Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Moja wapo ya sifa ya dini ni Universality. Sasa dini Ipo kwa Wapare, wajita , wakerewe na wajaluo tuu , hiyo ni prima facie evidence kuwa Kuna tatizo. Wao waendelee kucheza maparedi Yao kwenye makanisa Yao na kuzishika amri za kale za kiyahudi ambazo kimsingi ni Mila zaidi zilizopo kwenye agano la kale ambazo Yesu alizi ove rule Haina shida lakini wasiumize kichwa kwa Imani isiyowahusu
alafu hayo mapared hayana maana
Unaposema kutawala Dunia, una maana gani? Kushikilia vyombo vya dola na Serikali zote Duniani.

Mpaka sasa Kanisa Katoliki lipo mahali pote Duniani.

Catholic maana yake kitu kilichoenea Duniani kote. Pamoja na misukosuko mingi katika vipindi mbalimbali, ikiwa ninpamoja na kuwaua mitume wote (isipokuwa mtume Yohana aliyekufa kifo cha kawaida), Kanisa Katoliki lilizidi kuenea na linazidi kuenea.

Jana usiku, tumepokea wakristo wapya 7 toka familia za Kiislam, siyo kwa sababu ya kusimama barabarani na kuhubiri kwa kelele au kuutusi uislam, au kulitusi dhehebu lolote.

Wanaoutukana ukatoliki, waendelee lakini hawataleta athari yoyote. Yesu alimwambia Simon, 'wewe ni Petera (rock) na juu ya hiyo petera nitalijenga Kanisa langu, na wala milango ya jehanamu haitalishinda". Kama Kanisa Katoliki siyo la Kristo, kuna siku litapotea, lakini kama ni la Kristo, wazidi kutukana, lakini litazidi kustawi zaidi siku hadi siku hata kama kutakuwa masaibu ya namna gani.
namaanisha kutawala dunia kama ilivyotawala roman empire....simaanishi kuenea maana kama kuenea duniani sisi islamic ndo tupo kila mahali na n mara 3 ya idafi ya katolic wordwide
 
Usipoteze muda kubishana na mjinga. Kiimani unatakiwa kumwombea.

Paulo aliyekuwa kiongozi mkuu wa kulihujumu Kanisa la Kristo alikuja kuwa mtume wa Kristo aliyefanya kazi kubwa sana. Hata huyo unayemsema, usishangae siku nyingine akasimama mbele yako akikuhubira mafundishobya kweli kuliko hayo ya upotofu anayoyatoa sasa.

Ila kama wewe unayumba kwa sababu ya kutolijua neno la Mungu, jibidishe kuyajua maandiko:

Kwa ufupi kabisa, rejea hapa:

1) kwa nini Kristo aliuawa?
JIBU: Kwa sababu ya kutotii sheria.

2) Sheria gani
JIBU: Sheria ya Musa, yaani kumbukumbu la torati.

3) Sheria gani ilikuwa kuu kuliko zote kwenye kumbukumbu la torati?
JIBU: Sheria ya sabato

Yesu kutozingatia mafundisho ya mafarisayo kuhusiana na sabato, ndiyo mwanzo wa chuki za mafarisayo na makuhani dhidi ya Kristo. Tena wakasema wazi kuwa, kama angekuwa mwana wa Mungu angeitii Sabato. Naye akawaambia wazi kuwa yeye ni mkuu kuliko sabato. Yeye ni bwana wa Sabato. Kwa nini uiabudu siku ya Sabato badala ya kumwabudu yeye aliye bwana wa Sabato?

Kwa hiyo Kristo aliuawa kwa kutoitii sheria. Kwa kutoitii sheria za kumbukumbu la torati, ambako sheria kuu ni utii wa sabato. Kwa sababu kutokutii sabato lisingekuwa kosa kubwa la kuhukumiwa kifo na Pilato kiongozi mwakilishi wa mfalme wa Roma, wakamtengenezea kesi ya kubumba ya uchochezi kuwa anawachochea watu wasilipe kodi kwa mfalme Kaizari wa Roma.

Paulo anasema wazi Kristo alihukumiwa kwa sababu ya kutoitii sheria, akayashinda mauti. Baada ya ushindi wa Kristo yaani kuyashinda mauti, sisi tulioshinda na kufufuka na Kristo, tukirudi kuitumikia sheria, basi kifo cha Kristo ni bure.

Mkristo hustahili kuiabudu sabato, au kuiabudu siku, mwabudu Bwana wa Sabato katika kweli na haki.
Sasa kwa Nini makanisani vinetengenezwa vinyago vya kuabudu.

Yaani, unakutana na bonge la sanamu na watu wanalipipigia magoti. Mtu anaweza Toka zake misha kwenda kanisani kupigia magoti Sana. Hiyo sio sio Ibada ya kweli kama unavyotaka mwenyewe.
 
Kumbuka Yesu hakuanzisha kanisa ila mitume ndio walioanzisha kanisa. Likaenezwa kwa upanga.
.
 
Kuna namna waeza tupa ushahid juu ya hili? Pia kama ni hivyo inamaana sote tunaabud cku ambazo ni mapokeo ya wanadam? Kama ndivyo je kuna mweny haki wa kumwambia mwenzake sabato ni cku flan?
Mtume Paulo anasema siku siyo muhimu kwa maana hakuna siku ambayo Mungu aliiumba iliyo ya dhambi na nyingine ya utakatifu.

Alisema kuwa anayepumzika siku fulani kwaajili ya utukufu wa Mungu anafanya vyema, lakini asimlazimishe na mwingine kufanya vivyo hivyo. Ni hivyo hivyo kwa vyakula.

5 One person considers one day more sacred than another; another considers every day alike. Each of them should be fully convinced in their own mind. 6 Whoever regards one day as special does so to the Lord. Whoever eats meat does so to the Lord, for they give thanks to God; and whoever abstains does so to the Lord and gives thanks to God. 7 For none of us lives for ourselves alone, and none of us dies for ourselves alone. 8 If we live, we live for the Lord; and if we die, we die for the Lord. So, whether we live or die, we belong to the Lord. 9 For this very reason, Christ died and returned to life so that he might be the Lord of both the dead and the living.
 
alafu hayo mapared hayana maana

namaanisha kutawala dunia kama ilivyotawala roman empire....simaanishi kuenea maana kama kuenea duniani sisi islamic ndo tupo kila mahali na n mara 3 ya idafi ya katolic wordwide
Wakristo 2.4 billion

Muslims wapo 1.9 billion

Kwa hiyo 2.4 billion ni ndogo kuliko 1.9 billion?

Wakatoliki pekee ni 1.3 billion

Hivi ukizidisha 1.3 mara 3 unapata 1.9? Hesabu za wapi hizo?

largest, with more than two billion followers. Christianity is based on the life and teachings of Jesus Christ and is approximately 2,000 years old.

Kama hufahamu, chukua kuanzie leo, wakristo, katika ujumla wao, ni wengi kuliko Waislam katika ujumla wao.
Na kama wakatoliki ni wachache kama umavyosema, itawezekana vipi hao watu wachache wawatawale walio wengi kupindukia?

Tenganisheni ukweli na hadithi.
 
Wakristo 2.4 billion

Muslims wapo 1.9 billion

Kwa hiyo 2.4 billion ni ndogo kuliko 1.9 billion?

Wakatoliki pekee ni 1.3 billion

Hivi ukizidisha 1.3 mara 3 unapata 1.9? Hesabu za wapi hizo?

Na kama wakatoliki ni wachache kama umavyosema, itawezekana vipi hao watu wachache wawatawale walio wengi kupindukia?

Tenganisheni ukweli na hadithi.
roman empire ilivyotawalandunia inaaman kipindi kile warumi walikuwa weng kuliko mataifa mengne yote au ??
 
JE WAKATOLIKI TUNAABUDU MSALABA?
Kabla sijajibu swali la Msingi naomba nitoe utangulizi kidogo

Kwa hulka yake binadamu ni kiumbe ambaye ana tabia ya ku imagine karibu kila kitu ambacho anakiwaza au kukisikia na huwa anajaribu kutengeneza picha Fulani ya kitu hicho, kwa mfano mtu anaposikia jina la mtu Fulani ambaye hajawahi kumuona…… kwanza kabisa atatengeneza picha Fulani labda huyo jamaa ni mrefu, Mnene na kadhalika, na siku akimuona utamsikia akisema ‘aaaaa kumbe yupo hivi mimi nilifikiri yupo vile’

Hii ni hulka ya binadamu yeyote yule na hata kuhusu Mungu tunayehubiriwa na kwa kuwa hatujawahi kumona , nina hakika kila mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu yupo anapata picha Fulani ya Jinsi Mungu alivyo, na hiyo picha ni Tofauti kwa kila binadamu, picha hapa simaanishi uwezo wa Mungu kwa kuwa uwezo wa Mungu tunaweeza kuu feel ( hisi)kutokana na mambo ambayo anayatenda kwenye Maisha yetu ya kila siku.

Au pia mtu akisikia jina au habari za mji fulani kwa mfano SONGEA, kwa yule ambaye hajawahi kufika songea ni lazima atapata picha Fulani kichwani mwake, Kwmba ni Lazima kutakuwa na barabara za Vumbi kila sehemu, kuna wanaume weupe tu kama Mapunda N.K sasa siku akifika songea na kukuta kuna Rami barabara na mitaa yote ‘’ aaaaa Kumbe ndiyo kulivyo’Mimi nilifikiri papo vile.aaa kumbe kuna wanaume Weusi N.K

Sasa hizo picha zote kwa namna yoyote ile hazichukui Nafasi ya hivyo vitu kwa uhalisia wake, Miji, au watu husika, Ingawa zinawakilisha vitu hivyo kwa binadamu husika. Na hata picha za mnato kwa mfano hazichukui Nafasi ya mtu husika, kwani mtu husika anabaki kama alivyo na picha yake inabakia kama kiwakilishi tu cha muhusika.

Leo hii hatuwezi kuchukua picha ya mchazeji kama Fiston Mayele na kusema huyu ndiyo Mayele halisi.
SASA NAENDELEA NA SWALI NA MAJIBU YA MSINGI.
Jibu la Msingi ni HAPANA. Nitaeleza ni kwanini nasema wakatoliki hatuabuu sanamu, na labda tujiulize kwanza maswali yafuatayo ;
1.Je Mungu anachukia Kila sanamu ?
Jibu lake ni kwamba HAPANA, Mungu hachukii kila sanamu kwani hata yeye mwenyewe katika nafasi mbalimbali aliwahi kuagiza matumizi ya sanamu, nitakupeni mifano michache katika mingi, Katika agano la Kale tunaona kwamba Mungu alimuagiza Musa akatengeneze sanamu na kuziweka mahali ambapo Mungu atakuwa anazungumza naye na kumpa maagizo mbalimbali, tunasoma hilo katika kitabu cha kutoka 25 :10-22.

Pia kama mnakumbuka wakati wana waisrael walipokuwa Jangwani na baada ya kumnung ‘unikia Mungu,naye aliwaadhibu kwa kuwaletea nyoka wenye sumu waliwauma na watu wengi walikufa. Lakini baada ya Musa kuwaombea mshamaha kwa Mungu Naye Mungu alimuagiza atengeneze Nyoka wa shaba na kumtundika juu ya mti, na kila aliyeng’atwa na wale nyoka wenye sumu alipokwenda kumtazama yule nyoka wa shaba alipona baada ya kufanya hivyo( Hesabu 21 :4-9) sasa hapo tunaweza kujifunza kwamba aliyekuwa anaponya watu siyo ile Sanamu ya nyoka badala yake ni Mungu mwenyewe alikuwa anawaponya.

2.Je ni sanamu gani /zipi zinamchukiza Mungu
Mungu anachukia kila aina ya Sanamu ambayo inachukua nafasi yake, hapo namaanisha kila aina ya sanamu inayoabudiwa kama ndiyo Mungu mwenyewe , hiyo inamchukiza Mungu, Kwani Mungu yupo peke yake na kila kitu kinachochukua nafasi yake kuwa ndio Mungu anakichukia,kama mnakumbuka katika kitabu cha kutoka tunasoma kwamba wakati Musa alipokuwa mlimani sinai kupokea Amri za Mungu, alikaa huko kwa muda mrefu sana na waisrael imani ikawatoka, kiasi kwamba wakaamua kujitengenezea sanamu na kusema kwamba hiyo sanamu ya Ngo’mbe ndiyo Mungu wao aliyewatoa Misri na ndiye atakayewaongoza huko waendako.

Hivyo hii sanamu ni Lazima imchukize Mungu kwa kuwa inachukua nafasi ya Mungu, na siyo kwamba anawakilisha uwepo wa Mungu wa Kweli.Nenda kasome kitabu cha kutoka sur aya 32, isome yote.

3.Pia Mungu anakataza sanamu na kuziabudu na kuzitumikia, hapo ni sawa na kusema sanamu zimechukua nafasi ya Mungu. Hivyo sanamu zinakatazwa kama zinaabudiwa na kutukuzwa na kutumikiwa kama walivyofanya waisrael kama yule ndama, walimfanya kuwa ndiyo Mungu wao na walikuwa tayari kumuabudu na kumtumikia. Kwa kushindilia hoja hii soma kitabu cha kumbukumbu la Torati 4 :15 – 20)

4.Wakatoliki hatifanyi nini ?

Wakatoliki hatuabudu sanamu na kwa kuwa hakuna siku wala mahala ambapo tumewahi kufanya wala kusema hizi sanamu ndiyo Mungu wetu na kwamba tunaziabudu au tutaziabudu na kuzitii na kuzitumikia, hatujawahi kufanya hivyo na sidhani kama itatokea.

Tunaamini kwa Mungu Mmoja kama tunavyosali katika kanuni ya Imani yetu, na hakuna sanamu hata moja iliyowahi kupewa heshima kama hiyo.
NARUDIA TENA KWAMBA HATUFANYI KAMA WALIVYOFANYA WAISRAEL KULE JANGWANI KWA ILE SANAMU YA NDAMA.NDIYO KUSEMA HATUABUDU SANAMU.

5.Ijumaa kuu wakatoliki tunafanya nini ?
Katika Ibada ya ijumaa kuu kuna kipengele kinaitwa cha kuheshimu Msalaba.Mara nyingi huwa unatumika msamiati kuabudu msalaba.Lakini je kinachofanyika pale ni kitu gani hasa ? kwa mtu anayefuatilia vyema ibada hiyo atakumbuka kwamba kabla ya zoezi la kubusu msalaba halijaanza kiongozi wa ibada husema mara tatu maneno yafuatayo ‘’ HUU NI MTI WA MSALABA, AMBAO WOKOVU WA ULIMWENGU UMETUNDIKWA JUU YAKE’ na watu wote tunaitikia/ tunajibu ‘’ NJOONI, NJOONI, NJOOONI TUUABUDU’.
Sasa hapo kama kweli umeelewa tunachoabudu ninini ? mti wa msalaba au uokovu uliotundikwa juu yake ? Sasa wataalamu wa theologia wanatueleza kuwa tunaabudu wokovu juu ya msalaba, kwani kwa kufanya hivyo siyo kwa sababu ya ule msalaba, kwani kama kufa msalabani hata wakosaji wote katika jamii ya kiyahudi waliuawa kwa kutundikwa msalabani.

Hivyo basi tuna alikwa kuabudu wokovu uliotundikwa juu ya msalaba, na huo wokovu ninini basi ? Jibu ni YESU KRISTU na huyu Yesu Kristu ni nani ? katika katekisimu katoliki tunaambiwa kwamba Yesu Kristu ni Nafsi ya pili ya Mungu na ni Mungu sawa na Baba, hivyo kusema Yesu ni Mungu, na wokovu wetu ni Mungu ndiyo kusema TUNAMUABUDU MUNGU.

Na kwa wale ambao hawajawahi kuwa makini sehemu hii ya ibada ya ijumaa kuu nawaalika kuwa makini katika ibada ya mwaka huu na wale ambao wanasema kwamba ijumaa tunaabudu sanamu nao nawaalika wakafuatilie kipengele hiki vizuri. Ni hapo tu watapata majibu ya maswali yao na mashaka yao yatakwisha.

Na kuna wakati watani zetu huwa wanasema kwanini sisi wakatoliki tunaweka picha ya mtu katika misalaba yetu. Sisi huwa tunaweka picha ya Yesu katika misalaba yetu. Hao wanaouliza hivyo nao pia wanatumia misalaba lakini haina hiyo picha kwakuwa wanasema kwa kufanya hivyo watakuwa wanaabudu sanamu, lakini picha ya msalaba kwao siyo tatizo.

Hapo napenda kuwaeleza kwamba kuwa sisi wakatoliki tumeona kuwa na picha ya msalaba haitoshi kwani kitu muhimu ni kupata picha halisi ya Jinsi Yesu alivyokufa Msalabani, ndiyo maana tunaongeza na mtu pale msalabani.Kitu cha muhimu hapo ni msalaba wa Yesu na siyo tu msalaba PEKE YAKE .

Kwani msalaba ulioleta wokovu ni msalaba wa Yesu tu,kama suala lingekuwa ni msalaba tu kwani hata wale wanyanganyi waliuawa msalabani, na misalaba yao haikuleta wokovu kwa dunia.Ndiyo maana tunajazia na hiyo kitu ili kutoa picha halisi ya Yesu msalabani kusudi tunapoutazama msalaba wa Yesu tupate picha halisi ya kifo chake msalabani.

Bada ya kusema hayo basi naamini utakuwa ume imarika kiimani na hakuna mtu atakubabaisha juu ya hili suala la msalaba na masakramenti yote na tuwaeleweshe wale ambao hawaelewi kwa upendo na utulivu mantiki na liturujia nzima ya uwapo wa sanamu kwa wakatoliki
Nmekusoma mkuu
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
mwache tu ajifurahishe
 
roman empire ilivyotawalandunia inaaman kipindi kile warumi walikuwa weng kuliko mataifa mengne yote au ??
Usiwe unakariri bila kutafakari. Unaielewa Dunia ya wakati wa utawala wa Urumi?

Roman empire ilihusisha nchi za Ulaya, North America na kwa Mashariki iliishia tu Uturuki. Kwa hiyo, kiuhalisia haikutawala Dunia nzima.

Hivi unaamini kwa sababu Uingereza, Ufaransa, Spain, na Belgium kwa vile zilitutawala wakati huo, zitakuja kututawala tena kwa vile tu kwa sababu zamani zilitutawala?

Ufahamu kuwa kuna matukio hutokea mara moja tu kutokana na hali ya nyakati, wala hayawezi kutumika kama reference ya kutokea tena.

Inaonekana huujui kabisa ukatoliki. Ukatoliki siyo kama uislam, haujihusishi na mambo ya tawala za nchi. Mafundisho ya Kanisa ni juu ya ufalme wa mbinguni, na si ufalme wa Ulimwengu. Hayo ndiyo mafundisho ya ukristo.
 
Usiwe unakariri bila kutafakari. Unaielewa Dunia ya wakati wa utawala wa Urumi?

Roman empire ilihusisha nchi za Ulaya, North America na kwa Mashariki iliishia tu Uturuki. Kwa hiyo, kiuhalisia haikutawala Dunia nzima.

Hivi unaamini kwa sababu Uingereza, Ufaransa, Spain, na Belgium kwa vile zilitutawala wakati huo, zitakuja kututawala tena kwa vile tu kwa sababu zamani zilitutawala?

Ufahamu kuwa kuna matukio hutokea mara moja tu kutokana na hali ya nyakati, wala hayawezi kutumika kama reference ya kutokea tena.

Inaonekana huujui kabisa ukatoliki. Ukatoliki siyo kama uislam, haujihusishi na mambo ya tawala za nchi. Mafundisho ya Kanisa ni juu ya ufalme wa mbinguni, na si ufalme wa Ulimwengu. Hayo ndiyo mafundisho ya ukristo.
hapo tuweke nukta kwamba roman empire haikutawala dunia nzima?? ubishi usio namaana haufai . lkn kaa ukijua ROMAN inahatia ya kuua mamilion
 
Tukitumia lunar calendar ambayo Waisraeli wa Zamani waliyoitumia Kwa ajili ya kuhesabu siku na mwezi na mwaka, utakuja kugundua Sabato waliyopumzika haikuwa Jumamosi, inabadilikq kutokana na mwandamo wa mwezi kwa kalenda iliyopo.
Kalenda hii ilianzishwa na Papa Gregory ndo wasabato wanaitumia kujustify kuwa Sabato ni Jumamosi na kutumia Maandiko ya Kardinal Gibbons ila ukweli upo kwenye lunar calendar.
Ukiniambia Wayahudi wa Sasa wanapumzika Jumamosi nitakuambia wale ni Ashkenazim , Kuna uwezekano mkubwa hawana asili ya Kiebrania .
Hii elimu aliwahi nipa mtu mmoja kwa urefu sana nikabisha next time kuna mtu akanipa humu humu nikafatilia nikaanza kuielewa hadi walivyokuwa wana hesabu nikagundua mengi sana.
 
Tenganisha kati ya Roman Empire na Kanisa la Roman Catholic.
iliyona hatia ya kuua mamilion wasio na hatia ktk karne ya 16 17 na 18 ni roman katholic na sio roman empire nafikir nmetenganisha tayar
 
Unavyopiga magoti mbele ya sanamu ya bikira Maria unaheshimu au unaabudu?
Hakuna ibada ya namna hii katika ukatoliki.
Kupiga magoti kwa image ambaye umwakilisha bikra Maria ni ishara ya heshima kwake kwa maana ni mzazi wa Yesu Kristu.

Katika kanisa katoliki ibada zipo za aina mbali mbali kama vile sala,rozari,njia ya msalaba n.k.Misa ikiwa ndio ibada kuu ambayo huwakutanisha waumini wengi sehemu moja.

Ukatoliki unaelekeza yakuwa Mungu peke ndiye wa kuabudiwa na ukitambua mitume,watakatifu,na malaika.
 
Kwa asilimia kubwa kwa baadhi ya hao wahubiri wa SDA, mafundisho yao ni kulishambulia Kanisa Katoliki kama vile wameambiwa kuwa watafika mbinguni kwa kufanya mashambulizi hayo.

Lakini wapo wasabato wazuri kabisa ambao hawana muda na hayo mafundisho yao yasiyo na msingi wa neno la Mungu.

Kuna wakati kulikuwa na ujenzi wa Kanisa Katoliki, nilishangaa Kanisa la SDA lilituma wawakilishi wao, na wakatoa mchango wa fedha milioni 5. Na kabla ya harambee, walishiriki ibada ya pamoja toka mwanzo hadi mwisho.
Chief, nakubaliana nawe. Ila Kuna mafundisho yao mengine wanaamini siku ya mwisho kanisa la roman catholic wataungana na USA kuwatesa wasabato kwa kuwalazimisha kusali jumapili. Msingi. Wa mafundisho yao nikulishambulia kanisa katoliki
 
Sawa yeye ameongea hivyo na akaona yuko sahihi na mimi pia nataka nijue kutoka kwake,Hiyo Jumamosi anayosema ndio sabato kaitoa kwenye kalenda ipi?ya kirumi,ya waislam au wayahudi,kalenda kutoka mbinguni au(ambayo sidhani kama ipo),kalenda ya wamisri,wahindi n.k

Hizo ibada za sanamu katika ukatoliki ni zipi? maana nachojua sisi ibada yetu imekuwa ni misa ambayo hufanyika siku zote za wiki(Jumapili ikiwa ni siku ambayo waumini ufika kwa namba kubwa kanisani).Ibada hii ya misa imegawanyika sehemu kuu mbili:Lituriji
img_1_1662670834151.jpg
a ya neno na liturijia ya ekaristi(sasa hapa sanamu ni lipi linaloabudisanamu hili hapawa?)
a
 
Back
Top Bottom