Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Mimi ni mlutheran , lakini watu kupingana na taasisi ya ukatoliki yenye zaidi ya miaka 2000+ ni ujinga kwa haya madhehebu ambayo hayana hata 300 years.. ni sawasawa na kujilisha upepo halafu sijawahi bahatika kusikia kiongozi wa katolik anatoka hewani na kuanza kujibishana na Hawa wenye dini zao. Hata ibada za katolik ni nadra sana kukuta wanapondea dini za wengine.
Huu ni wakati wa sisi watu weusi (Africans) kufikiria mara mbili mbili jinsi ya kuenenda na dini tulizoletewa badala ya kupingana kwa ajili yake.
Dini zote zilikuwa/zina na lengo moja dhidi wafuasi wake nalo ni kuwaondolea fikra za udadisi ili wafuate kama kondoo.
 
Labda nami niweke neno kdg.. je siku ya sabato ya bwana ni lini? Kama ni jmos au jpili bas naomba aya toka kweny biblia. Pia kama unaweza muuliza huyo mchungaj ingekua heri atupe majibu hayo, lingine... Ni nani aliezipa majina cku tulizonazo? Maana kweny maandiko hazijaandwa jmos au jpili!!
Una uhakika kwenye biblia jumapili haijatajwa ni siku gani mkuu????
 
Mambo ya kiimani yanahitaji sana ufunuo wa macho na utambuzi (akili) ya imani.
1. Je, Sanamu ni nini? Je ni ya nani?
2. Je, hakuna vitu vingine vingi vyenye hadhi ya Sanamu vilivyo amriwa vitengenezwe na kuweka sehemu fulani fulani kwenye hekalu la Bwana!?
3. Je, kuabudu ni kufanya nini?
4. Je, ni tendo la kiroho ama unaweza kuliona hata kwa macho?
5. Je, wanapoabudu wanatamka maneno gani?
6. Je, kuna mtu aliwahi kwenda mbinguni na kurudi kuthibitisha kuwa watu wa dini fulani hawapo kule waliojazana ni watu wa dini fulani?

NB: Si Kila mtu anaweza kuisoma Biblia na kuielewa! All in all ni kitabu cha rejea lakini kikubwa ni imani na matendo ya mtu dhidi ya binadamu!
 
Huu ni wakati wa sisi watu weusi (Africans) kufikiria mara mbili mbili jinsi ya kuenenda na dini tulizoletewa badala ya kupingana kwa ajili yake.
Dini zote zilikuwa/zina na lengo moja dhidi wafuasi wake nalo ni kuwaondolea fikra za udadisi ili wafuate kama kondoo.
Umenena vizuri kabisa...
Dini nyingi ni conspiracy na elite capture!
Kuna watu wananufaikamo sana!
Dini haijengi shule, hospitali, miradi ya kijamii wao kazi yao kuhubiri mitafaruko na chuki dhidi ya wengine!
Kwa waganga wao! Kwa ushirikina wao! Kwa uasherati wao! Kujikweza kujitenga na kujiona bora wao!
Yaani maisha ya hapa duniani wanataka waishi kivyao vyao tu.
Wakati amri iliyokuu ni UPENDO!
 
Pale mnapoenda kuziinamia na kuzibusu sanamu kwenye majengo yenu ya ibada, ndiyo shida inapoanzia.
Unafahamu Wayahudi walifanya nini kwa nyoka wa shaba, au kwenye sanduku la Agano?

Tatizo watu wanasoma juu juu biblia hata hawaelewa content. Hivi ukisimama bendera inapopandishwa ina maana unaiabudu bendera? Hivi bendera si kitambaa tu, kinaweza kukufanyia nini?

Inapata thamani kutokana na pale unapojua inawakilisha kitu gani.

Hata noti yako ya sh 10,000 si karatasi tu, ina nini cha pekee? Inawakilisha tu ile thamani ya mali mliyokubaliana. Ndiyo maana hiyo karatasi inaweza kuwa kama takataka tu ukiipeleka mahali ambapo haifahamiki uwakilishi wake wa thamani ya mali. Ni sawa, leo hii unyanyuliwe hapa, ukawekwe katikati ya msitu wa Amazon, usipatiwe chakula wala maji, usipewe simu wala chombo chochote cha usafiri lakini pembeni uwekewe mabag makubwa 10 ya noti za sh 10,000. Utajiona ni tajiri au maskini usiye na msaada?
 
Nimewahi kusikia hayo mafundisho, yao, halafu nashangaa na waumini wao wanaamini. Mara waseme namba 666 au 616 iliyokuwa ikimaanisha mfalme Kaisar Nero, kuwa eti ni papa.

Nadhani wanazidi kulichokonoa Kanisa Katoliki baada ya kuona huo unabii wao wa Kanisa Katoliki kuwalazimisha kusali Jumapili, hautimii.

Walisema mwisho wa Dunia utakuwa mwaka 1844, haikuwa.

Wamesema Kanisa Katoliki litawalazimisha wasabato kusali Jumapili, haijatokea na hata dalili tu hazipo.

Mungu atazidi kuwaumbua wenye mafundisho ya uwongo siku zote.
Kuna wakati, we just need to be proud of our faith. Binafsi sielewi kama WASABATO NI WAKRISTO KWELI AU SOME SORT OF A CULT? Ukienda India utakuta mchana kweupe watu wanatembeza barabarani Mungu Sanamu wao ma wako comfortable. They simply do not give a damn of your opinion or queries on your faith. Wakati mwingine tunapoteza muda kutaka kukidhi au kujibu maswali ya wale wanaokosoa imani yao kuliko kujibidisha kuelewa imagine yako na kuiishi.
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
In short ni kwamba anayesema Catholics wanaabudu sanamu hana analojua. Catholics wana mambo yao mengine ambayo wanawajibika kuyatolea ufafanuzi lakini sio swala la sanamu.

Wasabato wanaamini mafundisho yaliyotolewa na Ellen G White kuliko yaliyomo kwenye Biblia na hili ni tatizo kubwa. Kwa msabato mafundisho ya Biblia yakipishana na maono ya Ellen G White basi ya Ellen yatapewa kipaumbele na ya Bible yatapewa Back seat. Wasabato wengi hawajui hili ila ndo iko hivyo.
 
Pale mnapoenda kuziinamia na kuzibusu sanamu kwenye majengo yenu ya ibada, ndiyo shida inapoanzia.
Sanamu ni ya nani? Inahusu nini kiimani?
Je, kwenye Biblia yako hakuna sehemu imeandikwa MUNGU aliagiza masanamu yatengenezwe na yawekwe sehemu fulani kimkakati?
Je, mwenye kueshimu Sanamu inayomkumbusha jambo la kiMUNGU na yule mwenye michoro au mapicha ya ajabu kwake au kwenye simu/PC yake wapo sawa?
Mngeeleweka kama mngewasema hao wakatoliki kwa kuweka masanamu ya mashetani, miungu ya ngono, majini, malaika wachafu na mapepo ya kuzimu!
Tofauti na hapo jaribuni kuwapongeza kwa kubuni utaratibu mzuri wa kuvuta tafakari na utashi wa kiMUNGU ukiwa ndani ya majengo ya ibada!
Bora mara mia niangalie msalaba au Sanamu ya Yesu inifikirishe kiimani kuliko kuhangaika na misambwanda ya mapepo yaliyotumwa kikazi sehemu za ibada!
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
RC hatuna utaratibu wa kujibizana Aisha majukwaani au makanisani. Sisi ni mtu wenye matunda.
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Imani ni metaphysical, Transcendence. Kama vile katika sacrament, tunaamini ni mwili wa Kristo. Imani ni kila kitu. Kama unaamini sacrament ni mwili wa Kristo, basi kwa imani tunaabudu msalaba kama ishara ya kukubali kuwa ukombozi wetu umetokana na msalaba. Kama unaabudu na kunaamini mninga kama mninga basi huo ni ushirikina. Soma vizuri Waebrania 11 utanielewa sana. Na kama humuelewi Paul hapo basi tena. Mnayumbishwa sana na ulokole unaojali miujiza na biashara.

Tumsifu Yesu Kristo.
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Usipoteze muda wako hangaikia mbingu yako. Hata yeye mwenyewe hilo halitampeleka mbinguni
 
Soma Luka 24 . Soma iyoooo
Hiyo Luka 24 unazungumzia cku ya kwanza ya juma wale wanawake walikwenda kaburini wakiwa na mafuta. Cjaona sehem imeandikwa jpili. NB: hakikisha aya unayonipa iwe na sehem imeandikwa jpili au jmos au alhamis!! Plz
 
YESU alifufuka siku gani unaweza nipa jibu????
 
Elezea kidogo aiseee jibu lako
Soma biblia Luka 24:01 unazungumzia kufufuka Kwa yesu, ambapo biblia inaeleza alifukufka siku ya kwanza ya juma. Na kama Leo watu wanaazimisha kufufuka Kwa yesu, ni dhahiri kuwa yesu alifufuka siku ya kwanza ya juma ambayo n jumapili, kama jumapili n siku ya kwanza ya juma. Hesabu uone siku ya 7 itakuwa lini na ni ambayo imeelekezwa na bwana katika kitabu Cha kutoka 20:08.
 
Hiyo Luka 24 unazungumzia cku ya kwanza ya juma wale wanawake walikwenda kaburini wakiwa na mafuta. Cjaona sehem imeandikwa jpili. NB: hakikisha aya unayonipa iwe na sehem imeandikwa jpili au jmos au alhamis!! Plz
Kama una biblia kiswahili Cha kisasa nayo soma Luka 24 alafu njoo unifate
 
Wengi hawafahamu na kudanganywa na Waadventista wasabato na wayahudi wa Sasa wa kule Middle East ambao asilimia kubwa walikuwa assimilated Jews.
Na inashangaza Wasabato kupingana na Wakatoliki na wanatumia kalenda ileile ya Papa Gregory kuthibitisha mambo Yao badala ya kwenda kwenye Lunar calendar, Kalenda ya Mungu wa kweli.
Unaamini yesu alifufuka siku ipi?
 
Kwa mujibu wa mafundisho ya Wasabato mwafrika mweusi haruhusiwi kwenda kuhubiri kwa wazungu ulaya ila wao wazungu ni ruksa kuja kuhubiri kwa waafrika[emoji3][emoji3][emoji3]ndiomana hao Wasabato wanaojiita Wasabato masalia walitaka kuipindisha hiyo sheria ndani ya Wasabato
Sio kweli, kuna wahubir wengi kama Pr mhando, Pr Muganda... Hawa ni wachungaji wa kisabato ambao wamehubir dunian kote. Ni watanzania hawa.
 
Kama una biblia kiswahili Cha kisasa nayo soma Luka 24 alafu njoo unifate
Ctaki biblia yenye nyongeza na interest za wanadam!! Ishi humo!! Biblia ni moja hii ya zaman bas ingeandika hizi cku tulizonazo hata kwa kiebrania then zikitafsiriwa kwa kiswahili ningekuelewa!!
 
Back
Top Bottom