Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

K
Kuna namna waeza tupa ushahid juu ya hili? Pia kama ni hivyo inamaana sote tunaabud cku ambazo ni mapokeo ya wanadam? Kama ndivyo je kuna mweny haki wa kumwambia mwenzake sabato ni cku flan?
Kalenda hii tunayoitumia inaitwa Gregorian calendar, waislamu Wana kalenda yao kila Jamii Ina kalenda yao, majira na nyakati zilibadilika
 
K
Kalenda hii tunayoitumia inaitwa Gregorian calendar, waislamu Wana kalenda yao kila Jamii Ina kalenda yao, majira na nyakati zilibadilika
Kwa minajili hiyo hakuna mwenye haki wa kumkosoa mwingine kua cku ya sabato ni ni cku flan!! Kwamaana sote twafate taratibu za kibinadan.
 
Soma Luka 23 kuanzia fungu la 50, soma Kwa makini ili uelewe siku ya Saba ni ipi na siku ya kwanza ya juma ni ipi Kwa mjibu wa biblia.

Soma Luka 23 kuanzia fungu la 50, soma Kwa makini ili uelewe siku ya Saba ni ipi na siku ya kwanza ya juma ni ipi Kwa mjibu wa biblia.
Luka 23:50 unazungumzia juu ya Yusuf mtu wa arimathaya kwenda kuuomba mwili wa kristo ili akauhifadhi. Na umezumgumzia juu ya maandalio ya siku ya sabato only that haijsema Sabato ni jmos au jpili. Nnachotaka mimi nipewe aya inayosema siku ya sabato ni juma flan. Pia unajua ni nan alizipa majina hizi siku tulizonazo? Ukitambua hilo bas jua siku ya sabato wanadam ndio tumejipangia iwe lini!! Na hakuna mwenye mamlaka ya kumkosoa mwingine kwa kuifanya sabato iwe cku flan.
 
Mnaabudu sanamu ya Maria na Yesu
Wakati Amri ya Kwanza imekataa hilo swala

Kama hamuoni yatosha mkaamua kuifuta hiyo amri
Amri yetu ya kwanza inasema msiabudu Miungu Mingine ....... if ya kwenu inasema msiabudu sanamu well msiabudu tuu hatuwaangilii
 
Na yeye atueleze why waliandamana hadi airpot kulazimisha waende ughaibuni kwa mserereko!
Kwa mujibu wa mafundisho ya Wasabato mwafrika mweusi haruhusiwi kwenda kuhubiri kwa wazungu ulaya ila wao wazungu ni ruksa kuja kuhubiri kwa waafrika😀😀😀ndiomana hao Wasabato wanaojiita Wasabato masalia walitaka kuipindisha hiyo sheria ndani ya Wasabato
 
Ukibishana na mjinga wenye busara watashindwa kupambanua mjinga ni yupi.Hapa mweledi ni Bora akawahubiria wafuasi wake badala ya kurusha madongo Kwa wahumini wasiokuwa wa dhehebu lake.
 
Soma biblia Luka 23:50 na kuendelea, soma Kwa makini. Biblia inasema yesu alifufuka cku ya kwanza ya juma.
Ambayo Kwa lunar calendar sio jumapili, fatilia PDF uone vizuri.
Wayahudi wa zamani hawakutumia Gregorian calendar walitumia lunar calendar,hakuna neno "Sunday" kwenye lunar calendar. Walitumia mwezi kama saa ya kujua siku, miezi na miaka
Imeandikwa
Zaburi 81:3
[3]Pigeni panda mwandamo wa mwezi,
Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
Blow up the trumpet in the new moon, in the time appointed, on our solemn feast day.
 
Hii elimu aliwahi nipa mtu mmoja kwa urefu sana nikabisha next time kuna mtu akanipa humu humu nikafatilia nikaanza kuielewa hadi walivyokuwa wana hesabu nikagundua mengi sana.
Wengi hawafahamu na kudanganywa na Waadventista wasabato na wayahudi wa Sasa wa kule Middle East ambao asilimia kubwa walikuwa assimilated Jews.
Na inashangaza Wasabato kupingana na Wakatoliki na wanatumia kalenda ileile ya Papa Gregory kuthibitisha mambo Yao badala ya kwenda kwenye Lunar calendar, Kalenda ya Mungu wa kweli.
 
Katekism hajasema hivyo. Katekism inamuagiza kila mmoja akamtangaze Kristo.

Pamoja na ukweli huo, kuna waliozama kwenye hiyo taaluma wanaweza kujibu kitaaluma. Vinginevyo utababaisha halafu waonekane washindi. Kuna waliosomea biblia, kuna waliosomea elimu Mungu. Wewe unafikiri Kila mmoja anaweza? Mimi Nina taaluma yangu na ukiigusa nitaijibu bila kubabaisha.
 
Usipoteze muda kubishana na mjinga. Kiimani unatakiwa kumwombea.

Paulo aliyekuwa kiongozi mkuu wa kulihujumu Kanisa la Kristo alikuja kuwa mtume wa Kristo aliyefanya kazi kubwa sana. Hata huyo unayemsema, usishangae siku nyingine akasimama mbele yako akikuhubira mafundishobya kweli kuliko hayo ya upotofu anayoyatoa sasa.

Ila kama wewe unayumba kwa sababu ya kutolijua neno la Mungu, jibidishe kuyajua maandiko:

Kwa ufupi kabisa, rejea hapa:

1) kwa nini Kristo aliuawa?
JIBU: Kwa sababu ya kutotii sheria.

2) Sheria gani
JIBU: Sheria ya Musa, yaani kumbukumbu la torati.

3) Sheria gani ilikuwa kuu kuliko zote kwenye kumbukumbu la torati?
JIBU: Sheria ya sabato

Yesu kutozingatia mafundisho ya mafarisayo kuhusiana na sabato, ndiyo mwanzo wa chuki za mafarisayo na makuhani dhidi ya Kristo. Tena wakasema wazi kuwa, kama angekuwa mwana wa Mungu angeitii Sabato. Naye akawaambia wazi kuwa yeye ni mkuu kuliko sabato. Yeye ni bwana wa Sabato. Kwa nini uiabudu siku ya Sabato badala ya kumwabudu yeye aliye bwana wa Sabato?

Kwa hiyo Kristo aliuawa kwa kutoitii sheria. Kwa kutoitii sheria za kumbukumbu la torati, ambako sheria kuu ni utii wa sabato. Kwa sababu kutokutii sabato lisingekuwa kosa kubwa la kuhukumiwa kifo na Pilato kiongozi mwakilishi wa mfalme wa Roma, wakamtengenezea kesi ya kubumba ya uchochezi kuwa anawachochea watu wasilipe kodi kwa mfalme Kaizari wa Roma.

Paulo anasema wazi Kristo alihukumiwa kwa sababu ya kutoitii sheria, akayashinda mauti. Baada ya ushindi wa Kristo yaani kuyashinda mauti, sisi tulioshinda na kufufuka na Kristo, tukirudi kuitumikia sheria, basi kifo cha Kristo ni bure.

Mkristo hustahili kuiabudu sabato, au kuiabudu siku, mwabudu Bwana wa Sabato katika kweli na haki.

Nakuelewa kwa kiasi fulani. Lkn lazima nichimbe kwa undani kama kosa la kutotii sabato pekee ndilo lililoleta kuvutana na wayahudi.
 
Sawa yeye ameongea hivyo na akaona yuko sahihi na mimi pia nataka nijue kutoka kwake,Hiyo Jumamosi anayosema ndio sabato kaitoa kwenye kalenda ipi?ya kirumi,ya waislam au wayahudi,kalenda kutoka mbinguni au(ambayo sidhani kama ipo),kalenda ya wamisri,wahindi n.k

Hizo ibada za sanamu katika ukatoliki ni zipi? maana nachojua sisi ibada yetu imekuwa ni misa ambayo hufanyika siku zote za wiki(Jumapili ikiwa ni siku ambayo waumini ufika kwa namba kubwa kanisani).Ibada hii ya misa imegawanyika sehemu kuu mbili:Liturijia ya neno na liturijia ya ekaristi(sasa hapa sanamu ni lipi linaloabudiwa?)

Pale mnapoenda kuziinamia na kuzibusu sanamu kwenye majengo yenu ya ibada, ndiyo shida inapoanzia.
 
Kwanza ungeuliza kwa nini kwenye mkutano au mahakama unaonyesha heshima kwa kuinama kama wakatoliki,
Pili jiulize kwa nini kila nembo ya hospitali ina sanamu ya nyokaView attachment 2582168

Lkn si unajua kwamba baada ya kuona wameanza kumuabudu akaambiwa amtoe. Lkn hata maiti yake Musa alipokufa, haikuzikwa kama kawaida. Kuzuia watu wasiabudu kaburi lake.
 
JE WAKATOLIKI TUNAABUDU MSALABA?
Kabla sijajibu swali la Msingi naomba nitoe utangulizi kidogo

Kwa hulka yake binadamu ni kiumbe ambaye ana tabia ya ku imagine karibu kila kitu ambacho anakiwaza au kukisikia na huwa anajaribu kutengeneza picha Fulani ya kitu hicho, kwa mfano mtu anaposikia jina la mtu Fulani ambaye hajawahi kumuona…… kwanza kabisa atatengeneza picha Fulani labda huyo jamaa ni mrefu, Mnene na kadhalika, na siku akimuona utamsikia akisema ‘aaaaa kumbe yupo hivi mimi nilifikiri yupo vile’

Hii ni hulka ya binadamu yeyote yule na hata kuhusu Mungu tunayehubiriwa na kwa kuwa hatujawahi kumona , nina hakika kila mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu yupo anapata picha Fulani ya Jinsi Mungu alivyo, na hiyo picha ni Tofauti kwa kila binadamu, picha hapa simaanishi uwezo wa Mungu kwa kuwa uwezo wa Mungu tunaweeza kuu feel ( hisi)kutokana na mambo ambayo anayatenda kwenye Maisha yetu ya kila siku.

Au pia mtu akisikia jina au habari za mji fulani kwa mfano SONGEA, kwa yule ambaye hajawahi kufika songea ni lazima atapata picha Fulani kichwani mwake, Kwmba ni Lazima kutakuwa na barabara za Vumbi kila sehemu, kuna wanaume weupe tu kama Mapunda N.K sasa siku akifika songea na kukuta kuna Rami barabara na mitaa yote ‘’ aaaaa Kumbe ndiyo kulivyo’Mimi nilifikiri papo vile.aaa kumbe kuna wanaume Weusi N.K

Sasa hizo picha zote kwa namna yoyote ile hazichukui Nafasi ya hivyo vitu kwa uhalisia wake, Miji, au watu husika, Ingawa zinawakilisha vitu hivyo kwa binadamu husika. Na hata picha za mnato kwa mfano hazichukui Nafasi ya mtu husika, kwani mtu husika anabaki kama alivyo na picha yake inabakia kama kiwakilishi tu cha muhusika.

Leo hii hatuwezi kuchukua picha ya mchazeji kama Fiston Mayele na kusema huyu ndiyo Mayele halisi.
SASA NAENDELEA NA SWALI NA MAJIBU YA MSINGI.
Jibu la Msingi ni HAPANA. Nitaeleza ni kwanini nasema wakatoliki hatuabuu sanamu, na labda tujiulize kwanza maswali yafuatayo ;
1.Je Mungu anachukia Kila sanamu ?
Jibu lake ni kwamba HAPANA, Mungu hachukii kila sanamu kwani hata yeye mwenyewe katika nafasi mbalimbali aliwahi kuagiza matumizi ya sanamu, nitakupeni mifano michache katika mingi, Katika agano la Kale tunaona kwamba Mungu alimuagiza Musa akatengeneze sanamu na kuziweka mahali ambapo Mungu atakuwa anazungumza naye na kumpa maagizo mbalimbali, tunasoma hilo katika kitabu cha kutoka 25 :10-22.

Pia kama mnakumbuka wakati wana waisrael walipokuwa Jangwani na baada ya kumnung ‘unikia Mungu,naye aliwaadhibu kwa kuwaletea nyoka wenye sumu waliwauma na watu wengi walikufa. Lakini baada ya Musa kuwaombea mshamaha kwa Mungu Naye Mungu alimuagiza atengeneze Nyoka wa shaba na kumtundika juu ya mti, na kila aliyeng’atwa na wale nyoka wenye sumu alipokwenda kumtazama yule nyoka wa shaba alipona baada ya kufanya hivyo( Hesabu 21 :4-9) sasa hapo tunaweza kujifunza kwamba aliyekuwa anaponya watu siyo ile Sanamu ya nyoka badala yake ni Mungu mwenyewe alikuwa anawaponya.

2.Je ni sanamu gani /zipi zinamchukiza Mungu
Mungu anachukia kila aina ya Sanamu ambayo inachukua nafasi yake, hapo namaanisha kila aina ya sanamu inayoabudiwa kama ndiyo Mungu mwenyewe , hiyo inamchukiza Mungu, Kwani Mungu yupo peke yake na kila kitu kinachochukua nafasi yake kuwa ndio Mungu anakichukia,kama mnakumbuka katika kitabu cha kutoka tunasoma kwamba wakati Musa alipokuwa mlimani sinai kupokea Amri za Mungu, alikaa huko kwa muda mrefu sana na waisrael imani ikawatoka, kiasi kwamba wakaamua kujitengenezea sanamu na kusema kwamba hiyo sanamu ya Ngo’mbe ndiyo Mungu wao aliyewatoa Misri na ndiye atakayewaongoza huko waendako.

Hivyo hii sanamu ni Lazima imchukize Mungu kwa kuwa inachukua nafasi ya Mungu, na siyo kwamba anawakilisha uwepo wa Mungu wa Kweli.Nenda kasome kitabu cha kutoka sur aya 32, isome yote.

3.Pia Mungu anakataza sanamu na kuziabudu na kuzitumikia, hapo ni sawa na kusema sanamu zimechukua nafasi ya Mungu. Hivyo sanamu zinakatazwa kama zinaabudiwa na kutukuzwa na kutumikiwa kama walivyofanya waisrael kama yule ndama, walimfanya kuwa ndiyo Mungu wao na walikuwa tayari kumuabudu na kumtumikia. Kwa kushindilia hoja hii soma kitabu cha kumbukumbu la Torati 4 :15 – 20)

4.Wakatoliki hatifanyi nini ?

Wakatoliki hatuabudu sanamu na kwa kuwa hakuna siku wala mahala ambapo tumewahi kufanya wala kusema hizi sanamu ndiyo Mungu wetu na kwamba tunaziabudu au tutaziabudu na kuzitii na kuzitumikia, hatujawahi kufanya hivyo na sidhani kama itatokea.

Tunaamini kwa Mungu Mmoja kama tunavyosali katika kanuni ya Imani yetu, na hakuna sanamu hata moja iliyowahi kupewa heshima kama hiyo.
NARUDIA TENA KWAMBA HATUFANYI KAMA WALIVYOFANYA WAISRAEL KULE JANGWANI KWA ILE SANAMU YA NDAMA.NDIYO KUSEMA HATUABUDU SANAMU.

5.Ijumaa kuu wakatoliki tunafanya nini ?
Katika Ibada ya ijumaa kuu kuna kipengele kinaitwa cha kuheshimu Msalaba.Mara nyingi huwa unatumika msamiati kuabudu msalaba.Lakini je kinachofanyika pale ni kitu gani hasa ? kwa mtu anayefuatilia vyema ibada hiyo atakumbuka kwamba kabla ya zoezi la kubusu msalaba halijaanza kiongozi wa ibada husema mara tatu maneno yafuatayo ‘’ HUU NI MTI WA MSALABA, AMBAO WOKOVU WA ULIMWENGU UMETUNDIKWA JUU YAKE’ na watu wote tunaitikia/ tunajibu ‘’ NJOONI, NJOONI, NJOOONI TUUABUDU’.
Sasa hapo kama kweli umeelewa tunachoabudu ninini ? mti wa msalaba au uokovu uliotundikwa juu yake ? Sasa wataalamu wa theologia wanatueleza kuwa tunaabudu wokovu juu ya msalaba, kwani kwa kufanya hivyo siyo kwa sababu ya ule msalaba, kwani kama kufa msalabani hata wakosaji wote katika jamii ya kiyahudi waliuawa kwa kutundikwa msalabani.

Hivyo basi tuna alikwa kuabudu wokovu uliotundikwa juu ya msalaba, na huo wokovu ninini basi ? Jibu ni YESU KRISTU na huyu Yesu Kristu ni nani ? katika katekisimu katoliki tunaambiwa kwamba Yesu Kristu ni Nafsi ya pili ya Mungu na ni Mungu sawa na Baba, hivyo kusema Yesu ni Mungu, na wokovu wetu ni Mungu ndiyo kusema TUNAMUABUDU MUNGU.

Na kwa wale ambao hawajawahi kuwa makini sehemu hii ya ibada ya ijumaa kuu nawaalika kuwa makini katika ibada ya mwaka huu na wale ambao wanasema kwamba ijumaa tunaabudu sanamu nao nawaalika wakafuatilie kipengele hiki vizuri. Ni hapo tu watapata majibu ya maswali yao na mashaka yao yatakwisha.

Na kuna wakati watani zetu huwa wanasema kwanini sisi wakatoliki tunaweka picha ya mtu katika misalaba yetu. Sisi huwa tunaweka picha ya Yesu katika misalaba yetu. Hao wanaouliza hivyo nao pia wanatumia misalaba lakini haina hiyo picha kwakuwa wanasema kwa kufanya hivyo watakuwa wanaabudu sanamu, lakini picha ya msalaba kwao siyo tatizo.

Hapo napenda kuwaeleza kwamba kuwa sisi wakatoliki tumeona kuwa na picha ya msalaba haitoshi kwani kitu muhimu ni kupata picha halisi ya Jinsi Yesu alivyokufa Msalabani, ndiyo maana tunaongeza na mtu pale msalabani.Kitu cha muhimu hapo ni msalaba wa Yesu na siyo tu msalaba PEKE YAKE .

Kwani msalaba ulioleta wokovu ni msalaba wa Yesu tu,kama suala lingekuwa ni msalaba tu kwani hata wale wanyanganyi waliuawa msalabani, na misalaba yao haikuleta wokovu kwa dunia.Ndiyo maana tunajazia na hiyo kitu ili kutoa picha halisi ya Yesu msalabani kusudi tunapoutazama msalaba wa Yesu tupate picha halisi ya kifo chake msalabani.

Bada ya kusema hayo basi naamini utakuwa ume imarika kiimani na hakuna mtu atakubabaisha juu ya hili suala la msalaba na masakramenti yote na tuwaeleweshe wale ambao hawaelewi kwa upendo na utulivu mantiki na liturujia nzima ya uwapo wa sanamu kwa wakatoliki
Shukrani sana kwa elimu mkuu
 
Chief, nakubaliana nawe. Ila Kuna mafundisho yao mengine wanaamini siku ya mwisho kanisa la roman catholic wataungana na USA kuwatesa wasabato kwa kuwalazimisha kusali jumapili. Msingi. Wa mafundisho yao nikulishambulia kanisa katoliki
Nimewahi kusikia hayo mafundisho, yao, halafu nashangaa na waumini wao wanaamini. Mara waseme namba 666 au 616 iliyokuwa ikimaanisha mfalme Kaisar Nero, kuwa eti ni papa.

Nadhani wanazidi kulichokonoa Kanisa Katoliki baada ya kuona huo unabii wao wa Kanisa Katoliki kuwalazimisha kusali Jumapili, hautimii.

Walisema mwisho wa Dunia utakuwa mwaka 1844, haikuwa.

Wamesema Kanisa Katoliki litawalazimisha wasabato kusali Jumapili, haijatokea na hata dalili tu hazipo.

Mungu atazidi kuwaumbua wenye mafundisho ya uwongo siku zote.
 
Niwaombe sana, wewe mleta mada na wachangiaji baadhi.... Muachane na hii mada chonganishi katika masuala ya dini ambayo ninyi wote mnaonekana kutoijua kwa undani wake. Waachieni Wanazuoni/ wasomi wa biblia (Maaskofu na Wachungaji) ambao wanafundisha waumini wao makanisani kwa upendo na upole. Zaidi sana someni biblia na muende kwenye Ibada mara kwa mara huko mtakutana na ROHO wa Mungu atakayewafundisha kuijua kweli nayo kweli itawaweka huru.
 
Nakuelewa kwa kiasi fulani. Lkn lazima nichimbe kwa undani kama kosa la kutotii sabato pekee ndilo lililoleta kuvutana na wayahudi.
Nakutakia shule njema. Kutotii sheria za siku ya Sabato ndiyo ulikuwa mwanzo wa Yesu kukataliwa na Mafarisayo, Wanasheria na Makuhani.

The growing rejection of the Pharisees, who earlier had been friendly to Jesus, becomes apparent in this chapter. First, there are three incidents relating to the Sabbath, in which Jesus is accused of breaking the Mosaic law (Mt 12:1-21); second, Jesus’ power is attributed to the devil (vv. 22-37); third, the Pharisees demand a sign other than miracles (vv. 38-50).

The opening incident tells how the disciples, walking through the green fields on the Sabbath, began to pluck ears of grain and eat them because they were hungry. Mark 2:23-28 and Luke 6:1-5 also record the story. The Pharisees, on the alert for any ground of accusation of Jesus and His disciples, immediately accused them of doing that which is not lawful to do on the Sabbath. As Morgan points out, the hostility of the Pharisees began when Christ forgave sin (Mt 9:1-8), was increased by Jesus’ associating with publicans and sinners (vv. 9-13), and now is inflamed by Christ’s ignoring their petty rules about the Sabbath.57
 
Back
Top Bottom