crabat
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 4,323
- 2,207
Kilwa
kipindi cha banu Umayya
huu ni utawala wa kwanza katika kipindi hichi baada ya makhalifa wanne utawala wa banu Ummayya ulianza na Muawiya bin Abuu sufiyan ulifuatiwa na yazid bin muawiyya 61-64 Hijiria sawa na mwaka 680-685 A.D, utawala huu haukuwa mzuri, kwani ulikuwa na upungufu mwingi;'
baadaye ulifuatiwa na uongozi wa Umar ibn Abdul-Aziz, ambaye alijaribu kurudisha hali ya kawaida katika katika dola yake na zile za mashariki ya kati na mashariki ya Mbali
Marwan wa pili au Abdul malik marwan, alikuwa ni mmoja katika utawala huu yeye ndiye aliyefanikiwa kuufikisha Uislam Hispania miaka ya 86-96 hijiria (705-715 A.D)
Hispamia ilipokuwa chini ya utawala wake, wakati huo ikiitwa Andalus, kulikuwa na migogoro mingi iliyosababisha ukoo wa Abbas kujitenga, Abuu Muslim alllifanikiwa kupata wafuasi wengi ambao walimuunga mkoono kwa kuwahamasisha juu ya kile kilichofahamika (Ahlul Bayt.) ukoo unaotokana na Mtume ndio bora katika uongozi Mwishowe walipigana kati ya banu Umayya na Banu Abbas
banu Umayya wakashindwa watu wakamchoguwa Abuu abbas kuwa ni kiongozi wao na huo ndio ukawa Mwanzo wa utawala wa banu Abbas Mnamo mwaka 750 A.D
Kutokana na migogoro ya banu Abbas na Umayya Waislam wengi walimiminika kuingia Pwani ya Azania Mgogoro wa mwaka 750 ndio uliomsukuma Mtoto wa aliyekuwa Mtawala wa tatu, Marwan wa pili au Abdulmaliki ibn marwan akiitwa Hamza ibn abdul maliki ibn Marwan, afike katika visiwa vya Kilwa,;
Maelezo yanasema
Mtu mmoja jina lake Hamza alikuwa katika hao wa kwanza waliofika wakati huo hamza alikuwa mwanawe Abdul maliki aliyekuwa Khalifa aliyetawala kutoka Mwaka 65 Hijiria hadi 86 Hijiria Hamza ndiye aliyeleta Ustarabu
katika mwaka 755, kundi la Amu said, kizazi chenye mnasaba na sayyidna Ally kiliingia Somalia Mwaka 120 Hijiria (740 A.D), Zaid mjukuu wa hussein bin ali bin Abuu talib (r,a), aliingia katika mgogoro wa Uongozi na baadaye kuuwawa katika ya mwaka 724 hadi 743.)
Wafuasi wa Zaid Amu said wanaotoka kusini mwa Arabu, waliingia katika mwambao wa Afrika mashariki kisha wakaoleana na wasomali, wakati huo eneo la somalia linaitwa Afica ya kati kabla ya mkutano wa Berlin, wa kuligawa bara la Africa (Berlin Conference of 1884-feb 1885)
KIzazi hicho chenye nasaba moja kwa moja na Sayyid na Ally bin Abuu talib (R.A) Kilianzisha Diwani ya kwanza Ruga Vumba kuu na Vumba ndogo Wasin ikiongozwa na Ahmed bin hussein wa ukoo wa ba-Alui pia kizazi cha Abuubbbbakar bin Sheikh, ambaye alikuwa Mtawala wa vumba kubwa na vumba ndogo
kwa mujibu wa silsila ya viongozi wa mwambao huu utaona imeanzia kwa Ally bin Abuu Twalib na bibi Fatma (r.a) Sayyid hussein sayyid zeina el-Abidina ali, sayyid muhammad el-bakir,sayyid jafir sadiq,sayyid ali al harith, sayyid muhammad, sayyid issa, sayyid AHMED NA SAYYID Abdullah.
Silsila HIYO INAENDELEA KWA SAYYID Alui, ambaye kwake yeye huyu Bwana ukoo wa bani Alawi au Ba Alawi unapata mzizi wake
Ukoo huo umekwenda moja kwa moja mpaka kwa sayyid ABUUBAKAR MASELA el- Ba-alawi., ambaye ni mmoja katika ya hao ndugu wa mwanzo kuja Africa ya mashariki na kutoka kwa huyu kizazi kiliendelea mpaka kwa Shekh Abuubakar DIwani wa Ruga
Utaona kwemba katika mwambao wote wa somali mombasa Zanzibar pate, lamu na sofala zipo koo hizi za Ba-Alawi ba -Urri, na ba- Amir,
pamoja na makundi mengine ndugu saba wa Al-haswa wakaingia ndani ya Somalia katika mwaka 295 Hijiria (908 AD), Wakati wa mtawala wa Oman aitwaye El- wawari Bin matrash Ndugu hawa saba wakiwa na majahazi matatu walifika Mogadishu wakitokea Al-Haswa katika Pwani ya Oman katika kabila la El Azd
Mnamo mwaka 975 A.D, hassan bin Ally akiwa na majahazi saba kutoka Shirazi aliingia Kilwa yeye mweenyewe akabaki Kilwa kisiwani kisha jahazi lingine likiongozwa na mwanae aitwae Muhammad lilielekezwa Mombasa ' Mwingine aitwae Bashati alilielekeza jahazi lake nchi ya kua (Mafia) na aliyeitwa suleyman yeye alielekea pate na aliyeitwa Hussain alielekea Zanzibar, wakati watoto wake Daudi na Ali mmoja alikwenda Kismayu Somalia na mwingine akaenda (Visiwa vya Qamar Comoro)
hata hivyo G.S.P.Feeman Grenville akimnukuu Shekh Muhyidiin anasemakuwa yalikuwa majahazi saba jahazi la kwanza lilikwenda mandakh la pili lilikwenda Shungu la tatu lilikwenda katika mji uliitwa yanbu la nne lilikwenda mombasa na la tano lilikwenda katika kisiwa cha Kijani Pemba ) jahazi la sita lilikwenda katika nchi ya kilwa na la saba Hanzuani (morocco)
kwa upande wake Hassan bin Ally alipofika kilwa aliitamani sana sehemu hiyo na kuone pana manzari nzuri hapaja jengwa akaenda kumuona mtu mmaja aliyeitwa Muriri wa bari Ambaye alikuwa ni Muislam'
Huyo akampeleka kwa kiongozi wa eneo hilo la Mrima ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Bwana Kilwa Abdallah ibin Kilwa ambaye jina lake limenasibiswa na jina la mji wa KiLWA 'Hassan bin Ally alipewa sehemu ya Ardhi ya KIsiwa na huyu bwana kilwa baadaye alikuja kuwa kiongozi wa hapo
baada ya utawala wa Hassan bin ally baadaye aliitawala kilwa mwanaye ally bin hassan, amdaye yeye ndiye aliyeitanuwa dola ya Kilwa na kuwa kubwa na yenye umaarufu mkubwa katika pembe zote za Dunia wakati huo
......Ndipo sultan Ally alipoanza kueneza utawala wake tena alijitahidi akatanua biashara ya dhahabu iliyokuwa ikitoka sofala kwenda Mogadishu'
kwa ufupi wa maneno Utawala huu wa dola ya kilwa ukawa wa kitajiri na kutikisha dunia kwa wakati huo''
Walter rodney mwanahistoria mashuhuri anasema Africa ilistaarabika kupitia Uislam kabla Mzungu wa kwanza hajakanyaga mguu wake barani Africa
mataifa mbalimbali yalishuhudia maendeleo makubwa ya kilwa kupitia harakati mbalimbali za kimaendeleo hasa kuwanzia mwaka 1300 A.D, WAKATI HUO IKIWA CHANI YA ABDUL muzhafar hassan mjukuu wa mtawala wa mwanzo hassan bin ally ibin batuta anasema-
wakati nilipofika kilwa nilimkuta mtawala wake aliyekuwa anaitwa abu mudhaffar hassan akiifahamika kwa jina na Abul mawahib,
na hii ilitokana na wingi wa maajabu na ukarimu usio kifani
HiSTORIA inazidi kufichuwa zaidi kuwa Waislam wa kilwa walitumia baadhi ya nali zao kuimarisha miji yao badala ya ujenzi wa matope na miti waislamu hao ndio waliokuwa wa mwanzo kutumia mawe yaliyochanganywa na saruji na chokaa iliyotokana na matumbawe
kazi hiyo ya ujenzi ilikuwa bora kuliko ujenzi ule wa matope uliotumika hapo kabla ambayo majengo yake yame sababisha kupotea'
Dola ya kilwa ilikuwa na muundo wa kikee ulioendana na hali halisi ya wakati huo Kimaendeleo kiuchumi kitaaluma na kijaografia makao makuu ya dola hii yalikuwa kaole Bagamoyo lakini Ofisi zake kuu za utendaji zilikuwa Kilwa Kisiwani katika Ikulu ndogo na kubwa zikifahaamika kwa jina la Husuni kubwa na ndogo husuni kubwa ilijengwa karne ya 14, chini ya utawala wa Al hassan ibn suleyman ndani ya jiji la kilwa Kisiwani Jengo hili lilitumika mpaka mwaka 1843 baada ya mtawala wa mwisho kukimbilia Muscat nchini Oman
ikulu hiyo limetuama katika sehemu ya muinuko ikiitazama bahari ya hindi kwa upande wa mashariki mlango wa kilwa ulielekea upande wa kaskazini na jiji lenyewe la kilwa likibaki upande wa magharibi''
jengo hilo la kuvutia ambalo halijawahi kujengwa mfano wake kusini mwa jangwa kuu la sahara kabla ya karne ya 18 kipindi hicho jengo linakusanya zaidi ya vyomba 100, ambavyo vilitumika kama ofisi mbalimbali za ikulu kama taasisi
Eneo la kusini la jengo hili limegawanyika katika sehemu 'mbili yaani ile ya chini ya juu
sehemu ya chini ina ukubwa wa mita za mraba 2,116 na ina vyumba vya ofisi 38 kila upande ulikuwa na vyumba viwili katika ya vinne vyaenye kufanana
sehemu ya juu ya jengo hili ni enneo lenye vyumba vya ofisi na naeneo maalum kwa ajili ya wageni na wanadiplomasia
kusini magharibi ya eneo hili kulitengwa kwa ajili ya shughuli mbali muhimu kwanza zilijengwa nyumba za viongozi pili zilijengwa ofisi za kodi ya mapato na jirani na nyumba hiyo kulikuwa na kisima kirefu cha ukubwa wa mita 4.6 cha maji kileo leta maji ya kutosha
Upande wa maghribi ya ikulu hii ulikuwa na ukumbi mkubwa wa mkutano wenye mita za mraba 195.pia kulikuwa na ukumbi wa pili mdogo wa mikutano kwa ajili ya wageni maalum Upande wa kaskazini mashariki ya ukumbi huu kuna mabafu ya kuogea eneo hili lina ukubwa wa mita 13 lenye pembe sita kona zake za pembe tatu zina viti maalum vya kukalia muogaji na ngazi za kushukia !
kweli uongozi wa kiadilifu uliweza kuibadilisha africa na ikawa nchi tajiri duniani na kutajika' kote ulimwenguni)
........Inshaallah Tutaendelea.