Aqua
JF-Expert Member
- Jul 23, 2012
- 1,657
- 1,231
Wewe kama ni msomaji wa biblia unatakiwa ujue huo mstari,Mungu anasema watu wake wanapotea kwa kukosa maarifa.Pia biblia inasema chanzo cha maarifa ni kumcha Mungu,kwa hiyo ili uwe salama unatakiwa umche Mungu.Kivipi mkuu funguka tujue maarifa gani hayo.
Na kumcha Mungu kuna vitu vingi vina ambatana na hilo,namshukuru Mungu nilichojifunza wakristo wengi wasiokuwa na bidii ya kumtafuta Mungu na kumjua yeye pamoja na njia zake watapotea.Kuna kundi kubwa hata sasa limeshapotea linahitaji neema ya Mungu.Wengi wameng'ang'ania dini za wazazi wao bila kujua kwa nini wazazi wao wako huko,kila mtu anajukumu la kuiponya nafsi yake.Ni kweli kwa kupigwa kwake Yesu sisi tumepona,lakini kuna kitu unatakiwa ufanye.
Wakristo wengi hawasomi biblia,neno la Mungu halimo moyoni mwao kwa wingi,hivyo wengi wanaishi maisha ya kuwapendezesha wanadamu na si Mungu.Mtu kudanganya haoni shida,mtu kutukana haoni shida,wadada kuvaa mavazi ya utupu hawaoni shida,roho za uzinzi zinatenda kazi sasa kwa kasi kuliko ila watu hawajui.Watu wengi wanaanguka katika uzinzi,hata watumishi wa Mungu wanaanguka,shetani si wa kuchezea ukimpa nafasi anakuharibu.Mbaya zaidi wengi tunafanya mambo lakini hatujui athari zake katika ulimwengu wa roho.
Kwenda kanisani hakumfanyi mtu aingie mbinguni,kuwa kiongozi wa dini au mtumishi wa Mungu siyo tiketi ya kuingia mbinguni kama njia zako si njema machoni pa Mungu.Wengi wataangamia,ni bora leo ukampokea Yesu ili ufanyike upya.
Wengi kwa kutaka kutokupoteza personality zao wata angamia,Yesu alisema mtu akitaka kunifuata kwanza "aikane nafsi yake,kisha jitwike msalaba wake anifuate".Kuikana nafsi si jambo dogo kama watu wanvyodhania,mtumwa huwa akatai.Ukiwa mtumwa wa kristo maana yake unatakiwa kufanya kila unacho agizwa na Bwana,this is not the case with this generation.
Tofautisha utaratibu wa dini yako au kanisa lako na utaratibu wa Mungu usichanganye hivi vitu viwili.SOMA BIBLIA utajua Mungu anataka uishi vipi,watu wanawatii viongozi wao hata kama wanayowambia wafanye yako kinyume na neno la Mungu na hii inatokana na waamini hawayajui maandiko kwa hiyo inakuwa rahisi kupotoshwa.