Dini zimeingiza wengi kuzimu na zinazidi kupeleka wengi kuzimu.Kutokusoma Biblia kumakuwa ni tatizo la wengi matokeo yake mmetengnezewa vijitabu vingine kwani mkiachwa msome Biblia mtaujua ukweli.Huu ushabiki wa dini bila kuchunguza utakupeleka Jehanamu ,unaweza zania unaiponya nafsi yako kumbe unaiangamiza.
Yesu alikuwa wazi kwa habari ya hizi dini alisema "mtawatambua kwa matunda yao".Leo anngalia wafuasi wa hizo zinazosemwa ni dini za Mungu,tabia zao zikoje na je maisha yao katika jamii yakoje?
Huko disco wanaoenda ni wapagani?Je vilabuni?Vipi fiesta nako wote ni wapagani?
Umekaa kwenye dini yako miaka kibao lakini haijakusaidia hata kuishinda dhambi ya kusema uongo.
Muda wa kujilisha upepo umeisha,wengi mnatetea dini zenu kwa sababu hazijawabana na wala haziwakemei kwa habari ya dhambi.Time will tell,kweli mtu unashindwa kujua dini yako ulaya wanafanya nini?na wakileta hayo mambo na huku africa utapona?Mwenye masikio na asikie.Hatuingii mbinguni kwa sababu ya dini,mbinguni vinaingia vilivyo vitakatifu.
Sasa naanza kumwelewe yule mtumishi aliyekutwa amelewa alisema "mambo mengine inategemea kanisa wamekubalianaje" akimanisha kanisa fulani wanaweza kukubaliana jambo fulani si dhambi ingawa kwa kanisa jingine ni dhambi.Hapo inaonyesha Mungu hana nafasi bali ni makubaliano ya wanadamu,wengine wamekubaliana kunywa pombe kidogo si dhambi.
Wana waupotevu sometime wanachekesha utawasikia "mimi nikinywa bia yangu,sijamtukana mtu naenda nyumbani nalala kwani nitakuwa nimetenda dhambi".Jameni tutumie akilizetu haya mwanamke mzinzi naye atasema "mimi nikizini,nikajisafisha nikarudi kwa mme wangu nikampatia haki yake,kwa sababu sijamtukana mtu wala kumwumiza nitakuwa nimefanya dhambi?".
Soma biblia,soma biblia,soma biblia kila siku.