Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Huwezi kujibu hoja zote za wapotoshaji.
 
Kama unatumaini KRISTO hilo ndo neno kuuu shikilia hapo hapo usiache.
Ila nilichongamua Hadi Sasa hujajua siku ambayo huyo kristo alifufuka ikiijua basi hesabu zako zitakaa vizuri sana. Umebarikiwa na naomba ubarikiwe sana
Amina mkuu 🙏
 
Timiza kwanza mengine Hilo la jmosi sijui jpili achananalo.
 
Kanisa pa Mungu ,ni kanisa la SDA, kanisan pekee Ulimwengun linalofata maelekezo ya Mungu nasio wanadamu
Mtafuteni ile kweli ambayo ni kristo, hayupo kweny makanisa bali ijueni injil ya ufalme wa MUNGU na kumkiri Kristo ni mwana wa MUNGU nae alikufa cku ya tatu akafufuka!! Hata YESU aliwakataa mafarisayo na wakuu wa makuhani ambao ni washika sabato ya bwana na kuwaita ni wanafiki!!
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Mbona ni kweli ninyi ni waabudu sanamu na watu wanajua,mnajibu nini.

Hivi unajua wakati wa Dhiki Kuu Nabii wa uongo ambaye atapewa mamlaka na Mnyama kutoka baharini(ambaye ni papal establisment), atachonga sanamu ili wasiomcha MUNGU waiabudu? So you people are idol worshipers,na uovu wenu huo mtauendeleza hata in the last days,during the Great Tribulation,so hatushangai.
 
Kuna wakati, nilipokuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha 6, ikiwa ni pamoja na masomo ya biblia, nilialikwa kwenye mkutano wa wasabato. Nilienda huko nikiwa sijui kuwa ningepewa nafasi ya kuongea.

Cha ajabu, nikawekwa kama mtu wa kujibu maswali waliyokuwa wakiyaelekeza kwa Kanisa Katoliki. Nilijibu, kwa kadiri Roho alivyoniongoza.

Wote wakawa kimya kabisa. Nilishangaa mwishowe kufuatwa na viongozi wao kuwa eti wananiomba nijiunge nao na kisha niwe mchungaji wa Kanisa lao. Nilishangaa sana, nikawauliza kuwa tangu mwanzo wamelituhumu Kanisa Katoliki kuwa limepotoka, inakuwaje tena mimi Mkatoliki naweza kuwa kiongozi wao? Hawakuwa na jibu.

Nilivyomaliza masomo yangu ya shahada ya pili, nilipofika Dar, nikaalikwa na jamaa mmoja, aliwahi kuwa mtu mkubwa kwenye ngazi ya kitaifa kwenye Serikali. Yeye ni muislam. Nikaitikia mwaliko, nikaenda. Kufika huko nikashangaa walikuwa wamejaa wasomi wa dini ya Kiislam. Pekee yangu nilitengewe kiti, huku wao wote wakiwa wameketi kwenye majamvi. Nikaanza kuulizwa mambo ya Ukristo. Sikuwa nimejipanga kwa hilo. Lakini kwa utulivu niliwajibu kadiri nilivyoweza, hata wakaishiwa swali lolote.

Nilitafakari sana kwa nini niliitwa mimi, lakini baadaye nilikuja kutambua kuwa kuna ndugu zangu, nao walikuwa wasomi wazuri kwenye elimu ya Dunia, lakini hawakuwa vizuri sana kwenye mafundisho ya kiimani. Na kuna watu walitaka kuwabadilisha wale ndugu zangu kwenda uislam, na ikaelezwa kwamba kikwazo ilikuwa mimi. Hivyo wakinibadilisha mimi, basi wale wengine watanifuata.

Nashukuru mpaka leo wote tupo katika imani yetu.

Na neno la mwisho nililowaambia wale wasomi wa dini ya Kiislam ni kwamba sisi katika Ukristo tunaamini sana katika neema. Na neema hiyo inaweza kumwangukia yeyote, na ukashangaa aliyekuwa imamu au hata mpagani, siku nyingine anaweza kuja kuwa mkristo, tena kukuzidi hata wewe uliyedhania unaujua zaidi ukristo, akawa mwalimu wako.

Kwa hiyo usighadhabike Kanisa likinenewa vibaya. Kristo pamoja na ukuu wote, na mamlaka yote, alidhalilishwa, alitukanwa, alipigwa, alivuliwa nguo, alitemewa mate, hakuhangaika na waliomtendea hayo. Alipofufuka neno lake la kwanza lilikuwa Shalom, yaani muwe na amani, nimekamilisha, msiwe na mashaka. Mkristo unatakiwa kuyaiga maisha ya Kristo. Hatushindani katika kumjua au kumwabudu Mungu. Hata anayetusi, ujue Mungu ameruhusu, asipotaka, hawezi hata kuupanua mdomo wake.
Tumsifu Yesu Kristu.!
 
Biblia n Moja, hapana biblia ya mromani Wala msabato. Kutoka 20:01 linamuelekeza mwanadam kutokuabudu miungu, msalaba na Sanam ya bikra maria ni Moja wapo
Kanunue Biblia Ya bookshop za RC utagundua hakuna biblia Moja....... RC hatuabudu msalaba wala bikira maria Tunaheshimu tuu the same way Muslims wanamuheshimu mtume pamoja na nyota na mbalamwezi.....
 
Kuna wakati hata kumtaja Yesu walikuwa wanaona shida. Na huwa hawapendi kuitwa wakristo.
Hii chai umeweka chumvi badala ya sukari mkuu
JamiiForums1161832947.jpg
 
Kanunue Biblia Ya bookshop za RC utagundua hakuna biblia Moja....... RC hatuabudu msalaba wala bikira maria Tunaheshimu tuu the same way Muslims wanamuheshimu mtume pamoja na nyota na mbalamwezi.....
Biblia hyohyo kafungue kitabu Cha Luca 24:01 kama Iko tofauti upge picha hapa tuone
 
Mtafuteni ile kweli ambayo ni kristo, hayupo kweny makanisa bali ijueni injil ya ufalme wa MUNGU na kumkiri Kristo ni mwana wa MUNGU nae alikufa cku ya tatu akafufuka!! Hata YESU aliwakataa mafarisayo na wakuu wa makuhani ambao ni washika sabato ya bwana na kuwaita ni wanafiki!!
Acha ubishi... Yesu mwenyewe anajiita Bwana wa Sabato.

Mungu mwenyewe ni msabato.

Yesu Maisha yake yoteee alitunza Sabato .

Wewe ni nani??.
 
Acha ubishi... Yesu mwenyewe anajiita Bwana wa Sabato.

Mungu mwenyewe ni msabato.

Yesu Maisha yake yoteee alitunza Sabato .

Wewe ni nani??.
Kheeee, hii kali!! Haya saw!! NB: ni heri yao waiishio amri ya bwana. But hakuna njia yoyote ya dini ya kuupata ufalme wa MUNGU zaid ya kristo. Pia Kristo alikuja dunian c kuleta dini bali waliopotea ili wafanye toba. So dini ni mpango wa mwanadam!
 
Back
Top Bottom