Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

Umemnukuu ustadh ILUNGA HASSAN KAPUNGU mwenyezi Mungu amrehemu
 
dindi...
Hakuna tatizo.
Nimeandika kueleza historia ya yale yaliyotokea katika Vita Vita Vya Maji Maji.
 
Maalim unapendekeza nini kifanyike?
Hayo majina hayawakilishi uislamu bali Uarabu.
Mr Q,
Unavyopenda kuamini si tatizo.
Mimi naeleza historia ya Maji Maji ilivyokuwa.

Waislam wamenyongwa na wakati kabla hawajanyongwa akafika father kutoka Peramiho kuwabatiza.

Hili likasababisha majina yao ya Kiislam ukipenda ya Kiarabu yafutwe.

Hakuna tatizo ndugu yangu.
Mimi niko hapa kusomesha historia ambayo si wengi mnaijua.
 
Hayo majina ni ya kiarabu sio ya kiislamu
Najua unajua shida ni udini wa kupindukia

Mzee ukiendekeza haya utakuwa mjinga
 
Hayo majina ni ya kiarabu sio ya kiislamu
Najua unajua shida ni udini wa kupindukia

Mzee ukiendekeza haya utakuwa mjinga
Panzi...
Kuendekeza, ''scholarship,'' toka lini iwe ujinga?
Sipendi kusema haya lakini kidogo umeniudhi.

Unajua nimeandika vitabu vingapi kuhusu somo hili ninalosomesha hapa?

Unajua nimealikwa vyuo vingapi ndani na nje ya mipaka yetu kueleza haya ninayosomesha hapa?

Unajua kuwa nimebadilisha historia nzima ya uhuru na sasa wanafunzi wanasoma historia mpya ya TANU na historia mpya ya Julius Nyerere?

Unajua, unajua, unajua...
Huu ndiyo unaita, ''kuendekeza ujinga?''

Huu ndiyo unaita udini?

Wewe ulitaka mimi nikunje mikono wakati historia ya wazee wangu waliopigania uhuru wa Tanganyika inavurugwa kisa imejaa Waislam?

Nani sasa mdini kati yangu na hao?
 
Masta...
Jaribu kunielewa ninachoeleza.
Sipiganii jina hapa.

Hawa watu wamepewa majina ambayo si yao tena kwa kutumia ghilba.
Hawa watu mashujaa wamepigana na watu waliovamia nchi yao kutoka Ujerumani.

Hawa wamenyanyua silaha dhidi ya adui.
Hawa watu walikuwa Waislam.

Katika wakati wao wa umauti ndiyo wanafanyiwa haya.
Wanaambiwa wanaambiwa wabadili dini zao au wauawe kwa kunyongwa.

Mbona wewe husemi lolote kuhusu hili?

Huyu father aliyetumwa kutoka Peramiho alikuja Mahenge kubadili historia za hawa wazalendo.

Kwa nini hili hutaki kuliona?
Au unadhani hawa Wazungu walikuwa na haki ya kufanya vile?
 
RO7...
Mada iliyopo mezani si hiyo.
Ikiwa unapenda tujadili hili fungua uzi mpya.
UJINGA na UDINI umekujaa wewe Mzee Mohamed Said

Kwahiyo pakifutwa Dominic na kuandikwa Abdulrahman ndio atafufuka au?

Ninyi Waarabu wenye nywele nyeusi na ngumu, Pua pana na lips pana mnashangaza sana.
 
Acha Uongo Mzee
 

Dominic nalo jina?



Kukuuuu [emoji239][emoji239][emoji239]
 
Mi nimekuelewa,Ila Tumuachie Allah!!
Kiokotee,
Hili la kusahihisha historia na kuandika ukweli hili aachiwi Allah.

Hili tunaliweza.

Hili mimi nimetaka msaada wa Allah na nimelifanya limekamilika kuliko mategemeo yangu.
 
Mzee wangu Mohamed Said.
Ama kwa hakika umesheheni historia muruwa ya nchi yetu.

Kuna mambo mengine ni muhimu kuyatafakari, kwa mfano jina Julias, Robert, Said, Hamad na fananio za hayo. Hayaleti taswira njema ya asili yetu ambayo tumetokana nayo. Tumepandikiziwa utu usio wetu ndo maana chembe za ubaguzi zinatutafuna kila kukicha.

Nilidhani unapambania kutaka kuondoa majina yasiyo ya asili mbele ya majina ya mashujaa wetu. Kumbe unataka kuyaswitch kwa muelekeo wa kibaguzi.

Turudi katika asili yetu bila kuathiri imani zetu
 
Je mtu akibatizwa ama kuslimu anakuwa hana haki ya kubadili jina lake?
 
Achana na hawa wanaotumia lugha za kuudhi ili kujenga hoja.

Tujirande uwanjani na hoja makini na tujengane kifikra.

Mimi nakupinga kwamba waliobatizwa walipaswa kutobadili majina.

Waliopigana Majimaji ni Watanzania na hawakusukumwa na Uislam ama Ukristo wao bali Uzalendo wao usio na chembe ya udini bali asili yao
 
Msanii,
Ninachoeleza ni kuwa hawa wazalendo wengi wao walikuwa Waislam inasemekana 75%.

Baada ya kuhukumiwa kunyongwa wakati wanasubiri kifo ndiyo father kutoka Peramiho akaja kuwabatiza na kuwapa majina mapya ya Kikristo.

Haya ndiyo yaliyotendeka.
Mimi nasomesha yale yaliyotendeka ambayo wengi walikuwa hawayajui.

Ndiyo nikaeleza kuwa Songea Mbano jina lake khasa ni Abdulrauf Songea Mbano.
Mkomanile jina lake ni Khadija.

Haya ndiyo muhimu kwangu na nayaeleza kwa kuwa hayakuwa yanajulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…