JE WAKATOLIKI TUNAABUDU MSALABA?
Kabla sijajibu swali la Msingi naomba nitoe utangulizi kidogo
Kwa hulka yake binadamu ni kiumbe ambaye ana tabia ya ku imagine karibu kila kitu ambacho anakiwaza au kukisikia na huwa anajaribu kutengeneza picha Fulani ya kitu hicho, kwa mfano mtu anaposikia jina la mtu Fulani ambaye hajawahi kumuona…… kwanza kabisa atatengeneza picha Fulani labda huyo jamaa ni mrefu, Mnene na kadhalika, na siku akimuona utamsikia akisema ‘aaaaa kumbe yupo hivi mimi nilifikiri yupo vile’
Hii ni hulka ya binadamu yeyote yule na hata kuhusu Mungu tunayehubiriwa na kwa kuwa hatujawahi kumona , nina hakika kila mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu yupo anapata picha Fulani ya Jinsi Mungu alivyo, na hiyo picha ni Tofauti kwa kila binadamu, picha hapa simaanishi uwezo wa Mungu kwa kuwa uwezo wa Mungu tunaweeza kuu feel ( hisi)kutokana na mambo ambayo anayatenda kwenye Maisha yetu ya kila siku.
Au pia mtu akisikia jina au habari za mji fulani kwa mfano SONGEA, kwa yule ambaye hajawahi kufika songea ni lazima atapata picha Fulani kichwani mwake, Kwmba ni Lazima kutakuwa na barabara za Vumbi kila sehemu, kuna wanaume weupe tu kama Mapunda N.K sasa siku akifika songea na kukuta kuna Rami barabara na mitaa yote ‘’ aaaaa Kumbe ndiyo kulivyo’Mimi nilifikiri papo vile.aaa kumbe kuna wanaume Weusi N.K
Sasa hizo picha zote kwa namna yoyote ile hazichukui Nafasi ya hivyo vitu kwa uhalisia wake, Miji, au watu husika, Ingawa zinawakilisha vitu hivyo kwa binadamu husika. Na hata picha za mnato kwa mfano hazichukui Nafasi ya mtu husika, kwani mtu husika anabaki kama alivyo na picha yake inabakia kama kiwakilishi tu cha muhusika.
Leo hii hatuwezi kuchukua picha ya mchazeji kama Fiston Mayele na kusema huyu ndiyo Mayele halisi.
SASA NAENDELEA NA SWALI NA MAJIBU YA MSINGI.
Jibu la Msingi ni HAPANA. Nitaeleza ni kwanini nasema wakatoliki hatuabuu sanamu, na labda tujiulize kwanza maswali yafuatayo ;
1.Je Mungu anachukia Kila sanamu ?
Jibu lake ni kwamba HAPANA, Mungu hachukii kila sanamu kwani hata yeye mwenyewe katika nafasi mbalimbali aliwahi kuagiza matumizi ya sanamu, nitakupeni mifano michache katika mingi, Katika agano la Kale tunaona kwamba Mungu alimuagiza Musa akatengeneze sanamu na kuziweka mahali ambapo Mungu atakuwa anazungumza naye na kumpa maagizo mbalimbali, tunasoma hilo katika kitabu cha kutoka 25 :10-22.
Pia kama mnakumbuka wakati wana waisrael walipokuwa Jangwani na baada ya kumnung ‘unikia Mungu,naye aliwaadhibu kwa kuwaletea nyoka wenye sumu waliwauma na watu wengi walikufa. Lakini baada ya Musa kuwaombea mshamaha kwa Mungu Naye Mungu alimuagiza atengeneze Nyoka wa shaba na kumtundika juu ya mti, na kila aliyeng’atwa na wale nyoka wenye sumu alipokwenda kumtazama yule nyoka wa shaba alipona baada ya kufanya hivyo( Hesabu 21 :4-9) sasa hapo tunaweza kujifunza kwamba aliyekuwa anaponya watu siyo ile Sanamu ya nyoka badala yake ni Mungu mwenyewe alikuwa anawaponya.
2.Je ni sanamu gani /zipi zinamchukiza Mungu
Mungu anachukia kila aina ya Sanamu ambayo inachukua nafasi yake, hapo namaanisha kila aina ya sanamu inayoabudiwa kama ndiyo Mungu mwenyewe , hiyo inamchukiza Mungu, Kwani Mungu yupo peke yake na kila kitu kinachochukua nafasi yake kuwa ndio Mungu anakichukia,kama mnakumbuka katika kitabu cha kutoka tunasoma kwamba wakati Musa alipokuwa mlimani sinai kupokea Amri za Mungu, alikaa huko kwa muda mrefu sana na waisrael imani ikawatoka, kiasi kwamba wakaamua kujitengenezea sanamu na kusema kwamba hiyo sanamu ya Ngo’mbe ndiyo Mungu wao aliyewatoa Misri na ndiye atakayewaongoza huko waendako.
Hivyo hii sanamu ni Lazima imchukize Mungu kwa kuwa inachukua nafasi ya Mungu, na siyo kwamba anawakilisha uwepo wa Mungu wa Kweli.Nenda kasome kitabu cha kutoka sur aya 32, isome yote.
3.Pia Mungu anakataza sanamu na kuziabudu na kuzitumikia, hapo ni sawa na kusema sanamu zimechukua nafasi ya Mungu. Hivyo sanamu zinakatazwa kama zinaabudiwa na kutukuzwa na kutumikiwa kama walivyofanya waisrael kama yule ndama, walimfanya kuwa ndiyo Mungu wao na walikuwa tayari kumuabudu na kumtumikia. Kwa kushindilia hoja hii soma kitabu cha kumbukumbu la Torati 4 :15 – 20)
4.Wakatoliki hatifanyi nini ?
Wakatoliki hatuabudu sanamu na kwa kuwa hakuna siku wala mahala ambapo tumewahi kufanya wala kusema hizi sanamu ndiyo Mungu wetu na kwamba tunaziabudu au tutaziabudu na kuzitii na kuzitumikia, hatujawahi kufanya hivyo na sidhani kama itatokea.
Tunaamini kwa Mungu Mmoja kama tunavyosali katika kanuni ya Imani yetu, na hakuna sanamu hata moja iliyowahi kupewa heshima kama hiyo.
NARUDIA TENA KWAMBA HATUFANYI KAMA WALIVYOFANYA WAISRAEL KULE JANGWANI KWA ILE SANAMU YA NDAMA.NDIYO KUSEMA HATUABUDU SANAMU.
5.Ijumaa kuu wakatoliki tunafanya nini ?
Katika Ibada ya ijumaa kuu kuna kipengele kinaitwa cha kuheshimu Msalaba.Mara nyingi huwa unatumika msamiati kuabudu msalaba.Lakini je kinachofanyika pale ni kitu gani hasa ? kwa mtu anayefuatilia vyema ibada hiyo atakumbuka kwamba kabla ya zoezi la kubusu msalaba halijaanza kiongozi wa ibada husema mara tatu maneno yafuatayo ‘’ HUU NI MTI WA MSALABA, AMBAO WOKOVU WA ULIMWENGU UMETUNDIKWA JUU YAKE’ na watu wote tunaitikia/ tunajibu ‘’ NJOONI, NJOONI, NJOOONI TUUABUDU’.
Sasa hapo kama kweli umeelewa tunachoabudu ninini ? mti wa msalaba au uokovu uliotundikwa juu yake ? Sasa wataalamu wa theologia wanatueleza kuwa tunaabudu wokovu juu ya msalaba, kwani kwa kufanya hivyo siyo kwa sababu ya ule msalaba, kwani kama kufa msalabani hata wakosaji wote katika jamii ya kiyahudi waliuawa kwa kutundikwa msalabani.
Hivyo basi tuna alikwa kuabudu wokovu uliotundikwa juu ya msalaba, na huo wokovu ninini basi ? Jibu ni YESU KRISTU na huyu Yesu Kristu ni nani ? katika katekisimu katoliki tunaambiwa kwamba Yesu Kristu ni Nafsi ya pili ya Mungu na ni Mungu sawa na Baba, hivyo kusema Yesu ni Mungu, na wokovu wetu ni Mungu ndiyo kusema TUNAMUABUDU MUNGU.
Na kwa wale ambao hawajawahi kuwa makini sehemu hii ya ibada ya ijumaa kuu nawaalika kuwa makini katika ibada ya mwaka huu na wale ambao wanasema kwamba ijumaa tunaabudu sanamu nao nawaalika wakafuatilie kipengele hiki vizuri. Ni hapo tu watapata majibu ya maswali yao na mashaka yao yatakwisha.
Na kuna wakati watani zetu huwa wanasema kwanini sisi wakatoliki tunaweka picha ya mtu katika misalaba yetu. Sisi huwa tunaweka picha ya Yesu katika misalaba yetu. Hao wanaouliza hivyo nao pia wanatumia misalaba lakini haina hiyo picha kwakuwa wanasema kwa kufanya hivyo watakuwa wanaabudu sanamu, lakini picha ya msalaba kwao siyo tatizo.
Hapo napenda kuwaeleza kwamba kuwa sisi wakatoliki tumeona kuwa na picha ya msalaba haitoshi kwani kitu muhimu ni kupata picha halisi ya Jinsi Yesu alivyokufa Msalabani, ndiyo maana tunaongeza na mtu pale msalabani.Kitu cha muhimu hapo ni msalaba wa Yesu na siyo tu msalaba PEKE YAKE .
Kwani msalaba ulioleta wokovu ni msalaba wa Yesu tu,kama suala lingekuwa ni msalaba tu kwani hata wale wanyanganyi waliuawa msalabani, na misalaba yao haikuleta wokovu kwa dunia.Ndiyo maana tunajazia na hiyo kitu ili kutoa picha halisi ya Yesu msalabani kusudi tunapoutazama msalaba wa Yesu tupate picha halisi ya kifo chake msalabani.
Bada ya kusema hayo basi naamini utakuwa ume imarika kiimani na hakuna mtu atakubabaisha juu ya hili suala la msalaba na masakramenti yote na tuwaeleweshe wale ambao hawaelewi kwa upendo na utulivu mantiki na liturujia nzima ya uwapo wa sanamu kwa wakatoliki