaa zao walibatizwa na kupewa majina mapya.
Kama jamaa zao hawajalalamika basi walioandika upya wako sahihi.
dindi...
Hakuna tatizo.
Nimeandika kueleza historia ya yale yaliyotokea katika Vita Vita Vya Maji Maji.
 
Maalim unapendekeza nini kifanyike?
Hayo majina hayawakilishi uislamu bali Uarabu.
Mr Q,
Unavyopenda kuamini si tatizo.
Mimi naeleza historia ya Maji Maji ilivyokuwa.

Waislam wamenyongwa na wakati kabla hawajanyongwa akafika father kutoka Peramiho kuwabatiza.

Hili likasababisha majina yao ya Kiislam ukipenda ya Kiarabu yafutwe.

Hakuna tatizo ndugu yangu.
Mimi niko hapa kusomesha historia ambayo si wengi mnaijua.
 
Hayo majina ni ya kiarabu sio ya kiislamu
Najua unajua shida ni udini wa kupindukia

Mzee ukiendekeza haya utakuwa mjinga
 
Hayo majina ni ya kiarabu sio ya kiislamu
Najua unajua shida ni udini wa kupindukia

Mzee ukiendekeza haya utakuwa mjinga
Panzi...
Kuendekeza, ''scholarship,'' toka lini iwe ujinga?
Sipendi kusema haya lakini kidogo umeniudhi.

Unajua nimeandika vitabu vingapi kuhusu somo hili ninalosomesha hapa?

Unajua nimealikwa vyuo vingapi ndani na nje ya mipaka yetu kueleza haya ninayosomesha hapa?

Unajua kuwa nimebadilisha historia nzima ya uhuru na sasa wanafunzi wanasoma historia mpya ya TANU na historia mpya ya Julius Nyerere?

Unajua, unajua, unajua...
Huu ndiyo unaita, ''kuendekeza ujinga?''

Huu ndiyo unaita udini?

Wewe ulitaka mimi nikunje mikono wakati historia ya wazee wangu waliopigania uhuru wa Tanganyika inavurugwa kisa imejaa Waislam?

Nani sasa mdini kati yangu na hao?
 
Tatizo la kuwa na wasomi ambao hawajaelimika litaendelea kuitafuna sana Africa. Inashangaza kuona mtu anapigania kutambulishwa kwa majina ya 'Slave masters', majina yetu ya asili tunayaona hayana maana, hii ni aibu. Imenikumbusha song of lawino and ocol
Masta...
Jaribu kunielewa ninachoeleza.
Sipiganii jina hapa.

Hawa watu wamepewa majina ambayo si yao tena kwa kutumia ghilba.
Hawa watu mashujaa wamepigana na watu waliovamia nchi yao kutoka Ujerumani.

Hawa wamenyanyua silaha dhidi ya adui.
Hawa watu walikuwa Waislam.

Katika wakati wao wa umauti ndiyo wanafanyiwa haya.
Wanaambiwa wanaambiwa wabadili dini zao au wauawe kwa kunyongwa.

Mbona wewe husemi lolote kuhusu hili?

Huyu father aliyetumwa kutoka Peramiho alikuja Mahenge kubadili historia za hawa wazalendo.

Kwa nini hili hutaki kuliona?
Au unadhani hawa Wazungu walikuwa na haki ya kufanya vile?
 
RO7...
Mada iliyopo mezani si hiyo.
Ikiwa unapenda tujadili hili fungua uzi mpya.
UJINGA na UDINI umekujaa wewe Mzee Mohamed Said

Kwahiyo pakifutwa Dominic na kuandikwa Abdulrahman ndio atafufuka au?

Ninyi Waarabu wenye nywele nyeusi na ngumu, Pua pana na lips pana mnashangaza sana.
 
Panzi...
Kuendekeza, ''scholarship,'' toka lini iwe ujinga?
Sipendi kusema haya lakini kidogo umeniudhi.

Unajua nimeandika vitabu vingapi kuhusu somo hili ninalosomesha hapa?

Unajua nimealikwa vyuo vingapi ndani na nje ya mipaka yetu kueleza haya ninayosomesha hapa?

Unajua kuwa nimebadilisha historia nzima ya uhuru na sasa wanafunzi wanasoma historia mpya ya TANU na historia mpya ya Julius Nyerere?

Unajua, unajua, unajua...
Huu ndiyo unaita, ''kuendekeza ujinga?''

Huu ndiyo unaita udini?

Wewe ulitaka mimi nikunje mikono wakati historia ya wazee wangu waliopigania uhuru wa Tanganyika inavurugwa kisa imejaa Waislam?

Nani sasa mdini kati yangu na hao?
Acha Uongo Mzee
 
Tatizo la kuwa na wasomi ambao hawajaelimika litaendelea kuitafuna sana Africa. Inashangaza kuona mtu anapigania kutambulishwa kwa majina ya 'Slave masters', majina yetu ya asili tunayaona hayana maana, hii ni aibu. Imenikumbusha song of lawino and ocol

Dominic nalo jina?

Kukuuuu [emoji239][emoji239][emoji239]
 
Mi nimekuelewa,Ila Tumuachie Allah!!
Kiokotee,
Hili la kusahihisha historia na kuandika ukweli hili aachiwi Allah.

Hili tunaliweza.

Hili mimi nimetaka msaada wa Allah na nimelifanya limekamilika kuliko mategemeo yangu.
 
TATIZO LA MAJINA YA KIISLAM KATIKA KUMBUKUMBU YA VITA VYA MAJI MAJI (1905 – 1907) MAHENGE SONGEA
Katika kumbukumbu ya Vita Vya Maji Maji Songea sehemu inayotia simanzzi kubwa ni pale penye kaburi kubwa la halaiki walipozikwa wazalendo 67 walionyanyua silaha dhidi ya dhulma za Wajerumani. Hawa walihukumiwa kunyongwa.

Kando ya kaburi hili la halaiki kuna kaburi moja lililo peke yake.
Hili ni kaburi la Abdulrauf Songea Mbano aliyenyongwa peke yake na kuzikwa kwenye kaburi la peke yake.

Hapo Mahenge ilikuwapo orodha ya majina ya wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam.

Lakini karatasi hii yenye majina ya Kiislam yamewekwa mbele ya majina haya majina mengine ambayo si ya Kiislam.

Linaanza jina lake la Kiiislam kisha lingine mfano Abdulrahman (Dominic) Mputa Gama.

Ingekuwa kama siku kuchomekwa jina lingine jina lingesomeka kama hivi, ‘’Abdulrahman Mputa Gama.’’

Kazi hii ilifanywa na padre kutoka Peramiho aliyeletwa Mahenge kuwabatiza Waislam kwa ahadi kwa kuwa wakikubali kubatizwa hawatanyongwa.

Orodha hii yenye majina ya Kiislam hivi sasa imeondolewa na badala yake kuna orodha mpya yenye majina mengine ambayo yanasomeka kwa mfano wa hapo juu, ‘’Dominic Mputa Gama,’’ badala ya ‘’Abdulrahman (Dominic) Mputa Gama.’’

Labda tujiulize nani anafanya haya nani anamtuma nini nia ya kufanya hivi?
Lipi lisilotakiwa lijulikane katika historia ya Vita Vya Maji Maji?
https://www.theeastafrican.co.ke/te...-7SNVfAliRvaeGuYtrn0n4dPKU1IGudszkPmpZuJpbqe0
Mzee wangu Mohamed Said.
Ama kwa hakika umesheheni historia muruwa ya nchi yetu.

Kuna mambo mengine ni muhimu kuyatafakari, kwa mfano jina Julias, Robert, Said, Hamad na fananio za hayo. Hayaleti taswira njema ya asili yetu ambayo tumetokana nayo. Tumepandikiziwa utu usio wetu ndo maana chembe za ubaguzi zinatutafuna kila kukicha.

Nilidhani unapambania kutaka kuondoa majina yasiyo ya asili mbele ya majina ya mashujaa wetu. Kumbe unataka kuyaswitch kwa muelekeo wa kibaguzi.

Turudi katika asili yetu bila kuathiri imani zetu
 
Mr Q,
Unavyopenda kuamini si tatizo.
Mimi naeleza historia ya Maji Maji ilivyokuwa.

Waislam wamenyongwa na wakati kabla hawajanyongwa akafika father kutoka Peramiho kuwabatiza.

Hili likasababisha majina yao ya Kiislam ukipenda ya Kiarabu yafutwe.

Hakuna tatizo ndugu yangu.
Mimi niko hapa kusomesha historia ambayo si wengi mnaijua.
Je mtu akibatizwa ama kuslimu anakuwa hana haki ya kubadili jina lake?
 
Panzi...
Kuendekeza, ''scholarship,'' toka lini iwe ujinga?
Sipendi kusema haya lakini kidogo umeniudhi.

Unajua nimeandika vitabu vingapi kuhusu somo hili ninalosomesha hapa?

Unajua nimealikwa vyuo vingapi ndani na nje ya mipaka yetu kueleza haya ninayosomesha hapa?

Unajua kuwa nimebadilisha historia nzima ya uhuru na sasa wanafunzi wanasoma historia mpya ya TANU na historia mpya ya Julius Nyerere?

Unajua, unajua, unajua...
Huu ndiyo unaita, ''kuendekeza ujinga?''

Huu ndiyo unaita udini?

Wewe ulitaka mimi nikunje mikono wakati historia ya wazee wangu waliopigania uhuru wa Tanganyika inavurugwa kisa imejaa Waislam?

Nani sasa mdini kati yangu na hao?
Achana na hawa wanaotumia lugha za kuudhi ili kujenga hoja.

Tujirande uwanjani na hoja makini na tujengane kifikra.

Mimi nakupinga kwamba waliobatizwa walipaswa kutobadili majina.

Waliopigana Majimaji ni Watanzania na hawakusukumwa na Uislam ama Ukristo wao bali Uzalendo wao usio na chembe ya udini bali asili yao
 
Mzee wangu Mohamed Said.
Ama kwa hakika umesheheni historia muruwa ya nchi yetu.

Kuna mambo mengine ni muhimu kuyatafakari, kwa mfano jina Julias, Robert, Said, Hamad na fananio za hayo. Hayaleti taswira njema ya asili yetu ambayo tumetokana nayo. Tumepandikiziwa utu usio wetu ndo maana chembe za ubaguzi zinatutafuna kila kukicha.

Nilidhani unapambania kutaka kuondoa majina yasiyo ya asili mbele ya majina ya mashujaa wetu. Kumbe unataka kuyaswitch kwa muelekeo wa kibaguzi.

Turudi katika asili yetu bila kuathiri imani zetu
Msanii,
Ninachoeleza ni kuwa hawa wazalendo wengi wao walikuwa Waislam inasemekana 75%.

Baada ya kuhukumiwa kunyongwa wakati wanasubiri kifo ndiyo father kutoka Peramiho akaja kuwabatiza na kuwapa majina mapya ya Kikristo.

Haya ndiyo yaliyotendeka.
Mimi nasomesha yale yaliyotendeka ambayo wengi walikuwa hawayajui.

Ndiyo nikaeleza kuwa Songea Mbano jina lake khasa ni Abdulrauf Songea Mbano.
Mkomanile jina lake ni Khadija.

Haya ndiyo muhimu kwangu na nayaeleza kwa kuwa hayakuwa yanajulikana.
 
Back
Top Bottom