Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

Kwa mfano tukikubaliana na hizi makala makala zinazotolewa na waisilamu siku za hivi karibuni, nini kitabadilika? Mimi nadhani hizi makala huenda ni sehemu ya syllabus za mafunzo yanayotolewa na vikundi vya waisilamu vinavyokutwa misituni, kama kile cha Mtwara, mapango ya Amboni na hivi karibuni watoto wa kule Moshi. Naliunga mkono jeshi la polisi katika juhudi za kupambana na vikundi hivi, ikibidi hata kutumia risasi za moto kichwani ili watu tubaki na amani.

cc: Waandishi wa makala za kichochezi

 
Mleta mada ni mtenganishi. Nadhani unafurahia yafanywayo na bokoharam, alshabab, isis. Unakwama wapi katika kuendeleza maisha yako, familia yako na jamii inayokuzunguka: kielimu, kiuchumi na kijamii.
 
Kwa hiyo unataka kutuambia Quran imefundisha vita kwa kutumia mbinu ya maji kama sio kwanini tusiite vita vya imani za kishirikina.Unajua ndugu yangu ugonjwa wa kufuata hadithi za Mohamed Said kumeharibu akili za watanzania wengi sana hasa wakaazi wa Pwani ya Tanzania na maeneo ya Kariako.

Ngongo,

Mimi si mpiga hadithi.

Mimi ni mwandishi na nina heshima yangu katika midani ya utafiti.
Naamini nilishakuwekea hapa siku zilizopita vitabu na paper zangu.

Vitabu vilivyochapwa na wachapaji bingwa duniani na paper nilizotoa
katika vyuo tofauti ndani na nje ya Tanzania.

Lakini tuna msemo Waswahili tunasema: "Akutukanae hakuchagulii tusi."

Hii picha ni ya juma liliopita.
Niko na Prof. Mohamed Bakari wa Fatih University, Istanbul.

Haiyumkini kuwa nilkwenda kote huko kwenda kuwasikilizisha hadithi:


2015%2B-%2B1


Ngongo,
Utapata tabu sana na mimi.
 
Atapata tabu na wewe kwa kuwa umekwenda hadi Istanbul tena ukapiga picha na prof Mohamed Bakari, naye ukamsomesha hizo hadithi? ???????

Ninaona utasumbuka sana wewe kuwashawishi watu juu ya uelewa wako hata kama unaweka picha ulizopiga na kina wasira n.k, kwa sababu hakuna mtu duniani anajali unapigaga picha na nani hadi aelewe kwamba unafahamu.

Unaweza kulazimisha hoja masikioni mwa watu lakini kinachoingia akilini na moyoni, huna uwezo wa kukifahamu tu richa ya kukicontrol.

Ehhhe, leta picha zingine ulizopiga na sadamu hussein!.



Ngongo,

Mimi si mpiga hadithi.

Mimi ni mwandishi na nina heshima yangu katika midani ya utafiti.
Naamini nilishakuwekea hapa siku zilizopita vitabu na paper zangu.

Vitabu vilivyochapwa na wachapaji bingwa duniani na paper nilizotoa
katika vyuo tofauti ndani na nje ya Tanzania.

Lakini tuna msemo Waswahili tunasema: "Akutukanae hakuchagulii tusi."

Hii picha ni ya juma liliopita.
Niko na Prof. Mohamed Bakari wa Fatih University, Istanbul.

Haiyumkini kuwa nilkwenda kote huko kwenda kuwasikilizisha hadithi:


2015%2B-%2B1


Ngongo,
Utapata tabu sana na mimi.
 
Unajua ndugu zanguni waislamu punguzeni Umwinyi pigeni kazi. Mnaniaibisha kwa kuleta story za kuchezea bao au kunywea kahawa juzi kati kuna jamaa anadai mababu zake tu ndo walioleta uhuru. Sawa hata kama ni kweli itatusaidiaje ? Historia itumike tu kutuoa mwongozo mbele tunaendaje. Kama tuengeagalia history kwa jinsi wazungu walivyoendelea na sio tulivyoteswa na kudumaza kwa case study ya hapa hapa nyumbani tungekuwa mbali sana. Miaka ya 50 na 60 tulikua sawa na Singapore, China tuliwazidi Uturuki leo hizi nchi ziko wapi ?
 
Tabby,
Umeingia mjadala katikati na ndiyo maana ukawa hujui mantiki wala historia ya mimi kuweka picha.

Umefanya haraka labda ungesubiri Ngongo mwenyewe anijibu ungeelewa.

Nimeanza na picha niko BBC Studio za Glasgow nafanya kipindi cha historia ya Africa.

Ikaja picha niko Berlin, Zentrum Moderner Orient namalizia kuandika kitabu.

Kisha Geneva United Nations.

Halafu London Tower Bridge.

Na Prof. Ali Mazrui Nile Hilton, Kampala.

Nyingine Harlem, New York....nk. nk.

Nyingine Capitol Hill Washington. ..

Mimi sikukulazimisha kunijibu...

Umeingia kwangu kwa kutaka mwenyewe. ..

Nilisahau picha nyingine Library of Congress, Washington. ..

Hayo ya Sadam ni hamaki zako.
Pole sana.

Sioni sababu ya mie kujibu kejeli.

Naamini ushanifahamu.
Ukipenda kunijua zaidi ingia hapa: www.mohammedsaid.com
 
Mohamed Said naona umekuja kivingine. Lakini hata ile gharika ya Nuhu ilikuwa ni vita kati ya waislamu na Nuhu. Waislamu wakafunikwa na maji na nuhu akasepa. Yale maji ya gharika yalitumika kuwabatiza kwa nguvu Bahati mbaya nuhu alisahau kufunga bomba hivyo wakazama. Kwa kifupi ujinga wa dini ukizidi watu wanakuwa hovyo
 
Historia zingine lengo lake huwa ni kuleta chuki tu miongoni mwa wana jamii waliostarabika
Mimi nikuombe ndugu yangu albuluushiy kwamba yote yaliyotokea wakati huo ni ya kuhadithiwa tu na hakuna awaye yeyote ambaye yupo hai kwa sasa kuthibitisha maelezo haya. Lakini kubwa kuliko yote historia hii inajenga chuki kati ya uislam na ukristo na na hivyo basi ni vema jambo hili likaachwa lipite kama ambavyo lilikwisha pita

Majini ya kiislamu bila chuki yataishije? Jihad itapiganwaje? Na ujinga utakumbatiwaje?
 
Last edited by a moderator:
27 / 2/ 1906, Vita vya Majimaji ni vita vilivyopiganwa na wazee wa kiislamu kupinga utawala wa kimabavu wa Kijerumani, lakini kwa makusudi vita hivi historia yake imechafuliwa kwa makusudi kuonesha kuwa vilikuwa vita vilivyopiganwa kwa imani za kishirikina.

Ikumbukwe kuwa kusini mwa Tanzania kuna mkoa unaitwa Lindi, ambapo ndani ya mkoa wa Lindi kuna wilaya inaitwa Kilwa ambapo hapo mwanzo ilikuwa ni dola kamili ya Kiislamu iliyokuwa na utawala kamili na kutumia pesa yake na kuhukumu watu kwa mujibu wa dini ya Kiislam, ambapo kanda yote ya kusini mwa Tanzania walikuwa wanafuata mfumo wa kiislam.

Wajerumani walipoingia walikuta Makadhi na watu wote wakiwa katika imani ya Kiislam huku maisha yakienda bila matatizo yoyote, Wajerumani wakaanza na kufanya mambo ambayo hayakukubalika katika jamii kwa kulazimisha ili malengo yao yafikiwe, maafisa na askari walikuwa wanatembea na rozari na kulazimisha watu kuwa Wakristo kinguvu, baadhi ya maaskari walibaka wanawake wa kiislam ndani ya maboma yao na huko mashambani, hata waislam walipotaka kujua kwanini wake zao au mabinti zao wanabakwa, walijibiwa majibu ya karaha na dharau.

Ndipo chuki ilizidi kuwa juu ya Wajerumani, wazee wa kiislam waliwahimiza vijana wao kujiandaa kwa kujikomboa kutoka katika utawala wa kikafiri, wakisema wakati wa dola ya Kiislamu mambo haya hayakuwepo na iweje leo, ndipo kiongozi wa Wamatumbi aitwae Kinjeketile Ngwale aliwaongoza wapiganaji wa Kimatumbi kupambana na Wajerumani, wakati wote huo ukatili wa Ujerumani ulikuwa unajulikana kote kusini, wakati vita vinaanza na vilianza kwa nguvu kubwa, Wajerumani waliua kila walieona huenda ni adui yao, majeshi ya Ujerumani wakaanzisha kampeni kubwa kukamata kila waliemuona katika majumba ya ibada.

Kumbuka wakati huo nyumba za ibada ilikuwa ni Misikiti na kila wakati wa sala majeshi ya Ujerumani yalivamia misikiti na kumkamata kila waliemkuta humo, ndipo chifu wa Suleymaan Mamba wa kabila la Wamwera akatangaza vita kwa watu wake kuwa kila atakapoonekana Mjerumani akatwe kichwa, nae chifu Abdallah Chami wa kabila la Wangindo nae akatangaza vita rasmi kwa Wajerumani, nae chifu Mataka Ambunje wa kabila la Wayao nae akatangaza vita rasmi na Wajerumani, haikutosha nae Chifu Songea Rauf Mbano wa kabila la Wangoni nae akatangaza vita Wajerumani, na hapo makabila matani makubwa Kanda ya Kusini wakawa wanapigana na Wajerumani, na baadhi ya makabila madogo madogo nayo yakawa yanapigana kuwasaidia ndugu zao dhidi ya Majeshi dhalimu ya Ujerumani.

Makabila hayo ni kama Wandendeule, Wamatengo, Wambunga, Wandamba n.k. Wapiganaji wa vita hivyo mnamo tarehe 5/8/1905 walivamia misheni ya Kanisa Katoliki huko Nachingwea na kufanya shambulio la kustukiza na kuua makumi ya wanajeshi wa Ujerumani na kumuua Askofu Cassian Speis ambae huyu ndio alikuwa Askofu wa kwanza Dar es salaam.

Na mnamo tarehe 14/8/1905 wapiganaji hodari walivamia boma la Mjerumani na kufanya uharibifu mkubwa hali iliyopelekea mapigano makali yalioacha majeruhi na maiti kila upande, wapiganaji wengi walikuwa wanatumia mishale, mikuki, mundu, silaha za jadi na bunduki kadhaaa walitoka baada ya kuwaua majeshi ya Ujerumani, na Mjerumani akitumia bunduki za moto na kupelekea majeshi ya wazalendo kuzidiwa nguvu na Mjerumani kushinda vita hivyo.

Ikumbukwe majeshi ya mjerumani walikuwa wanachoma majumba moto ili kuwakamata wanaume lakini waliokuwa wanaungua mpaka kufa walikuwa ni watoto na wanawake. Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi 67 walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea Makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona wakubwa wa kituo hicho.

Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko. Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo, na badala yake imewekwa karatasi nyingine ambayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudumu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka.

Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kijadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba.

Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33,34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni;

“Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa Majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi. ”Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka.

Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho. Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu. Tulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata.

Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo;

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k.

Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko? Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam. Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii. Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa Kisiwani, huko nikamkuta Mzungu wa Kifaransa akiandika historia ya Kilwa Kisiwani akiitwa Thiery, ameweka kambi na majenereta ya umeme, solar power na makompyuta. Kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni Misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale.

Kilwa Kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za Kiislaam katika mwambao wa Afrika Mashariki, ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah. Tuliposoma kazi ile ya Yule Thiery Mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa. Sikuwa na la kumfanya. Kizazi cha vijana wa Kiislaam hakitopata historia ya kweli ya Kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika Uislam wao.

Maisha yao ya kila siku, hawa wanajua ni nini hasa wamekifanya kwa wazee wetu, kuanzia kwa Chifu Kimweri mpaka Chifu Mkwawa, wanasema etia mejiua, ni nani anaweza kujiua mpaka kukin’goa kichwa chake jamani?!

Majeshi yaliyofanya mauaji dhidi ya wazee ni Major Johannes, Captain Mortz Merker, Luteni Spiegel, Staff Sajent Engalnd na wengineo!

Ewe Allah (S.W.T.), Wazidishie adhabu hao madhalimu wa Kijerumani, Amiiyn!

Ahsateni, Nakutakieni siku njema!

Swali chokonozi....

Kwa nini hakuna "Black Arabs"

Mkuu unamaanisha wakristo ndio wavivu wa kusoma?
 
Ukitaka kumfurahisha muislamu we mdanganye tu kwa kuisifia dini yake,mfano mwambie,hapa duniani magenius wa kiislam ni wengi kuliko wakristo..wallah kma ana binti yake atakupa .!!hawa jamaa hawawz beynd thr religion.

Hahaha...mkuu acha hizo bana!!! Hahaha
 
Hivi kabla ya kuja kwa wazungu wakoloni ni nani alianzisha biashara ya utumwa Afrika Mashariki? Ni nani alikuwa anawatoboa waafrika miguu na kuipenyeza minyororo?
-Ni nani alikuwa anawahasi waafrika ili wasizae na mabinti zao?

-Ni nani alianzisha usultan zanzibar?

-Lakini pia hayo mangome ya kilwa naa kwingineko unakozungumzia ni nani aliyoijenga?

-Na hiyo dini unayoitetea na kuiona ya haki uliletewa na nani? Kama wasingekuja waarabu je ungekuwa muislam? Hahaha...

Za kuambiwa/za kusoma.....changanya na zako, Sioni sababu ya kutengeneza mazingira ya udini kwa karne hii zaidi ya kufanya maendeleo zaidi.
 
Nemulo,
Ukitaka historia ya utumwa itabidi kwanza usome Transatlantic Trave Trade.

Unaijua?
 
Ukitaka kumfurahisha muislamu we mdanganye tu kwa kuisifia dini yake,mfano mwambie,hapa duniani magenius wa kiislam ni wengi kuliko wakristo..wallah kma ana binti yake atakupa .!!hawa jamaa hawawz beynd thr religion.

nimecheka sana mkuu
 
safi kwa makala nzuri, cku nyingine utuletee jinsi waafrika walivyoteswa na waarabu kwenye biashara ya utumwa
 
Mzee! Respect to you. You are a great man your achievement are so good.
It is said that kama hujui ulipotoka hutajua unapoenda, wewe ni msomi, sisi weusi it is obvious na kuna proofs nyingi msomi kama ww utakuwa ulikutana nazo tulikuwapo kabla hata ya hizi dini za walowezi kuingia, we were great men of kush we had our gods and we did built pyramids, mathematics, philosophy, governments and so many more.
Kwanini wasomi kama nyie mnazdi turudisha kwa slaves masters way of worship and mind slavery. You supposed to educate the masses abt the truth, muslim christianity etc hizi si dini za watu weusi si tamaduni zetu hizi.
Let us emancipate our selves from mental slavery.
 
Mzee! Respect to you. You are a great man your achievement are so good.
It is said that kama hujui ulipotoka hutajua unapoenda, wewe ni msomi, sisi weusi it is obvious na kuna proofs nyingi msomi kama ww utakuwa ulikutana nazo tulikuwapo kabla hata ya hizi dini za walowezi kuingia, we were great men of kush we had our gods and we did built pyramids, mathematics, philosophy, governments and so many more.
Kwanini wasomi kama nyie mnazdi turudisha kwa slaves masters way of worship and mind slavery. You supposed to educate the masses abt the truth, muslim christianity etc hizi si dini za watu weusi si tamaduni zetu hizi.
Let us emancipate our selves from mental slavery.

non but our selves will free our minds,
 
Back
Top Bottom